Nataka kuacha Chuo nijiingize katika ujasiriamali kwa mtaji huu

Nataka kuacha Chuo nijiingize katika ujasiriamali kwa mtaji huu

Kigorohe

Senior Member
Joined
May 21, 2019
Posts
160
Reaction score
255
Habari wana JF!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24, nipo mwaka 3 moja kati ya vyuo hapa nchini. Lakini moja kati ya vitu vinavyoniumiza hapa duniani ni pale ninapoishiwa hela ya matumizi na kunilazimu niombe nyumbani ili niendelee na maisha ya chuo japokuwa umri wangu unatosho kutafuta mwenyewe.

Kwa sasa nimejichanga mpaka nimefikisha 600k. Nikiangalia ugumu wa maisha baada ya kumaliza chuo nataman niache tu au nipospond mwaka ili nijaribu bahati katika ujasiria mali. Nipeni ushari wenu
 
With no matter how, usiache chuo mwaka wa tatu...malizia kipande kilichobaki, ungekuwa first year labda, wakati unamaliza masomo uwaze namna gani unaweza anza ujasiriamali huku unafanya utafiti wa kutosha juu ya hicho unachoenda kufanya, usiingie kichwa kichwa, utakuwa na possibility kubwa ya kufeli.
Mtazamo tu.
 
Mzee komaa umalize game la chuo...

Sometimes kweli, ukiwa chuo unaona kama unapoteza time tu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Umepiga semisters 4 unashindwa kumalizia kipande kidogo hicho!!!! Komaa dogo hiyo laki 6 itumie kumalizia safari yako uliyoianza.

Ukishaikamilisha ndo uanze kuifungua akili yako jinsi ya kupata mtaji kwaajili ya ujasiriamali. Hata kama GPA uliyonayo yatishia Amani wewe malizia tu hicho kipande.
 
Anza Biashara ukiwa bado unasoma chuo usiache chuo hakuna sababu yoyote ya msingi ukaamua kuacha chuo piga biashara ukiwa chuo huu ndio mda sahihi wa ww kufanya biashara anza ukiwa unasoma chuo wateja wako wakuu wawe wanafunzi wenzako ukimaluza chuo unalisongesha tu wakati wenzako wanalalamika hawana ajira wewe utakuta biashara yako imeshaanza kusimama unateleza tu wakati huo gamba tayari unalo. Biashara ikiwa ngumu na kazi zikiwepo una switch tu dogo maisha ni kuwa mjanja kama sungura kuwa na option mbili biashara na cheti apo lazima utusue.
 
Mimo nilipostpon chuo lkn sio kwa kuwah ujasiriamal...!!niliona maisha yatakuwa magum chuon baada ya kumkazia lecturer aliyechana paper langu ndan ya chumba cha test

Nilikonda ndan ya cku 2....ila baada ya hapo ndo nkaamua kutafta pesa...!!kwa hasira maana hata dem aliniacha kisa cna pesa

Mpaka sasa life linaenda...biashara imecmama.....sijutii kuacha chuo

Sema pia elim ya sasa inasumbua...unapigika chuo...unakuja kupigika mara mbili mtaan...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kujua bahati yako mkuu chukua hilo ganda then ingia mtaani, maana kazi zipo ila wenye kuhitaji ni wengi so lazima kuna watakao pata na kuna watakao kosa sasa utajuaje kama ww ni kati ya watakao pata?

Chukua ganda ili angalau uwe na option zaidi since ushapoteza muda wako labda ungelikimbia mapema ulipomaliza tu kidato cha nne, kwa sasa kwako mbele ni karibu sana kuliko nyuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom