Habari ndugu wana JF
Mimi kutokana na maisha kuwa magumu nafikiria kuacha chuo ili nijihusishe na uzalishaji Mali.
Nazungumza haya kutokana na kauli ama ushauri wa POLEPOLE kwa wanachuo waliokosa mkopo.
Nimefikia uamuzi huu ila sijajua nianze kufanya shughuli gani.
Duh! Itanibidi niitekeleze kauli mbiu ya mheshimiwa sana.
[emoji86] [emoji86] [emoji86] [emoji86] [emoji86] [emoji86] [emoji86]
Haina haja kuacha chuo jamaa yangu.sema naye mheshimiwa sijui kauli yake kaitoaje.cha kufanya kukuruka na vishughuli/vijibiashara hata kama ni vidogovidogo ukiwa hapo hapo chuoni.tumia mkusanyiko wa jumuiya ya hao wanachuo wenzako kama soko lako na fursa kwako.
Mm sijui upo chuo gani na mazingira yako yakoje.lakini ninachofahamu ni kwamba mahali popote penye mkusanyiko wa watu kwa mjasiliamali tayari hiyo ni fursa kwako.cha msingi ni kusoma mazingira na kuona nini kifanyike.
Swala la mtaji lisikutishe,mtaji ni kiasi chochote,kikubwa ni commitment kwa hicho kiasi kidogo utakachoanza nacho na kuweka strategies muafaka.Binafsi nakumbuka nilikua nashindwa kuanza ujasiliamali kwa kusingizia sina mtaji kwakuwa pesa kidogo niliyokuwa napata niliibatiza jina la ''hii ni pesa ya kula tuu''. Amini usiamini siku moja sijui ni nini kilinifungua akili siku hiyo nilipata kama laki moja (100,000/=) nikasema kuanza leo nakuwa mfanyabiashara nitahakikisha hii pesa naiweka chini ya uangalizi maalumu wa kuizungusha bila kuila.wakati huo ilikuwa 2011 nilikuwa SUA kama mwanafunzi.nilianza kununua flash na kuziuza kwa wanafunzi wenzangu.baada ya muda kidogo nikawa naweza kununua computer 1 used na flash kidogo na kuviuza.baada ya mwaka hivi nikawa na zaidi ya 2m. Mda huo kwakuwa wadau wakawa wananijua na kuniamini ikawa napata order na baadhi wakawa wanatoa advance nikichanganya na mtaji wangu naleta mzigo wa maana.
Huwezi amini sikuwa na mkopo lkn nilipata unafuu mkubwa sana wa maisha pale chuoni.leo hii ninavyoongea namshukuru sana mungu kwakuwa misingi ile ile niliyotoka nayo chuoni niliingia nayo mitaani nimekuwa nikifanya biashara tofauti tofauti kulingana na mazingira ya wakati huo.
Baada ya chuo nilifanikiwa kupata kazi mahala fulani sitapenda kupataja hapa jamnvini.ila ukija inbox nitakwambia bila shida yoyote. Hapa napo nilijifunza kitu kipya wakati wengi wanafikiria mtu ukipata kazi ni suluhisho na kuanza kuutegemea wenyewe kujikimu kimaisha. mm nikajiongeza kwa kutumia mshara wangu kutunisha biashara yangu.any way story ni ndefu lkn mpaka sasa biasha zangu ni za milioni nyingi kiasi na kiasi nimetoa ajira kwa watanzania wenzangu wachache.mungu akipenda nategemea kuachana na kibarua nilichonacho nisimamie miradi yangu.
Kitu ambacho nataka ukiona inafaa ujifunze hapa ni kwamba mtu anayeweza kutatua magumu uliyonayo ni wewe mwenyewe kwa kutumia mtaji mkubwa uliopewa bure na Mungu ambao ni "akili" yako mwenyewe.mtaji wa pesa huongozwa na mtaji mama ambao ni akili.hivyo pesa kidogo zikiongozwa vizuri zitakuwa nyingi tuu.
Nawasilisha.