Nataka kuanza kuuza nguo kwa mtaji wa Tsh. 50,000/-

Nataka kuanza kuuza nguo kwa mtaji wa Tsh. 50,000/-

mdizi 2021

Member
Joined
May 4, 2021
Posts
55
Reaction score
52
Habarini wana group, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. mwishoni mwa mwezi huu nina mpango wa kuanza biashara ya NGUO, akiba yangu ni elfu 50.

Sehemu nilioiwaza ya kununua mzigo ni Karume nasikia hapo ukiwahi asubuhi saa 11 au 12 unapata nguo mzuri sana kwa bei ya elfu 5 au chini yake reja reja kwa nguo 1. Wana jamvi naomba mnipe maujanja jinsi ya kupata wateja haraka na changamoto zake hii biashara.

Nataka kutembeza maana sijapata sehemu ya kuweka ndo kwanza naanza. Najua humu wapo watu wazoefu waliobobea kwenye biashara hii. Pia nitashukuru sana mkinipa ramani ya sehemu ya kutembeza zenye wateja wengi hata mikoani nitashukur sana.

1624949334486.png

 
Hapo ukiwa makini utalaza hata 15,000 kwa siku cha msingi usikatae faida kidogo maana mwingine anataka kama amenunua shati elf 5000,aliuze 10,000. Hapo kupata mteja utapoteza muda wako wakati huko njiani utapishana na watu wengi wanaitaka hio bidhaa kwa 6000/7000. Usiweke faida kubwa.
 
Habarini wana group, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. mwishoni mwa mwezi huu nina mpango wa kuanza biashara ya NGUO, akiba yangu ni elfu 50.

Naomba nikuchoree ramani vizuri hapa....

Kabla ya kuanza kununua nguo nenda karume siku moja hiyo saa 11-12 angalia tu biashara inavyoensa na nguo zinavyouzwa na bei zake, toka hapo nenda Ilala boma hiyohiyo saa 11-12 angalia nguo zinavyotoka na bei zake.....

i) angalia nguo gani unataka ziuze, kwa mtaji wako unahitaji nguo ambazo zitatoka haraka basi nguo za wanachuo haswa mabinti na rika la wadada wa chuo na juu kidogo litakufaa......

2) angalia wanapenda nguo gani, nawewe unapenda kuuza nguo gani,

Mimi naonaga skin zinatoka tena ilalaboma ni 3000,4000 na chache 5000 ukinunua 10 ukaenda uza elfu 8 utapata 80 faida 30 na hizohizo skin jeans unaweza uza hata 10 niwewe tu.....

unaweza nunua track suits kama za kina zuchu kwa elfu 3 ukaenda ziweka vizuri ukauza kwa elfu 8,.....

unaweza nunua shiffon brouse japo ni ngumu kutusua nzuri maana wadada wanadesign zao wanazopenda za shiffon brouse

Unaweza nunua magauni mchanganyiko, ilala boma nilipata hadi magauni ya gucci kwa elfu 2000....

Unaweza nunua tshirt za kike na skirt za kike nzuri ukaenda uza ukapata pesa na mtaji ukakua.....

Kinachiangaliwa ni passion yako, yani wewe mwenyewe ufight huko uoate mzigo nzuri, kiasi kwamba wakitaka gauni, skin au tahrt nzuri wajue wanazipata kwako.....

mtumba unatoboa kweuoe sana angalia nguo gani zinavaliwa na wadada haswa wakubwa wa rika nililokutajia sio chini ya hapo.....pia angalia hali ya hewa ya huko usije ukachukua masweta etc utakwama.....ukipata vipochi na vibei pale nje ilala boma kwa 5000 wannavyofungua chukua....

jioni unapita kwenye hostels mbalimbali unawauzia au weekend ukiishanunua mzigo, unajisogeza unawauzia.....

kagua nguo magaunikagua kwenye shingo, mikononi, kwapani, na chini.....alafu na kiunoni lisiwe limetawanyika aaah libane kidogo.....

Skin kagua pia msamba usiwe mkubwa au umechakaa, check kiuno kisiwe kikuuubwa, kagua chini ikiwa imebana vzuri na inavutika pia itakuwa poa zaidi....

All the best
 
Back
Top Bottom