Nataka 50,000,000 ya pamoja, nilime heka ngapi za nyanya/viazi mviringo?

Nataka 50,000,000 ya pamoja, nilime heka ngapi za nyanya/viazi mviringo?

Tafadhali nipeni msaada wazoefu, msimu gani unafaa kwa kilimo cha mazao tajwa hapo juu,pamoja na gharama zitakazotumika kuhudumia,lengo langu ni 50M mtaji nilionao cash ni 10M ,lengo langu kuwa mkulima/mfanyabiashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu chonde chonde kilimo kinachangamoto nyingi mno hasa kwa beginner utapunwa hiyo 10M yoteee uchizike niliwahi kulima nikiwa mgeni shamba LA 1.5M per acre nilitoa 3M gharama tena mazao perishable ni hatari zaidi hivyo bora ununue mazao ukae kidogo uuze japo faida kiduchu ila afadhali Ila kama mbishi Lima acre 1 upate uzoefu ulime kwa ukaribu na wazoefu.Lima mahindi na maharagwe japo umechelewa labda next season unaweza mahindi kwa kumwagilia Ila maharage yakumwagilia sio mazur Mimi zao ambalo naona haliumizi kichwa ni mahindi na maharagwe yaani simple palilizi moja Kwisha japo mahindi siku hizi tunapiga dawa ni changamoto kwa shamba kubwa maana kila mmea inabidi ipate dawa vibarua wanaripua.
 
Kwenda sokoni bila connection ni bora uuzie shambani hivi nashangaa MTU unabeba mazao from nowhere huyo sokoni kisa kasikia sokoni bei ni sh. Kadhaa hapo katikati kuna mnyororo inabidi kila MTU ale kabla ya final consumer ikumbukwe ukitaka kula inabidi uliwe pia ukitaka soko zuri ni gharama ya pesa na mda ukubali kula deal na watu wa faida as long as kuna maslahi
Na huko shambani hao hao mnaowakataa madalali watakuja kwa kutaka mzigo kwa bei "ndogooo" kama kuagonjwa ka corona!sijui watu wakimbilie wap
 
Back
Top Bottom