Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

The higher the calculated risk the higher the profit.

Hakuna bilionea aliefanikiwa kwa kuajiriwa..hayupo! Ukitaka kuyamudu maisha lazma utoke kwenye comfort zone yako ya kuajiriwa uje mtaani ukiwa na kacapital kako kadogo then uanze from the scratch down ili uijue biashara husika vizuri, from that stage kama kweli huko focused, disciplined and strong determined mafanikio kwako hayaepukiki.

Kila la kheri!
 
Wewe ni wale mnaoamini biashara lazima uanze na mabilioni. Btw hapa nazungumzia mentality ya Watanzania in general,whatever the business, mentality yao ni hii hii.
Rudi kwenye hoja ya mtoa mada ni mafanya kazi wa kuajiliwa kanunua NOAH mbili na sasa anashawishika kuacha kazi ili aendeshe mradi wake huo je ni wakati muafaka?? Acyana na kuanzisha biashara na kiwango cha mtaji hili lina utofauti kidogo na ombi la mtoa mada mkuu.
 
Halafu kazi yenyewe ukute ndo uticha...!!!
Hapo sihitaji ushauri aisee ni kama safari ya kuhama nchi hii yani sitafuti ushauri kwa mtu nikipata nafasi hiyo.
Fastaaaa..!!
Bwaga kamanda,kuajiriwa ndo mwisho wa akili zako hapo.!!
kumbe mkuu na ww una mpango wa kuhama nchi kama mimi? tuhame mkuu
 
Rudi kwenye hoja ya mtoa mada ni mafanya kazi wa kuajiliwa kanunua NOAH mbili na sasa anashawishika kuacha kazi ili aendeshe mradi wake huo je ni wakati muafaka?? Acyana na kuanzisha biashara na kiwango cha mtaji hili lina utofauti kidogo na ombi la mtoa mada mkuu.
Msimamo wangu uko wazi wala haujajificha.
 
Magari Si Biashara Ya Kueleweka. Tafuta Kipato Toka Biashara Isiyohamishika Kwanza. Ukishaona Umewekeza Vya Kutosha Ndipo Uache Huko. Wanaokuambia Usiache Kazi Bado Hawakutakii Mema. Huwezi Kutajirika Ukiwa Umeajiriwa
Tatizo sio kumshawishi asiache kazi bali kwa uwekezaji upi wa kumfanya aache kazi iliyo mpa mtaji??

Namkumbuka myaturu mmoja miaka ya 90+ nikiwa mbeya tech, alikuwa akiitwa ipini huyu bwana alikiwa ni stoo keeper lakin alikuwa ana vi hiace vya kutoka mbalizi tu mwanjelwa ,sokomatola zaid ya sita na kwa miaka hiyo alikuwa anatembelea hillux na toyota surf lakin kamwe hakuacha ile kazi yake pale ya kukusanya magodoro ya wanachuo na kurudisha magodoro pindi chuo kinapo funga na kufungua lakin alikuwa na pesa ya kutosha kabisa kuacha kazi ,nilijifunza kitu kikubwa sana kutokwa kwa mnyaturu yule sijui yupo wapi kwa sasa he was ma role model and he will till then.
 
Hofu ya kujiajiri ni kubwa na ndiyo maana kila wasomi wanataķa kuajiliwa na Serikali. Kikubwa ni kujiamini na kusimamia malengo yako.Fanya tathimini yako kwa kina, hangalia uzowefu wako kwa uwo Mradi wako mpya wa kujiajiri na huindae familia yako kiakili na kimazingira ili iweze kukubaliana na mabadiliko yoyote yatakayo tokea, Pia wapo watumishi wengine pamoja na ajira zao serikalini pia ni wajasiliamali wazuri tu.
 
Tatizo sio kumshawishi asiache kazi bali kwa uwekezaji upi wa kumfanya aache kazi iliyo mpa mtaji??

Namkumbuka myaturu mmoja miaka ya 90+ nikiwa mbeya tech, alikuwa akiitwa ipini huyu bwana alikiwa ni stoo keeper lakin alikuwa ana vi hiace vya kutoka mbalizi tu mwanjelwa ,sokomatola zaid ya sita na kwa miaka hiyo alikuwa anatembelea hillux na toyota surf lakin kamwe hakuacha ile kazi yake pale ya kukusanya magodoro ya wanachuo na kurudisha magodoro pindi chuo kinapo funga na kufungua lakin alikuwa na pesa ya kutosha kabisa kuacha kazi ,nilijifunza kitu kikubwa sana kutokwa kwa mnyaturu yule sijui yupo wapi kwa sasa he was ma role model and he will till then.
Watu Kama Hao Hawana Courage Ya Kujisimamia. Sikushauri Mtu Kama Huyo Awe Mfano Kwako. Hajiamini. Zipo Kazi Kweli Kuacha Unaitisha Ukoo Kujadili, Lakini Huyo Mtunza Stoo Ilibidi Aache Ili Ajira Kwa Wengine Zipatikane. Labda Kama Alikuwa Na Chanel Ya Udokozi/wizi
 
Hii nidham ya uoga sijui watanzania tunapoitoa jaman!! Why tunapenda kufanya kaz za watu? Mbona mimi niliacha kaz na kuanza kama machinga na sasa nina kipato mara 20 zaid ya nilivyokuwa kazin
Hoja hapa siyo nidhamu ya uoga bali aendelee na kazi ili aongeze more assets na miradi ndiyo aache kazi. Mfano akiwa kazini anaweza asiguse mapato ya Noa hence akaanzisha more projects...
 
ukitaka kufanya maamuzi magumu kama hayo usipoteze muda kuomba ushauri humu
Duuuuh kumbe ushauri wa humu JF ni useless?? Hii sikubaliani nayo...
Mkuu, jipangie malengo yaani miaka 3 hadi 5 mbele halafu utaangalia unataka kufanya nini.

Ila endelea na ajira yako na ziachie Noah zikuingize pesa kama miaka 3 au 5 hivi.

Baada ya hapo utaangalia upanue biashara hiyo au uanzishe biashara ingine.

Kwa mfano kama una nyumba ambayo ndiyo ya familia basi ongeza ingine uipangishe.

Pia anza ufugaji wa kisasa au ukulima wa kisasa yaani unanunua mashine ya kulimia ya kuvuna na unakuwa ukizikodisha.

Hivi vijimradi vidogovidogo vitakusaidia kufanya majumuisho ya mapato yako kwa mwezi na kwa mwaka.

Wakati unafanya haya yote ndiyo unajiandaa kuacha hiyo kazi yako.

Hivyo nakushauri uache kazi baada ya miaka 5 kuanzia sasa.
 
fuata moyo wako...

uchungu wa maisha yako unayo wewe hapo sio watu wengine...

kama bill gates angeajiriwa microsoft isingekuwepo leo....

kina bakhresa, mengi wameajiriwa nana nani
 
Duuuuh kumbe ushauri wa humu JF ni useless?? Hii sikubaliani nayo...
Mchache sana unaweza kuwa useful. Kuna makapi mengi sana humu sasa utachukuaje ushauri wa makapi? Hivi unaweza kuomba ushauri kutoka kwa mwajiriwa kuhusu kujiajiri.
 
Back
Top Bottom