Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

Mimi pia ushauri wangu ni kuwa acha kazi baada ya miaka mitano kutoka sasa. Katika kipindi hiki weka malengo ya muda mfupi sana kama miaka mitatu hivi ya kutanua biashara yako hiyo; lets say in three years uwe na haisi au noah tano, sita etc. Halafu miaka miwili inayofuata iwe ni kuwekeza katika biashara tofauti na hiyo ya usafirishaji. After five years, fanya tathmini kisha amua. Nimetoa ushauri huu kwakuwa nikijenga assumption ya profit of 35% of your sales inakuwa kama laki nane hivi. Matumizi yako ya familia itabidi yasizidi laki nane kamili ili biadhara isianguke. Na ili biashara yako ikue inabidi some of your profit have to be re invested. Kwa maana hiyo tokadirie utawekeza nusu ya faida; that means utabakiwa na laki nne kamili kila mwezi ya kula na familia.

Kwa ujumla maamuzi ni yako; ila kwasasa nakushauri uvute subira kidogo kwa miaka mitano ambayo iwe ni ya uwekezaji kwelikweli; ujinyime na ufunge mkanda kwaajili ya uwekezaji hususani kwenye kutanua biashara yako ya sasa na kufungua biashara mpya.

Kimsingi unaweza kuamua kuacha kazi hata sasa hivi na biashara yako ikashamiri vyema zaidi kuliko sasa. Lakin kiukweli ni kuwa risk level bado ipo juu sana kwakuwa noah mbili bado hazikupi fursa ya kutegemea zenyewe kwa zenyewe at the time of crisis. Binafsi ni muumini wa kujiajiri na ninapenda kujiajiri; nakushauri kama roho yako ikikupa wasaa wa kufanya kazi basi endelea lkn weka kikomo cha muda na goals. Ushauri wangu ni miaka mitano inatosha kabisa kwako kufanya maamuzi magumu; changamoto za biashara utakuwa umeziona kiasi cha kutosha na biashara utakuwa umeizoea.
 
Biashara ya nyumba hailipi ila inapaswa kuwa retirement plan yako ambayo hutegemei irejeshe faida katika uhai wako bali ije ikulee ukiwa mzee ktk wakati ambao huwezi mikiki mikiki ya kutafuta rizki. Just like ppf, pspf etc
 

Woga wako ndio umasikini wako. Fanya mchanganuo wa kipato pande zote mbili, ukishaona upande upi unalipa fanya maamuzi. Watanzania wengi ni waoga sana kufanya maamuzi, usichoke kujaribu, kwani utafia hapo kazini? Vunja mifupa ingali meno bado ipo!
 

Word! Thank you!
 
Unaweza acha ukawin. Mara nyingi biashara za kuanzia chini huwa tunazidharau haaa die wasomi. Ningekuwa Mimi ningeuza Noah moja nikafungua duka LA chakula tRNA mawili. Mfano ukiuza Noah 9mil. Hapa napata maduka ya uswahilin kama mawili ila sehemu nzuri ni kama ukipata tegeta au kijichi stend. Mzigo Wa million NNE ni mkubwa sana. Ukipata location nzuri mauzo ya laki NNE per day ni kawaida sana. Faida kwa hayo mauzo Inaweza fika mpaka 70000. Hapo ukizoeleka mikopo kwa makampuni ya vyakula ni normal sana hapa unaweza jikuta mtaji wako ukawa unafanyia mambo mengine. Na baadae ukiwa concord unaweza kuwa unafata vyakula mikoan kama mchele mahindi maharage na kuna kuyauza kwa being rahisi. Tatizo letu wasomi tunaogopa macho ya watu. Na Mara nyingi tunafikiria biashara za mabilion
 
Ushauri mzur sana ila kwangu Mimi miaka mitano ni mingi sana. Kwa kukadilia sasa hivi atakuwa above 30 letsay 38. Akija komaa baada ya hapo atakuja jikuta hata thinking capacity inakuwa sio kama sasa pia majukumu yatakuwa mengi. Kiukweli kuacha kazi sasa hivi ukaendeshe Noah simshaur
 
Binafsi, kiwango cha chini kabisa ajipe muda wa miaka mitatu ya kuendelea na kazi. Ndani ya muda huu awe na focus ya kutanua biashara ambayo amekwishaianza, asianzishe biashara mpya. Ndani ya kipindi hiki cha miaka 3 atajifunza mengi kuhusu biashara hiyo na atakuwa kwenye nafasi ya kushughulikia vzuri changamoto alizoziona baada tu ya kuacha kazi.
 
Wasomi wanashida saaana. Wametawaliwa na woga wa kushindwa na ndio chanzo cha umaskini, uliona wapi mwajiriwa katajirika jamani?. Ndugu yangu duniani waliofanikiwa ni wale waliothubutu. Achana na kazi za kuwatajirisha watu na wakati wewe unazeeka na nenda kajitajirishe mwenyewe. Uzoefu wa kazi tayari unao na utaalam hauzeeki, ukifanya biashara zako zikagoma si unaweza kuanza upya ajira, tatizo wengi wetu tina mawazo mgando ya imani ya kuwa watumwa wa watu. Kwani huyo tunayemfanyia kazi kafanyaje bana. Jiajiri bana halafu miaka mitano au kumi ijayo utakuja kuwa ajiri hao hao walosema usiache kazi na uwatume kweli kweli ili waendelee kukutajirisha zaidi
 
Amebakiza mwaka mmoja tu sasa.
 
