Habarini wana group, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. mwishoni mwa mwezi huu nina mpango wa kuanza biashara ya NGUO, akiba yangu ni elfu 50.
Sehemu nilioiwaza ya kununua mzigo ni Karume nasikia hapo ukiwahi asubuhi saa 11 au 12 unapata nguo mzuri sana kwa bei ya elfu 5 au chini yake reja reja kwa nguo 1. Wana jamvi naomba mnipe maujanja jinsi ya kupata wateja haraka na changamoto zake hii biashara.
Nataka kutembeza maana sijapata sehemu ya kuweka ndo kwanza naanza. Najua humu wapo watu wazoefu waliobobea kwenye biashara hii. Pia nitashukuru sana mkinipa ramani ya sehemu ya kutembeza zenye wateja wengi hata mikoani nitashukur sana.
Mwanangu, ngoja nishare uzoefu wangu
Nilifanya hii mambo 2015/16 japo indirect. Aisee inalipa, siku za wkend nilikua naenda Ilala pale asubuhi saa 11 niko kweny gari kutokea River-side. Nilikua nikifika pale nafanya survey kwanz kama dakika 10 to 20 hiv kuona wapi leo napata viwalo vikali.
Baada ya hapo nikawa naanza kuchagua sasa na bonge la fuko la debe 6 mwana. Siku wahi kulijaza ila manunuzi ya pale pia sikuwahi zidisha lak 1. Nilifanikiwa hadi kufahamika na baadhi ya wauzaji, wakanijua ni mzee wa wkend.
Aisee pale masaa yanavyosogea bei zinapanda. Niliwahi acha nguo za 1500 nikaja baada ya nusu saa nikakuta anauza 2500 [emoji1787]
Ila sikua nauza reja reja mwenyew. Nilikua mwajiriwa, nikawa na ndugu zangu wa 4 vijijin nikinunua natuma wanauza, so wkend nilizigawanya kila mmoja nikienda leo ni hadi wk 3 au 4 zipite, sometimez vijijin biashara ilikua inakua mbaya ila anawez enda hata mwez nanusu hajamaliza mzigo kwa mtu mmoja.
Ila baada ya sagula sagula ya Ilala nikawa nahamia k/koo kujazia vinguo special vya watoto, chupi za watoto, wanawake, shidilia, boxer kidogo japo hiz za wanaume hazikua fast moving.
Nilikua nikifika geto pale namwaga mzigo chin naanza kupanga bei za kuuzia kulingana na uzuri na bei niliyonunulia, nikawa natenga kwa kuweka kweny mifuko midogo midogo ikiwa na bei zake ndani. So kama waliuza zaidi ilikua no yao, mi nilikua nahitaji warudishe mtaji wangu tu, faida nilikua naigawa nusu yao nusu yangu.
Ila badae nilihama Dar nilikuana kero za usafiri na mafuriko nikasema nikajaribu maisha mikoani. Ila najipanga nitakuja tena nianze upya. Niliipenda hii biashara siyo siri.