Mentor
JF-Expert Member
- Oct 14, 2008
- 20,328
- 23,909
Hizi ndio mentality za Watanzania wengi. Yuko radhi kung'ang'ania ajira ya laki 7 ila anaogopa kuchukua risk ya biashara inayoweza kumuingizia 3m
Point ya watu wengi na yangu ni hii; Noah kazinunua kwa mkopo unaotokana na mshahara. Now najua utasema kuwa watu wengi wanafanya biashara wakiwa na mikopo kwa nini yeye ashindwe?
The answer is, siongelei kushindwa, naongelea maximizing profit. Akibaki kwenye hiyo ajira yake mpaka mkopo wake ukaisha kisha akaendelea kusimamia mradi wake atakuwa huru na mbali zaidi kiuchumi kuliko kuacha sasa na kulipa madeni kwa pesa ya magari.
Again wengi wamemshauri vyema, kuwa na source nyingine ya income zaidi ya hizo Noah. Tulienda shule si ili tuwe waoga wa ku-dare lakini ili tuwe smarter ones. Ni vyema wakati anamalizia mkopo atafute another source of income. Hata kama sio mkubwa sana - kwa mfano nyumba ya kupanga (but pliz mkuu usijenge viboksi useme nyumba ya kupanga) - lakini diversify your income.
Mwisho, kazi unayofanya! Mfano, mimi ninaipenda kazi ninayoifanya kwa kuwa niliitaka muda mrefu. I enjoy doing it. Na bonus ni kuwa haininyimi uhuru wa muda wangu. Ninaweza kufanya mambo mengine kadri nitakavyo bila kuathiri utendaji wangu. Sometimes, kuajiriwa ni kutimiza ndoto yako kwa njia ambayo usingekuwa huko usingeweza kuitimiza lakini haimaanishi unakuwa mtumwa wa kazi na haimaanishi uridhike na mshahara wako..always seek to invest your money. Kama unaogopa kabisa biashara be a disciplined saver...savings account and save diligently, buy shares or government bonds if your finances allow. Point is, never put all your eggs in one basket.