Inapaswa Matarajio awekewe Walinzi kama kweli tu Wazalendo na tuna thamini mchango wakeWatu wengi kama wewe hawajui mchango wa tpdc kwenye uchumi ama maisha yao ya kila siku.
Watu wengi wanaijua TANESCO ila hawajui wanaosapoti tanesco kwenye kazi zake ni kina nani.
Kwa kukusaidia, umeme unauona unawaka nchi hii 60% unatokana na gas na hiyo gas mmiliki wake ni tpdc.
Tpdc anaiuzia gas tanesco kwenye mitambo yake ya kinyerezi, ubungo na pia tpdc anaiuzia gas songas ambayo inazalisha umeme inauizia tanesco.
Kwa hiyo zaidi ya 60% ya umeme unatokana na gas na mmiliki wa hiyo gas ni tpdc.
Tpdc ni kampuni yenye makusanyo ghafi zaidi ya bilioni 600 kwa mwaka, maana yake inakusanya zaidi ya bilioni 50 kwa mwezi kutokana nakuuza gas.
Pamoja na hilo tpdc ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia utafiti na uchimbaji wa gas na mafuta kwenye ardhi ya Tanzania.
Sheria ya mafuta ya mwaka 2015 iliipa tpdc mamlaka ya kua shirika la mafuta la taifa ama National Oil Company, hivyo inatakiwa ianze biashara ya kuagiza na kuuza mafuta kwa jumla na rejareja(bulk and retail) na sheria inaitaka tpdc iwe na umiliki wa 50% ama zaidi wa mafuta yanayoingizwa hapa nchini. Ndio maana unaona wameanza biashara ya kuuza mafuta, wameanzisha sheli(vituo vya kuuza mafuta) zao na wanatakiwa kila mwaka kujenga ama kurent/lease sheli 5 kwa mwaka.
Unaona kwa uchache tpdc ina ulaji mwingi sana maana wana mamlaka kama hawawezi jambo basi walipeleke kwenye private sector kwa sharing agreements. Unaona hapo jinsi kuna potential ya mikataba minono ya mafuta, gas na mambo kama hayo.
Mataragio toka ameingia pale amekua kikwazo kwa madalali na wapiga deal ambao wanataka mtu wao awepo pale awapitishie deals, mikataba na mambo kama hayo watajirike haraka. Ndio maana unaona kila siku zengwe juu yake.
Biashara ya Mafuta na Gas Dunian imejaa watu katili sana hata kufadhili uharamia mkubwa