Nataka 50,000,000 ya pamoja, nilime heka ngapi za nyanya/viazi mviringo?

Mkuu chonde chonde kilimo kinachangamoto nyingi mno hasa kwa beginner utapunwa hiyo 10M yoteee uchizike niliwahi kulima nikiwa mgeni shamba LA 1.5M per acre nilitoa 3M gharama tena mazao perishable ni hatari zaidi hivyo bora ununue mazao ukae kidogo uuze japo faida kiduchu ila afadhali Ila kama mbishi Lima acre 1 upate uzoefu ulime kwa ukaribu na wazoefu.Lima mahindi na maharagwe japo umechelewa labda next season unaweza mahindi kwa kumwagilia Ila maharage yakumwagilia sio mazur Mimi zao ambalo naona haliumizi kichwa ni mahindi na maharagwe yaani simple palilizi moja Kwisha japo mahindi siku hizi tunapiga dawa ni changamoto kwa shamba kubwa maana kila mmea inabidi ipate dawa vibarua wanaripua.
 
Na huko shambani hao hao mnaowakataa madalali watakuja kwa kutaka mzigo kwa bei "ndogooo" kama kuagonjwa ka corona!sijui watu wakimbilie wap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…