Nataka kuacha kazi niingie kwenye kilimo nishaurini

Nataka kuacha kazi niingie kwenye kilimo nishaurini

Kilimo siyo kitonga kama unavyohadithiwa kaka. Fikiria mara mbilimbili kabla ya kuchukua hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
teh..teh..teh... acheni kumtisha yeye kesha piga hesabu kwenye laptop halafu mnamwambia nini? eti hakilipi? awapi huo utakuwa wivu wa kike! mwache aingie atajua hukohuko kuwa uwaziri hausomewi!
hebu fikiria unaenda shamba unauanalia mpunga unasema hapa siwezi kosa ngunia kumi wakipiga zinatoka mbili na debe 3 imekaaje hii! sasa hivi vitu hawezi kukuelewa mpaka aingie shambani.
au kuna jamaa alilima kwa simu alidaiwa fedha zote na picha anarushiwa siku ya kwenda shamba hakulikuta msimamizi kampiga mwanzo mwisho na cha kumfanya hana.
ziko story nyingi hivyo ukiingia ukileta zako tutajifunza jinsi ya kupata mafanikio zaidi.
 
Kwa hiyo faida yake ni kitoweo kwa familia?
hata hiyo inaweza kuwa faida pia fikiria ukienda wanakamata njiwa kama watano wanawachomea na ugali hivi unaweza kuona wameokoa kiasi gani kwa mboga? lakini wapo watu walikuwa wanaenda kununua ila kwa wakati ule walikuwepo kwa kuliwa sasa inaposemekana kwa biashara nakubali kabisa inaweza lipa sana tu kwa kuwa mfugaji atamaanisha anachofanya.
 
Usisubutu hata kidogo kuacha kazi kwa hela za kilimo cha msimu mmoja utakuja jutia kamwe jipange kwanza kilmo kichanganye ndo uache kazi ujue kila pembe ya kilimo au kama ni kilimo cha bangi sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku umeacha kazi umelima matikiti yako umeyapakiza kwenye fuso unayo kama 9,000 hivi kwa matarajio ya kuuza 2000 kwa piece unafika sokoni fuso kama 50 hivi hivyo inabidi uuze 500 hapo ndo utaelewa nini maana ya kuacha kazi
 
ngoja tutumie nguvu kidogo kukushauri ili tujaribu kuupa ubongo wetu starehe kwa kilimo unachotaka kufanya.
  1. kwanza nategemea ya kuwa wewe utakuwa ni mtoto wa mjini hata kama maisha yenu ya asili ni kijijini lakini kuna uwezekano kabisa kwa zaidi ya miaka 15 haujui vizuri shughuli za shamba zinafanyikaje?
  2. swala la umri ni la msingi kwako kwa kuwa kuna umri ambao unaweza kushindwa kuingia na kufanya hata kwa asilimia 30 shughuli ya mojakwa moja shamba.
  3. ujuzi na uzoefu wako kuhusu kilimo unachotegemea kufanya ukoje sio swala fulani alilima matikiti yakamtoa hivyo na wewe unaona ni vyema ukalima matikiti je unajua misimu ya zao unalotaka kulima na je umefanya utafiti wa kutosha
  4. maeneo gani unataka kufanya kilimo na kuna faida gani ukilinganisha na maeneo mengine na hapa ni pamoja na miundo mbinu na fursa nyingine zinazoweza kuwezesha kufanya vizuri katika kilimo unachotarajia.
  5. kuna changamoto gani katika kilimo tarajiwa na umejipanga vipi kuzikabiri hapa zipo za ndani na nje lipo swala la mbegu feki pia magonjwa.
  6. kilimo aina gani unategemea kufanya cha kutegemea hali ya hewa (kilimo asili) au kilimo cha kisasa.
  7. umetenga mtaji kiasi gani na kwa kuanzia unafikiri ni fedha kiasi gani kinahitajika katika kuanzisha kilimo
  8. je wajua jumla ya shughuli zinazotegemewa kufanyika kuanzia kutayarisha shamba mpaka kuuza mazao je zinahitaji vifaa gani na bajeti yake ya kununua ikoje.
  9. walaji wako wakoje na unafikiri ni soko kiasi gani bidhaa yako inaweza kuchukua. je mazao unayotegemea kuzalisha wewe mwenyewe ni sehemu ya soko je matumizi yako yakoje
  10. je ipo faida itakayokuwezesha kuendelea na maisha yako ya kawaida au faida itakayopatikana itatumika kuendesha mradi
  11. umejipanaje kaika kusimamia
  12. unawashirikishaje wenyeji katika kuzalisha na mavuno na je unategemea kuwa na wafanyakazi wangapi na utawalipaje
yapo mengi mno kwa jioni hii yakutoshe pamoja na michango ya wadau mbalimbali iliyotolewa ila bado ushauri wangu kutoka moyoni kabisa karibu ufanye kilimo lakini kwa miaka ya kwanza sikushauri uache kazi vinginevyo unatoka katika familia bora wanaweza kukuwezesha ukianguka lakini kama ni zetu hizi mdogo wako hana ada sikushauri uache kwanza.
hata hivyo usiogope nia yako ya ndani ikufanikishe kwa kuwa hata aliyewezesha taa kuwaka alifanya majaribio 1000 sasa asingefanye mengine leo tungekuwa giza.
 
