Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 87
bwana burn ni wewe ndo mheshimiwa Lwakatare au? maana tuliambiwa ataingi ukumbini.. karibu.. lkn la kushangaza nahisi tayari jamaa washakubadilisha kabla ya wewe kuwabadilisha maana tumezowea kuona kina Tambwe,Salum msabah,Kabouru,Lamwai wakibadilishwa halafu ndo wanajiunga na CCM RASMI.. wakowapi? hongera Kwa mafisadi kukunua..
Burn at least wewe unaelekea maan wengi wetu tumebaki kukinyooshea kidole khuku tumesimama mbali CCM wako hivh CCM iko vile but no one dares to do anything.
Wengi wetu pamoja na kuyaanika makosa, maovu na uozo wa CCM bado tumekiri kuwa hatuna Chama pinzani chenye uwezo wa kupambana na Chama hiki cha mafisadi. Matokeo yake tunaishia tu kulalamikia wananchi na upofu wao katika kukichagua chama CCM.
Bora yako ambaye umeamua kuitumia haki yako ya msingi ipasavyo. Ni matumaini yangu kuwa ukishajiunga na CCM hutaungana nao katika UFISADI na uozo wote unaotajwa bali utasaidia, utapigana katika kukibadilisha kwani umeshajua ugonjwa wake.
wewe ni shujaa miongoni mwa mashujaa wapigao kelele bila vitendo.
Kila la heri, ukihitaji msaada usisite kluwa wazi.
Mpeni chama mbadala basi kama hamtaki ajiunge na CCM. Kwa ambao hawataki ajiunge na CCM mnamshauri ajiunge na chama gani? Mimi binafsi so far sijaona chama chochote ambacho I'm willing to commit to. Labda watu mnaweza kutusaidia hata na sisi wengine kujua wapi pa kwenda.
(Samahani kama kuna tusi au lugha inayoweza mkwaza mtuhapo juu) " We dare to talk openly"
Mkuu nimeona mantiki yako. nadhani ni rahisi kuwadhoofisha hawa kutokea ndani, nakuunga mkonoNajua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM(sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka). Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi. Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
Umejidhatiti vipi kuyakabili mapapa ya CCM?
Umejidhatiti vipi kuyashinda waliyoshindwa waasisi wa CCM?
Umejidhatiti vipi kuhakikisha hulali kama wanasiasa machachari wa CCM (waliojitokeza/ wanaojitokeza/wakafanya waliyofanya, watajitokeza baadae kama ulivyojitokeza wewe) na bado wakaanguka chali aidha kwa tamaa mbali mbali au mfumo wa CCM?
Umejidhatiti vipi kuhakikisha hutatuchosha kwa kuwafadhili wapinzani kama ulivyodai hapo juu ukiwa ndani ya CCM?
Umejidhatiti vipi hurudi (ukinyonga) huku utokako kisa uendako ukakukuta ni kubaya au kuzuri zaidi? (Tutakupokeaje? Kwa makofi au kutuandikia humu mkekani kwamba unatafuta pa kuingia tena?)
All in all umejidhatiti vipi kuhakikisha mizani ya UWILI wako na CCM hautalilia kwako?
Nani kakudanganya kiumbe wewe mabadiliko na maendeleo huletwa ukiwa TU ndani ya chombo cha kilicho madarakani? (Mbona kwa miaka zaidi ya 40 ya uhuru hatujayaona?
Nani kakudanganya kiumbe wewe ukiwa kigeu geu/ kutokua na msimamo na kutojua ufanyalo ndio njia ya mabadiliko?
Nani kakudanganya kiumbe wewe CCM atatawala milele Tanzania hii?
Nani kakudanganya kiumbe wewe CCM itang'olewa na mtu kama wewe usie na msimamo?
(Samahani kama kuna tusi au lugha inayoweza mkwaza mtuhapo juu) " We dare to talk openly"
Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo
kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM (sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka).
Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi.
Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo,
siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM(sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka). Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi. Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
Wewe na yeyote aliye pamoja nawe ni watu wa kuogopwa kama ukoma. Kinachowavutia huko ndicho wengi tunachokipigia kelele - uozo ndani ya CCM.
Manyang'au hujikusanya kwenye mzoga, ole wao mzoga ukiisha.