Mkuu wazo zuri, na nikupongeze kwa ujasiri wako wa kuacha ajira ili kujiajiri, pokea maua yako, ni wachache sana wanaweza hili...
Kwanza kuhusu mgahawa ku deal na aina mbili za vyakula ( Biriani na pilau ) Naona kijiwe( mgahawa) utafifia kwa namna fulani, kwasababu...
Biriani ni aina ya chakula chenye viungo vingi sana, huwezi kufululiza kula kila siku lazima tu utakinai... yaani vile viungo ndio vitakukinaisha au utapoteza hamu ya hiko chakula.
Chakula aina ya biriani kinafaa kuliwa mara moja moja sana kutokana na uwingi wa viungo vyake, kwaicho ukifululiza kuuza biriani kila siku, kuna asilimia nyingi za chakula kubaki.
Ushauri wangu, mgahawa wako usi base kwenye biriani na pilau tu, Weka vyakula vyakula vyote vya kiswahili na jitahidi kuwa m'bunifu.
Mfano : ugali unaweza kuweka na mboga kama dagaa, kisamvu cha karanga, matembele, maharage yaliyoungwa nazi, samaki / kuku / maini / nyama choma ( kimoja wapo kati ya hivyo ) bila kusahau na mrenda.
Wali mzuri wa mafuta uliotiwa nazi na mboga mboga nyengine zenye ladha.
Hivyo biriani na pilau ni extras tu maana hapa katikati ya week watu hawatakua na mzuka navyo kama nilivyokwambia biriani inakinaisha.
Zingatio : Jitahidi sana kua mbunifu jikoni, hakikisha kinatoka chakula chenye ladha / kitamu sana.
Mwisho : Ukitaka kufanikiwa kwenye hii biashara cheza sana na social media hasa Instagram, inabidi uwe mtundu hasa wa kuandaa contents, kuandika captions zenye mtiririko mzuri unaovutia na usio chosha n.k
Naamini utafanikiwa, kila la kheri kwenye safari yako. Kwakua mimi naishi kinondoni, nitakua mteja wako wa kudumu.