pia naweza kukusahuri kama unaingia kwenye kilimo uchanganye na mifuko kuna kazi naendelea kuifanya ikikamilika nitaiweka hapa ili kwa michango yenu niweze kuiboresha ambayo nitaonyesha kwa kiasi gani unaweza kufanikiwa ukitumia kilimo na mifugo katika kukuza kipato.
 
Kama kichwa kinavyojieleza, nimekuwa kwenye ajira mwaka wa pili, nimeona biashara zinalipa, haswa kilimo biashara, nahitaji ushauri na jinsi ya kupata masoko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kinalipa lakini kila kinacholipa hupatikana kwa jasho sana. it is not that easy. ukitaka kuingia katika kilimo kwanza kusanya taarifa nyingi kuhusu kilimo. kusanya mtaji wa kutosha na kubali kuanzia kwenye zero point. na ukishaingia ni kama mtu akaingia kwenye maji kwa nia ya kujua kuogelea.usidhani utapata mafanikio kwa muda mfupi.
achana kabisa na stori za mitandaoni kuhusu mamilioni ya kufikirika kutoka kilimo. hayo utayaona kadiri unavoendelea na si kwa muda mfupi bali utachukua muda. katika kilimo unavoanza sivo unavomalizia kwa sababu kila mara unajifunza na kubadilika
kinachohitajika ni uvumilivu na juhudi.
kama upo karibu na sehemu ya kuanzisha kilimo hebu anza kwanza ungali kazini but Usikate tamaa ukikwama mahali bali songa mbele.
NI KWELI KILIMO KINALIPA
 
duh,naona wakuu kwa % kubwa wanakutisha kabla hata hajatueleza kiundani kuhusu mpango wa kilimo mkuu mtoa mada. lete maelezo ya kutosha keanza
 
Anza kufanya hiyo biashara kabla hujaacha kazi, biashara zina changamoto sana hasa ndio ukiwa unaanza. Ukiona umekua mzoefu na umekwishaijua biashara yako vizuri hapo ndio unaweza ukaacha kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Dibaji,
I salute you.
Unastahili kuwa katika Jamvi hili, unajua maana ya kuwa humu na unajua kujumuika na wana jamvi ukiwa umetuliza akili zako.
Ulivyomshauri mjenga hoja ni sasa kabisa. Ajiingize kwanza kwenye kilimo atakapoona amejisimika ya kutosha, Aache kazi.
Lakini! Kilimo kinalipa kuliko biashara zote tatizo tu ni ugumu wa shughuli yenyewe ila ukizoea unakuwa vizuri.
Kikubwa katika kilimo ni kujituma na kuwa self discipline kama biashara zingine zinazoendeshwa kibinafsi sababu hazina security kama kuajiriwa. ukitumia vibaya vyanzo vya kazi mwisho ni kufilisika.
Ajira haifilisiki unless otherwise.
Aachane na watu wapuuzi wasio na shughuli ya kufanya wanakuja kuropoka mambo ya kipuuzi na kurukia mambo yasio wahusu.
Mtu hajauliza swali kuhusu mkewe, wewe unaenda huko kutafuta nini?
 
Back
Top Bottom