Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,203
- 37,906
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna tatizo gani kwenye green colour?
bahati mbaya Sana Mimi nakuwa tofauti na wengine pindi ninapotaka kuanzisha Jambo langu, Mimi huwa naanzishaga tu bila kujiuliza maswali mengi, naanzishaga Kisha TRA watakuja, wizara itakuja, na wengine watakuja,Kisha tunakaa meza moja tunayajenga safar inaendelea, lakini ukifuata vigezo na mashart hata duka la vyombo la kawaida hutofungua.....inchi ngumu hiii
Kitu nilichojifunza wasomi tunachelewa sana kufanikiwa sababu tuna fanya analysis nyingi sana mwisho wa siku zinatukatisha tamaa.Tatizo sio majengo tatizo ni usajili wa hiyo shule kwa mjibu wa wizara husika.
Eneo liwe na 2accre ikiwa town ukiwa sio town accre7
Uombe kubali cha kujenga kwa kuwabatanisha yafuatayo
Hati ya kiwanja, uwezo wako 60m nk.
Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu vipi ulifanikiwa?Mi nilikua na makadirio ya milioni 25 kwa ujenzi wa madarasa na majengo yote ya shule.
mkuu umenena vyema, hizi shule zimekosa mvuta zaidi ya mtoto kujua English ya kuungaunga hakuna lingine pia inawadumaza watoto sana.Nitakushauri hivi wewe na watu wote wenye mawazo ya kuanzisha shule: Jambo muhimu sana sana ni kujitofautisha na wengine. Ilivyo ni kwamba kuna utitiri wa nursery school na kila unayokwenda unakuta ina sifa zile zile (kwa bahati mbaya sana ni sifa mbaya). 1. Ujanja janja wa kupiga fedha: Ukiondoa zile shule za maana kama Internatinal school, hizi nyingine zote wana vi-ada, vi-michango na tozo zisizo na maana. kwa mfano tu hili la kumpa mtu tenda ya kushona sare ni kero moja mbaya sana. Kwa nini kama umeamua wanafunzi wavae sare fulani usiwape uhuru wa kushona au kununua wanapotaka? Je, hakuna uwezekano wa wanafunzi kusoma kwa nguo za kawaida tu kama nchi nyingine? 2. Mazingira ya shule: Shule karibu zote nilizozungumzia zina mazingira yanayofanana i.e. ya hovyo, machafu, hakuna maua, miti wala bustani. 3. Vyakula vya hovyo: Vyakula navyo utadhani kuna sheria inataka walishe watoto vyakula vya aina moja. Wengi ni uji wa dona, ugali wa maharage nk. Anyway, kuna mengi sana yanafanya nursery zetu ziwe za kijima na wewe una nafasi ya kuanzisha kitu kipya (japo kwa style uliyoanza nayo tu naona utafuata mkondo). Mwisho nikuambie kuwa kama unataka kutengeneza faida ya mara moja kwenye shule, basi hiyo siyo biashara inayokufaa. Shule kwanza inatakiwa u-invest kwa muda ndiyo utaona matokeo yake.