Nataka kufuga nyuki kisasa

Hongera sana mkuu.
Hakika unazifi kunipatia hamasa.
Nmekuwa na lengo hili muda mrefu ila utekelezaji umekuwa mgumu kutokana na aina ya shamba nililo nalo.

Ipo siku nitakamilisha na mm
Kila jema liwe kwako
 
Leo wameenda kukagua mizinga...tumekuta mizinga 20 tu ndio imeingia.Wameikagua hakuna shida tunahisi labda kalenda yao imetupita
 
Hongera Mkuu jitaidi usiweke mizinga kwenye Mti ambao chini Kuna kichuguu Cha Mchwa maana Nyuki akai sehemu ambapo Mchwa wapo
Sikulijua hili mkuu,
Unaweza fahamu sababu gani inapelekea hili kitalaam?
 
Ndugu habari?
Vipi unaweza kunisaidia huko ulikopata shamba ni wapi na bei zao zikoje?
 
Nipe kazi ya kukuzalishia Makundi ya nyuki kwa mizinga yako hiyo yote 180- nnahitaji miezi 2 yote itajaa nyuki
Leo wameenda kukagua mizinga...tumekuta mizinga 20 tu ndio imeingia.Wameikagua hakuna shida tunahisi labda kalenda yao imetupita
Nyuki wakiwa wengi kutokana na kuwepo wingi wa Chakula chao utengeneza kundi jingine na kutafuta sehemu ingine na kuanza kundi jipya! Inaonekana maeneo jirani na ulipoweka mizinga kulikuwa na hayo 20 makundi ... Nyuki uwa na Scouts wanaotafuta maeneo bora ya kukaa so wakaona hiyo 20 mizinga na kuamia. Wakati wa kiangazi ni Nadra makundi kuongezeka na pia upatikanaji wa Chakula chao pia kunaweza Changia Nyuki kutozalisha makundi mapya.... hapo Technology hutumika na kuzalisha idadi yoyote ile ya Makundi ya Nyuki( kwa kuanza kwanza kuzalisha Malkia wao) ulaya na Kwengineko Kuna makampuni kazi yao ni kuzalisha Makundi ya nyuki na kuuza. Karibu tuongee tuje tukuzalsihie makundi ya Nyuki idadi utakayo! BEI MAELEWANO😁
 

Attachments

  • IMG_0707.jpeg
    668.4 KB · Views: 10
  • IMG_0708.jpeg
    788.3 KB · Views: 10
  • IMG_0709.jpeg
    444.3 KB · Views: 10
Habari mkuu, ulifanikiwa ? Mrejesho ukoje ni mwezi wa nane sasa
 
Boss kwa makadirio ya kawaida, kuzalisha makundi 100 ya nyuki kwa teknolojia yenu itanihitaji niwe na kiasi gani cha fedha?.
 
Boss kwa makadirio ya kawaida, kuzalisha makundi 100 ya nyuki kwa teknolojia yenu itanihitaji niwe na kiasi gani cha fedha?.
Kundi moja + Malkia ni 50,000 . Ambapo baada ya hapo utawingiza kwenye mzinga na Malkia ataanza taga mayai, na kuanza kuzaliwa nyuki ndani ya mzinga na workers wataanza zalisha asali na mzinga kuanza jaa Nyuki na Asali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…