Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

Hizi ndio mentality za Watanzania wengi. Yuko radhi kung'ang'ania ajira ya laki 7 ila anaogopa kuchukua risk ya biashara inayoweza kumuingizia 3m

Point ya watu wengi na yangu ni hii; Noah kazinunua kwa mkopo unaotokana na mshahara. Now najua utasema kuwa watu wengi wanafanya biashara wakiwa na mikopo kwa nini yeye ashindwe?

The answer is, siongelei kushindwa, naongelea maximizing profit. Akibaki kwenye hiyo ajira yake mpaka mkopo wake ukaisha kisha akaendelea kusimamia mradi wake atakuwa huru na mbali zaidi kiuchumi kuliko kuacha sasa na kulipa madeni kwa pesa ya magari.

Again wengi wamemshauri vyema, kuwa na source nyingine ya income zaidi ya hizo Noah. Tulienda shule si ili tuwe waoga wa ku-dare lakini ili tuwe smarter ones. Ni vyema wakati anamalizia mkopo atafute another source of income. Hata kama sio mkubwa sana - kwa mfano nyumba ya kupanga (but pliz mkuu usijenge viboksi useme nyumba ya kupanga) - lakini diversify your income.

Mwisho, kazi unayofanya! Mfano, mimi ninaipenda kazi ninayoifanya kwa kuwa niliitaka muda mrefu. I enjoy doing it. Na bonus ni kuwa haininyimi uhuru wa muda wangu. Ninaweza kufanya mambo mengine kadri nitakavyo bila kuathiri utendaji wangu. Sometimes, kuajiriwa ni kutimiza ndoto yako kwa njia ambayo usingekuwa huko usingeweza kuitimiza lakini haimaanishi unakuwa mtumwa wa kazi na haimaanishi uridhike na mshahara wako..always seek to invest your money. Kama unaogopa kabisa biashara be a disciplined saver...savings account and save diligently, buy shares or government bonds if your finances allow. Point is, never put all your eggs in one basket.
 
Dizaini kama unapima upepo hivi.. aliyetayari kufanya maamuzi yake hawezi hawezi kuomba ushauri humu akijua fika atakatishwa tamaa.
 
Reactions: y-n
Mimi nadhani ni vizuri kujiajiri ila usiache kazi kwanza.
Wekeza katika biashara nyingine zikishaanza kutengamaa na kuingiza faida acha ili uziendeshe vizuri.
Ila kama ni risk taker acha
 
RRONDO Umeongea jambo la msingi sana, biashara isiyokuwa na usimamizi haiwezi kutoa faida nzuri.
Kinacho waangusha wafanyakazi wengi ni kuanzisha biashara na kuwapa watu wengine wazisimamie, hapo wanapigwa mikwaju ya kutosha.Kama bishara yako inakupatia 40 kwa siku, ukiisimamia mwenyewe lazima ikupatie 50-80, hakuna mtu mwaminifu walau80% linapokuja swala la pesa.

Kitu kingine ambacho mtoa mada anatakiwa kukijua ni kwamba mbinja nyingi humchanganya mbwa.Nguvu kubwa ya kufanya maamuzi ya kimabadiliko inatakiwa itoke ndani mwako.Sasa hivi anachotakiwa kukifanya ni kuomba ushauri kwa waliowahi kuacha kazi na kujiajiri ili ajue njia atakayopita ipo je na sii kuomba ushauri wa kuacha kazi au la!
 
Kwanza nikupongeze kwa wazo zuri. Lkn mkuu kumbuka magari ni ya muda tu japo hata kazi unaweza kuachishwa wakatu wwte.
Ww endelea na kazi mkuu, hata miaka 5 uhakikishe umefikisha noah 4, umejenga nyumba yako nzuri, na nyingine km 2 umepangisha una maduka km 3 hiv na vitega uchumi vingine halafu uache kazi sasa hapo itakuwa safi.
Mfano. Noah zote mbili zinapata ajari, siyo km naombea hivyo inaweza tokea. Je, utahimili kuishi?
Mkuu hizi gari ni za kupita tu na usizitegemee sana.
Jenga nyumba angalau 3 uzipangishe. Sbb nyumba inaweza kudumu miaka 100 je, gari linaweza?
 