Haya mawazo yako bado yanaishi na yataendelea kuishi...bigUp
 
Ajira huwa ni sehemu ya kutafutia mtaji, ukishapata mtaji na unaona mambo yanakwenda sawa, unatakiwa kuacha kazi na kwenda kusimamia kitu chako.

Mfanyakazi hashauriwi kuacha kazi kabla ajira aliyonayo haijamuingizia kipato. Ieleweke kuwa hata kuacha kazi unatakiwa ujiulize, umeandaa kitu gani cha kukuingizia kipato? Kama ni magari ndugu yangu eti yanakuingizia hicho kiasi ulichokitaja hapo ni sawa na kucheza bila mziki. Nakushauri usiache kazi kwa sababu magari siyo asset ya maana yanaweza kukuacha katika wakati mgumu ambao hukutarajia.

Hakikisha unaanza kuwa na kitu durable cha kuingiza kipato, na siyo magari. Jenga Nyumba hata ya milioni 50 pangisha kwa mwaka. Nyumba ina uhakika zaidi kuliko hayo magari. Lakini pia vipo Vinci vya kuanzisha kuliko hayo.

Kwa maana huyo nakushauri kuwa endelea kufanya kazi. Tena Fanya kwa bidii. Hizo hiace zikusaidie kufanya nilichokwambia kuliko zikufanye uache kazi
 
Hahaaa coment kutoka kwa Mfanya kazu mtiifu.

Ulicho andika hapa ni Mawazo yako ya uoga tupu.

Fear of Uknown.

Kwa kifupi hii ni hofu ya kuhofia kisicho kuwepo.

Yaani unahofu mtu kupata matatizo kabla hajapata?

Kwa kifupi Mfanyakazi kuacha kazi na kujiajiri ni vigumu sana kwa sababu ya Addiction
 
Komaa na ujasiriamali ila watanzania tunao jiita wasomi tumejaa uoga sana kufanya maamuzi ya kujitegemea!!
 
acha kazi uone cha moto
Usimtishe,anatakiwa apate Elimu ya ujasiliamali,sio kama anaacha ila anabadilisha aina ya kazi,alikuwa anasimamiwa akiachacha atakuwa anajisimamia,anachotakiwa nikuwa na nidhamu ya shughuli zake.
 
Kama una kaajira mzee hebu kashikilie.Huku kwenye biashara ni kugumu kuliko.Utakutana ma makodi na maushuru ambayo ukikaa chini utaona unaichangia tu serikali kodi na mwisho wa siku hutoki na kitu.Mimi nafikiri serikali ingeweka kodi zinazolipika ambazo zitamshawishi mfanyabiashara kulipa Kwa hiari.
 
Siamini sana kwenye dhana ya kutafuta mtaji kwenye kazi ya kuajiriwa... Nimewahi kudhani hivyo kipindi nikiwa kwenye ajira, labda ni mimi binafsi ila njia hii haikufanya kazi kabisa. Nakumbuka niliacha kazi rasmi na kuingia mtaani nikiwa na kiasi cha laki mbili tu (tsh 200,000/-)

Lakini business plan niliyokuwa nayo ilikuwa ya mamilioni. Thanks Gof kwani nilipambana na vikwazo ladhaa... Vingi kutoka kwa watu wa karibu hasa ndugu kwa vitisho kwamba nimefanya mistake itakayo nicost... (Hii iliambatana na kukosa msaada wowote wa hali na mali kutoka kwa watu wa karibu)

Mwaka wa 6 sasa na ninashukuru Mungu nimeanza kusimama na kuelekea katika lengo.

Angalizo:- Fuata moyo wako na target zako. Usiache kazi kwa mkumbo wa matajiri wa kusadikika wa Facebook na instagram (nadhani unanielewa) Seriously there's no easy money in the streets....

- jiandae kisaikoloji kupambana na wakatishaji tamaa. Pia kuanguka mara kadhaa kabla hujasimama na kuanza mwendo.

- Kubali kwamba mawazo uliyonayo au tuite business plan, sio wewe wakwanza kuifikiri na sio wakwanza pia kuifanyia kazi. Fanya research kwanza.

- Epuka kabisa kuanza biashara kwa mtaji mkubwa. Anza na mtaji wa akili na nguvu zako kabla hujaingiza pesa zako katika biashara.

MWISHO-

NIKUTAKIE KILA LA KHERI KATIKA MAISHA UTAKAYO YACHAGUA.
Usikatishwe tamaa na hawa wazee wa "job security" [emoji4]
 
nakushauri angalia moyo wako unakusukuma kufanya nn ndipo uanze kufanya maamuzi magumu utatoka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…