Joyeuse
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 275
- 182
Wazima wana Jf.
Kama nilivyoeleza kwenye kichwa cha habari hapo juu.
Nina umri wa miaka 31. Nilimaliza shule ya msingi miaka 18 iliyopita. Sikufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari. Japo nilitaka sana kuendelea lakini hali ya nyumbani ilikuwa ngumu mno hivyo ikashindikakana hata kwenda zile shule za taasisi enzi zile.
Katika purukushani za maisha nilijichanga kipesa mwaka 2006 nikajiunga na elimu ya watu wazima ila majibu hayakuja mazuri bado nikashindwa tena kurudia kutokana na hali ya kifedha. Nikajitahidi tu kwenda English course nashukuru nimejua kingereza na pia nikasoma french course pia kifaransa najua.
Ila bado najiona sijakamilika bila elimu ,nataka kusoma. Mpaka leo hii kiu yangu nisome nifike chuo hasa. Japo naona watu wanaambizana haina haja ya kusoma bora kujiajiri lakini kujiajiri bila elimu sidhani kama unaweza fika mbali unless watu wakuendeshee.
Nina watoto 3 na mume pia.
Ila bado naitaka elimu ya sekondari.. na mara hii nimejipanga vizuri kabisa.
Je niko sahihi ama ndio nakumbuka shuka kushakucha??
Ushauri wenu ni muhimu sana kwa hili
Nannahitaji faraja na munipe moyo niweze kufanikisha hili
Natanguliza shukrani.