Acha tu kazi mbona mwenyewe niliacha na maisha yanaendelea tu watanzania tupende kujiajir jamani
Wazo zuri kumbuka ww uliingia kwanza kazini halafu ukatoka.
Tayari hapo ww una mtaji wa kutosha.
Kila mtu anapenda kujiajiri lkn mtaji ndiyo unasumbua.
Ukienda kukopa unaambiwa uwe na kiwanja sijui nyumba yaan masharti mengiiii
Km hauna vyote hivyo unafanyaje?
 
Wabongo bhana kuwa na Noah mbili anaona kazi sio issue! Hzo noah zinapiga mzinga mda wowote kijana kazi ni dhamana kopa zaidi benki uwekeze kwenye ardhi
 
Wengine wanalilia kazi ww wataka kuacha,acha uone
 
Pole yenu mnaong'ang'ana na ajira kisa mnaogopa. Subirini kushika pesa mkiwa na miaka 40-50
Mkuu utambue hapa duniani kila mtu anambinu zake za kutokea .
Maarifa yako sio yake wala sio yangu kwahyo tuyaache kama yalivyo ...
Kuna wenye majumba ya kifahari lakn hawalali kwenye hzo nyumba, kuna wenye kila utajiri lakn wanalala chini..
 
Hakuna hasara kubwa kama kuwekeza kwenye resources ambayo ina hamishika na kutembea ,wapi kiswele,tawaqal,safina ,nk? Na ni vipi iama hayo mdio yangekuwa masha ya kudumu na tegemeo lao? Usimshauri kuacha kazi bali mshauri kuboresha vyanzo vingine vya mapato vya vya kudumu.
 
Mimi naona uache kazi. Hizo gari unazikatia comprehensive insurance, unapga kaz na noah 1.
Kama wanakupa 40000 inamaana madereva wako wanapata zaid ya 80,000, so mnagawana faida. Sasa ukiendesha wewe ni faida mara 2. Pesa utazopata unainvest kwenye vtu vingne. All the best.
 
Ukiomba ushauri wa kuacha kazi kwa watu walioajiliwa au wapo wanatafuta ajira, watakushauri usiache kazi. Kwa kundi ambalo wameacha kazi au hawakuwahi kuajiliwa na wanamafanikio watakushauri ukomae na biashara zako. Lakini nikwambie ndugu, lisimamie kwa vitendo hilo suala lako, weka mazingira ya vitega uchumi vingine kama ulivyoshauriwa na wadau hapo juu na pia aindae akili yako kwa kuacha kazi. Fuata ushauri kwa watu waliofanikiwa kwenye hiyo biashara, watu walioshindwa wanamaneno mengi sana.
 
Usiache kazi kwa assets hizo, Acha kazi ukishapata assets zinazopanda thamani..
Au fanya kuchukua hizo gari piga biashara baada ya muda uza nunua tena, ufanye biashara mbili kwa wakati mmoja.
 
Hii nidham ya uoga sijui watanzania tunapoitoa jaman!! Why tunapenda kufanya kaz za watu? Mbona mimi niliacha kaz na kuanza kama machinga na sasa nina kipato mara 20 zaid ya nilivyokuwa kazin
biashara bhana ktu knachotufanya tuiogope,mfano unaweza kupata duka kubwa au gari kubwa la mizigo lakin hiv vyote vnaweza kupotea vyote ndan ya sku moja na ukarudi kuwa masikin,
 
Unaweza kuacha kazi.. Lakini wekeza zaidi.. Usiingie woga ndugu kuna watu kibao hawana kazi hata hiyo elimu hawana na ni wafanya biashara na wanatoka
Cha msingi buni miradi zaidi.. Halafu ndio uache.
I like the boss spirit of yours utafika mbali wala usitishwe. Omba Mungu akusimamie
 


Mbona profile icon yako haifanani na unachoandika hapa
 
Ni wazo zuri sana,achana na kitanzi kinachoitwa KUAJIRIWA, Hapo utaendelea. Acha pia kufikirikia MAWAZO mgando ya watu wengi kuwa bila ajira,maisha yatakuwa magumu au utateseka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…