Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo
Unajuaje tutashangaa ? Kwanza, CCM ndio kimbilio la wanafiki na mafisadi na huko ndiko wanakopata hifadhi. Pili, maadamu umepata ufunuo wahi ukate hiyo kadi maanake huku nje muda si mrefu hutabaki salama.
kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM (sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka).
Kama hayo mabadiliko hayakuweza kupatikana katika kipindi cha miaka karibia hamsini, kwa nini Burn leo hii aweze lililoshindikana - una nguvu gani ? Hivi sasa ni miaka miwili toka orodha ya mafisadi imetajwa na wote bado wamejaa tele kwenye uongozi ndani ya CCM na wewe uko nje - hicho hicho unachokikimbilia huko ndicho kinachowafanya wazidi kukumbatiwa huko.
Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi.
Kwetu wengine tunaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii hayo unayoita nguvu ya mabadiliko ya kuridhisha hatuyaoni zaidi ya usanii. Hebu tueleze hayo matukio ndani ya chama na serikali yanayotoa taswira ya mafanikio. Serikali iliwekwa madarakani na asilimia 80% ya wapiga kura, ni nguvu gani zaidi yahitajika kuongezwa - ya Burn kwa kutaka kadi ya CCM rasmi ?
Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo,
Je, vyama vya sasa kufadhiliwa na CCM, huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa njaa, umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na
CCM hovyo, ni sababu tosha ya kutufanya kujiunga na CCM ? Kama CCM inaweza kubaki ovyo pamoja na kelele za wachache upinzani, itakuwaje wote tukijiunga CCM ?
siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Kwa nini usubiri vibadilike na usiungane nao kuwabadilisha na badala yake unajiunga na CCM unayoita ovyo kuibadilisha. Unasema unawafuata NAPE, JERRY na vijana wengine machachari - hawa wamefanikiwa nini cha kujivunia ndani ya CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
Wewe na yeyote aliye pamoja nawe ni watu wa kuogopwa kama ukoma. Kinachowavutia huko ndicho wengi tunachokipigia kelele - uozo ndani ya CCM.
Manyang'au hujikusanya kwenye mzoga, ole wao mzoga ukiisha.