Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Mimi nafunga ndoa mwezi huu isee, nilikuwa nataka kufanya hii style nimemwambia wife Mimi nataka ndoa tu kanisani then tusepe zetu, ila yeye anataka sherehe nimemwambia sherehe atafanya yeye huko ukumbini Mimi kipindi hiko Niko geto, akimaliza sherehe anitafute, sipendagi usumbufu isee
Wanaume wengi hawapendi mbwembwe na sherehe, tatizo lipo kwa upande wa pili.
 
Inawezekana mkuu, Mimi nikikumbuka yakwangu mbaka nacheka.
Nilishtukizatuu watu wakashangaa ninafungandoa wakaja kanisani ilenatokatu naingia kwenye kimeochangu na wife naona watu rundo wananipigia vigelegele na magari yananifuata sijui ilikuwaje wengine nikawakuta home dah nilishangaasana.

Walinilaumu sana, wakajichangisha michango ya gafla waka nunua gambe sherehe ikawa hapohapo nyumbani hadi saa saba usiku maana kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndio walikuwa wakipigiana cm na kuongezeka.
Kwakweli sikuamini.
Mimi nimchangiaji mzuri wa harusi za wenzangu lakini yangu sikutaka kusumbua mtu nikaamua kufanya kimyakimya.


Hii Ndio Tabu ya Waswahili ni wagumu sana kuheshimu hisia za Mtu!! Wanapenda sana kupangiana mambo. Na wengine hujiapiza siku ya harusi ya mwanangu au kaka/dada/best lazima niweke kufuru. Hata kama mwenyewe hutaki.

Kwangu iliiuwa ngumu sana kukiepuka kikombe. Shori mwenyewe mwanza alijidai hata yeye hapendi harusi kumbe ilijuwa fix tu. Siku zilivyoenda presure ilikuwa kubwa sana. Japo niliweka shinikizo kuwakera watu wasuse kama kupiga marufu gambe lakini siku fua dafu.
 
Wanaume wengi hawapendi mambo ya sherehe sometimes hawa dada zetu ndio wanaforce sana.
Aisee ulijuaje maana hata mimi pia huwa sipendi complications maishani.Ikibidi hata nisichangishe watu kabisa, Ila nahisi bibie lazma agome wanawake hawa wana kasumba ya kutambiana.
Hapa hesabu video & photoshoot kali, ukumbi mkali, gari ya kifahari ya kutubeba on the event havikwepeki aisee.
 
Mkuu wewe sio wa Kwanza nahisi unaweza kuwa wa 999991.04 maana hata mimi nilifunga ndoa ya hivyo mwaka 2010 mpaka leo tunaishi na mwenzangu bila shida na tumejaaliwa watoto wawili.

Mimi niliona usumbufu kujaza watu na kuwakamua hela zao ingawa kwa kipindi kile madili yalikuwa mengi tu wala isingekuwa shida kuwachangisha watu.

So kama umeamua hivyo go on hakuna atakaye kuona wewe kituko kwenye jamii zetu.
 
Mkuu mbona fresh tu...Kama mambo unaona sio mazuri kipesa wewe nenda kale kiapo kanisani inatosha tu.. Sherehe ni Ziada
Mkuu, nilisimamia harusi ya kijana mmoja anasoma UDM ilikuwa simple sana, haikuwa na michango wala nini, kijana baada ya kutoka kanisani, hafla ilifanyika uwanja wa maonyesho wa mal Nyerere tena nje siyo ukumbini, watu walidhani ni kikao cha harusi baada ya kujua ni sherehe ya harusi walisogea kuona maana hawakuamini. Nilimpongeza sana kijana yule kwa kumuambia watu tunasoma kujikomboa kifikra na siyo kufanya mumbo kwa kukariri, tunakuwa watumwa wa mawazo ya watu. Tukatae.
 
Kisheria ndoa lazima iwe na sherehe.Ingawa sheria ya ndoa haijasema sherehe iwe vipi.Kwa hiyo fanyeni sherehe hata ya watu kumi tu haina tatizo.


Mkuu naomba nisaidie hicho kifungu cha sheria kinachosema

NDOA LAZIMA UWE NA SHEREHE
 
Aisee ulijuaje maana hata mimi pia huwa sipendi complications maishani.Ikibidi hata nisichangishe watu kabisa, Ila nahisi bibie lazma agome wanawake hawa wana kasumba ya kutambiana.
Hapa hesabu video & photoshoot kali, ukumbi mkali, gari ya kifahari ya kutubeba on the event havikwepeki aisee.
Wenyewe wanakwambia lile tukio linatokea once in life so lazima washerekee.
 
Ndio mpango wangu huo, nitaenda kufunga ndoa. Tukimaliza tunaenda zetu honeymoon, watu wanaosubiria sherehe wakafanyie kwao.
 
Wenyewe wanakwambia lile tukio linatokea once in life so lazima washerekee.
Ofcourse ni sahihi kufanya sherehe but wasting millions in a couple hours is the issue. Mnakula na kunywa 25-100 millions, Seriously???
Kitu ambacho mngeweza tumia mil.5 tu ku organise ka tafrija ka wanandugu wa pande zote mkala pilau na kupiga picha kwenye eneo zuri tu ingetosha. Ndio maana wengi wetu tunachelewa kuoa hali ya maisha ni ngumu kuridhisha fantasies za wanawake wa kileo.
 
Back
Top Bottom