Nataka kufungua duka la mchele, naomba ushauri

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
368
Reaction score
556
Nina mpango wa kufungua store ya mchele DSM, sipo kwa muda wa miaka 3.

Bahati nimefanikiwa kupata mashamba /mkoani Katavi, hivyo source kubwa ningetarajia kwanza iwe kutoka shambani, japo kwa sasa nilitaka niingie na Tone 2 nikiwa na cash Mil.2

Najua mtaji wangu unaweza kuonekana mdogo sana, lakini nilitaka kuwa na mwanzo mzuri/strong starting base point ambayo itaniruhusu kukua kwa uhakika sustainably

Naomba mawazo yenu. Nifungue maeneo gani jijini? Nahitaji vitu/vifaa gani japo vya msingi kama mizani nafahamu lakini aina gani nzuri kwa mfano. Vipi taratibu za vibali kama TRA serikali za mitaa nk, lakini wapi pia na vipi naweza ku rely kupata mzigo pale napo pungukiwa?

Nawashukuru sana kwa mawazo yenu na Mungu awabariki mtakao nichangia mawazo na uzoefu.

Akhsanteni.
 
Hongera ni wazo zuri sana, kuhusu mzigo Sehemu ziko nyingi wanazilima mpunga, Kyela_Mbeya, Usangu_Mbeya, Shinyanga, Bahi_Dodoma,Morogoro nk!wewe tuu na utafutaji.
 
Tani mbili sio mzigo wa kufungua kitu kinaitwa "store ya mchele" tena hapo unataka uutoe Katavi. Hiyo ni kianzio cha kufungua duka la mchele, sio store kibongobongo.

Ukisema store kwa lugha ya mtaani ni kwamba unauza jumla, sasa jumla gani ya tani mbili. Direct cost za mchele huwa ziko juu sana. Faida ya mchele huwa haizidi 200TSH kwa kilo hapo ni maximum, ukipata 50TSH/kg kawaida ukipata 100TSH/kg uko vizuri.

Chukua wastani wa 100TSH/kg zidisha na tani 2 hapo faida ya wastani baada ya kila kitu ni 200,000.
Hiyo ni profit baada ya kutoa ushuru wa kusafirisha, gharama za kusafirisha, kupakia na kushusha, kupaka mafuta, kuuchekecha kwenye mashine (grading), kulipia viroba na packaging, kusafirisha kutoka ambapo gari litaushusha mpaka store yako (probably utaungana na wenzio wanaoshusha soko la Tandika).

Anyway nisiandike sana. Hiyo ni biashara kichaa kwa mpango ulionao na uwezo wako. Najua watakuja motivation speakers wa JF waseme nina wivu na negativity ila nasisitiza kwa kubold na kupigia mstari. Hiyo ni biashara kichaa.

Badala yake bora uanzishe duka (sio store) la nafaka mbalimbali za rejareja. Naona una mtaji mdogo mkuu
 
Nyongeza ya hapo, kumbe una milioni 2 net, haiwezi kukupa tani mbili mpaka zikafika Dar. Atakayesema inaweza aseme inawezaje uone maajabu.
 
Tani mbili sio mzigo wa kufungua kitu kinaitwa "store ya mchele" tena hapo unataka uutoe Katavi. Hiyo ni kianzio cha kufungua duka la mchele, sio store kibongobongo.

Ukisema store kwa lugha ya mtaani ni kwamba unauza jumla, sasa jumla gani ya tani mbili. Direct cost za mchele huwa ziko juu sana. Faida ya mchele huwa haizidi 200TSH kwa kilo hapo ni maximum, ukipata 50TSH/kg kawaida ukipata 100TSH/kg uko vizuri.

Chukua wastani wa 100TSH/kg zidisha na tani 2 hapo faida ya wastani baada ya kila kitu ni 200,000.
Hiyo ni profit baada ya kutoa ushuru wa kusafirisha, gharama za kusafirisha, kupakia na kushusha, kupaka mafuta, kuuchekecha kwenye mashine (grading), kulipia viroba na packaging, kusafirisha kutoka ambapo gari litaushusha mpaka store yako (probably utaungana na wenzio wanaoshusha soko la Tandika).

Anyway nisiandike sana. Hiyo ni biashara kichaa kwa mpango ulionao na uwezo wako. Najua watakuja motivation speakers wa JF waseme nina wivu na negativity ila nasisitiza kwa kubold na kupigia mstari. Hiyo ni biashara kichaa.

Badala yake bora uanzishe duka (sio store) la nafaka mbalimbali za rejareja. Naona una mtaji mdogo mkuu
Asante kwa mchango mkuu
 
Back
Top Bottom