Nitakushauri hivi wewe na watu wote wenye mawazo ya kuanzisha shule: Jambo muhimu sana sana ni kujitofautisha na wengine. Ilivyo ni kwamba kuna utitiri wa nursery school na kila unayokwenda unakuta ina sifa zile zile (kwa bahati mbaya sana ni sifa mbaya). 1. Ujanja janja wa kupiga fedha: Ukiondoa zile shule za maana kama Internatinal school, hizi nyingine zote wana vi-ada, vi-michango na tozo zisizo na maana. kwa mfano tu hili la kumpa mtu tenda ya kushona sare ni kero moja mbaya sana. Kwa nini kama umeamua wanafunzi wavae sare fulani usiwape uhuru wa kushona au kununua wanapotaka? Je, hakuna uwezekano wa wanafunzi kusoma kwa nguo za kawaida tu kama nchi nyingine? 2. Mazingira ya shule: Shule karibu zote nilizozungumzia zina mazingira yanayofanana i.e. ya hovyo, machafu, hakuna maua, miti wala bustani. 3. Vyakula vya hovyo: Vyakula navyo utadhani kuna sheria inataka walishe watoto vyakula vya aina moja. Wengi ni uji wa dona, ugali wa maharage nk. Anyway, kuna mengi sana yanafanya nursery zetu ziwe za kijima na wewe una nafasi ya kuanzisha kitu kipya (japo kwa style uliyoanza nayo tu naona utafuata mkondo). Mwisho nikuambie kuwa kama unataka kutengeneza faida ya mara moja kwenye shule, basi hiyo siyo biashara inayokufaa. Shule kwanza inatakiwa u-invest kwa muda ndiyo utaona matokeo yake.