Tarakilishi
JF-Expert Member
- May 19, 2013
- 2,181
- 2,448
Mimi pia ushauri wangu ni kuwa acha kazi baada ya miaka mitano kutoka sasa. Katika kipindi hiki weka malengo ya muda mfupi sana kama miaka mitatu hivi ya kutanua biashara yako hiyo; lets say in three years uwe na haisi au noah tano, sita etc. Halafu miaka miwili inayofuata iwe ni kuwekeza katika biashara tofauti na hiyo ya usafirishaji. After five years, fanya tathmini kisha amua. Nimetoa ushauri huu kwakuwa nikijenga assumption ya profit of 35% of your sales inakuwa kama laki nane hivi. Matumizi yako ya familia itabidi yasizidi laki nane kamili ili biadhara isianguke. Na ili biashara yako ikue inabidi some of your profit have to be re invested. Kwa maana hiyo tokadirie utawekeza nusu ya faida; that means utabakiwa na laki nne kamili kila mwezi ya kula na familia.Mkuu, jipangie malengo yaani miaka 3 hadi 5 mbele halafu utaangalia unataka kufanya nini.
Ila endelea na ajira yako na ziachie Noah zikuingize pesa kama miaka 3 au 5 hivi.
Baada ya hapo utaangalia upanue biashara hiyo au uanzishe biashara ingine.
Kwa mfano kama una nyumba ambayo ndiyo ya familia basi ongeza ingine uipangishe.
Pia anza ufugaji wa kisasa au ukulima wa kisasa yaani unanunua mashine ya kulimia ya kuvuna na unakuwa ukizikodisha.
Hivi vijimradi vidogovidogo vitakusaidia kufanya majumuisho ya mapato yako kwa mwezi na kwa mwaka.
Wakati unafanya haya yote ndiyo unajiandaa kuacha hiyo kazi yako.
Hivyo nakushauri uache kazi baada ya miaka 5 kuanzia sasa.
Kwa ujumla maamuzi ni yako; ila kwasasa nakushauri uvute subira kidogo kwa miaka mitano ambayo iwe ni ya uwekezaji kwelikweli; ujinyime na ufunge mkanda kwaajili ya uwekezaji hususani kwenye kutanua biashara yako ya sasa na kufungua biashara mpya.
Kimsingi unaweza kuamua kuacha kazi hata sasa hivi na biashara yako ikashamiri vyema zaidi kuliko sasa. Lakin kiukweli ni kuwa risk level bado ipo juu sana kwakuwa noah mbili bado hazikupi fursa ya kutegemea zenyewe kwa zenyewe at the time of crisis. Binafsi ni muumini wa kujiajiri na ninapenda kujiajiri; nakushauri kama roho yako ikikupa wasaa wa kufanya kazi basi endelea lkn weka kikomo cha muda na goals. Ushauri wangu ni miaka mitano inatosha kabisa kwako kufanya maamuzi magumu; changamoto za biashara utakuwa umeziona kiasi cha kutosha na biashara utakuwa umeizoea.