Nataka kufanya biashara ya asali kutoka Tabora kuleta Dar es Salaam

Nataka kufanya biashara ya asali kutoka Tabora kuleta Dar es Salaam

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Posts
6,122
Reaction score
4,060
Salamu Waungwana wa Ukumbi huu adhimu.

Kuna visenti nimevipata mahali natafuta namna ya kuviongeza. Ninafikiria kufanya biashara ya Asali kwa kuanzia niende Tabora na kununua japo dumu mbili za lita ishirini ishirini za Asali mbichi ambapo nimeambiwa bei ya dumu la lita 5 ni kati ya shs Alfu 45 na 50 na kwa maana hiyo dumu mbili zenye lita 40 ni jumla ya shs Laki 4.

Napanga kuzileta dumu mbili hapa dar na kuiweka Asali kwenye chupa za ujazo wa lita moja moja ambapo huuzwa kwa bei ya kati ya shs Alfu 25 hadi 30 ambapo katika chupa zangu 40 ninatarajia kupata japo 1,000,000/ kwa bei ya shs 25 kila lita. Nikitoa shs 500,000/ za manunuzi ya asali na gharama nyinginezo ninabaki na Laki 5 za faida. Hii ni kws trip moja tu.

Ninakuombeni mnifahamishe Changamoto kadha wa kadha mnazoziona katiks Upambanaji wangu nonaofikiria kuujaribu kuufanya.

Karibuni.

1618301416487.png

 
Nawasubiria jamaa zangu waje watoe uzoefu wao! Mie mwenyewe nataka kujua.
 
Mimi kuna mtu ambaye ni my best friend anakuuzia lita 40 kwa sh 380,000 ukitaka asali iliyo safi na nzuri... niko Iringa....
 
Mimi napatika Singida hauna sababu yakufika Tabora ishia Singida nitakuuzia kwa 350000/= lita 20
 
Mkuu changamoto kubwa ya asali ni ubora tuu. wee zingatia ubora wa asali ama tafuta watu waaminifu ambao watakuwa wanakuuzia.
 
Michango yenu kuhusu changamoto za biashara hii inahitajika, ndugu zanguni...
 
Nachokiona unakaribisha madalali na kupigwa, ni nani amekwambia tabora asali ya lita 5 ni sh. 45000 hadi 50000??? Ngoja nikupe mchanganuo

  • Tabora mjini: lita 1 ni shilingi 7000, na lita 5 ni shilingi 35000.
  • Sikonge, huku ndipo ambapo asali nyingi inatoka na hao wanaouza tabora mjini wanafata huku na wananunua kama ifuatavyo: lita 1 sh.3000 na lita 5 shilingi 15000 kwenye kipindi cha high season, na kipindi kama hichi cha low season lita 1 inauzwa shilingi 4000 hadi 5500 na lita 5 inauzwa 20000 hadi 25000. Dumu la Lita 20 inauzwa kati ya 100000 hadi 120000

Hizo bei za sikonge ni tu pale kwa wauzaji wa jumla na sio kwenda dukani wanapouza rejareja.

Sio kila asali ni nzuri, nyingine zimechemshwa hivyo kuwa zaidi ya makini unaponunua kwa sababu utakosa wa kumuuzia.
Ni hayo tu, uliza swali kama unalo
 
Nachokiona unakaribisha madalali na kupigwa, ni nani amekwambia tabora asali ya lita 5 ni sh. 45000 hadi 50000??? Ngoja nikupe mchanganuo
- Tabora mjini: lita 1 ni shilingi 7000, na lita 5 ni shilingi 35000.
- Sikonge, huku ndipo ambapo asali nyingi inatoka na hao wanaouza tabora mjini wanafata huku na wananunua kama ifuatavyo: lita 1 sh.3000 na lita 5 shilingi 15000 kwenye kipindi cha high season, na kipindi kama hichi cha low season lita 1 inauzwa shilingi 4000 hadi 5500 na lita 5 inauzwa 20000 hadi 25000. Dumu la Lita 20 inauzwa kati ya 100000 hadi 120000
Hizo bei za sikonge ni tu pale kwa wauzaji wa jumla na sio kwenda dukani wanapouza rejareja.
Sio kila asali ni nzuri, nyingine zimechemshwa hivyo kuwa zaidi ya makini unaponunua kwa sababu utakosa wa kumuuzia.
Ni hayo tu, uliza swali kama unalo
Ninakushukuru mno mkuu Per Diem kwa mchango wako huu. Ubarikiwe. Nauliza mkuu, hizi bei unazozisema ni kwa ajili ua asali mbichi ya nyuki wadogo ama ya nyuki wakubwa?
 
Kwa hii mitaa yetu ya mbezi mwisho huku mor rd hiyo ni bei ya nyuki wakubwa! Asali mbichi ya nyuki wadogo tunauziwa hadi 30! Labda tunagongwa???[emoji15]
Kama unazungumzia nyuki wa kubwa sawa
 
Kwa asali mbichi yenye ubora ya nyuki wakubwa napatika Dar es Salaam , buguruni sheli unaona mzigo ndo unachukua bei dumu la lita 20 bei yake 200000 karibun
 
Kwa asali mbichi yenye ubora ya nyuki wakubwa napatika Dar es Salaam , buguruni sheli unaona mzigo ndo unachukua bei dumu la lita 20 bei yake 200000 karibun
bado unachukua mzee?
 
Back
Top Bottom