Nataka kufungua mgahawa ambao utakuwa maalum kwa kuuza Biriani tu maeneo ya Kinondoni

Nimekusoma mkuu, kila la kheri
 
Nashkuru sana kwa ushauri.
Samahani, unafkiri kwa maeneo ya Kinondoni na viunga vyake biashara ya biriani haiwezi kuwa yenye mafanikio zaidi ya biashara ya mishkaki ya kuku?
Biriani ni chakula kizuri na nichakula pendwa hasa siku za ijumaa ukiweka mambo vizuri watu wanafuata kile kilicho bora. Usikate tamaa kwenye ushindani na Muamini sana Mungu wako
 
Naipenda sana hii kazi ya chakula, hata hapa nilipo kuna vulnerability kubwa sana katika industry hiyo, in short watu ni kama wanachemsha chakula wanauza, hakuna hata siku 1 nimekula nikisema naam nimepata standard ya chakula kinachopendwa na kila mtu

ila tatizo kwangu Mimi kwenye suala hilo ni kama morinyo(yaani sjui kupika) sasa naogopa sana unaweza mpa mtu mawazo mazuri mazuri ambae ndio atakuwa mtaalam(chef) project yako umuombe mamba(The Quality & standard product) ila baada ya execution anakuletea kenge au mjusi mamba hahaha

ila kwa miji yote inayokuwa kwakeli kuna hii vulnerability hivyo kwa mtu anaeweza kuleta Quality na standard kwenye chakula bila kujali kwa aina gani kama ana capital basi aingie, in fact mama zetu(mama lishe) wengi wa huku miji midogo kama goba, Madale, tegeta na kwingeneko ukweli ni kwamba wanafanya kwa mazoea sana ukiwa fund na ukiwa serious unafanya kazi

Kuna watu wengi sana nikiwemo Mimi tunakula kwa hawa wamama sometimes kwasababu tu mazingira haya hamna mtu anaetua Huduma nzuri kuliko wao

Binafsi kwenye jambo hilo Mimi ni mbaguzi sana, naangalia kuanzia meza yako, kiti mpaka sahani yako kwa nje ipo vipi, chakula cha majumbani kwa watu huwa sifanyi hivi ila hivi vinavyouzwa basi kiukweli nakuwaga hivi sana
 
Nilikuwa nasikia tu biliani biliani, ... ile nakuja kukutana na hiyo biliani sasaa ... yaani ni mamichele tu kama michele mingine ... afadhali hata pilau tena BHAHEBHU!
 
Wabongo wanajua biryani ni ijumaa tu,sa itakuwaje?
 
Biashara ya chakula,yenye usafi,ubunifu na mapishi mazuri haijawah mkataa mtu….zingatia location,Jipe muda ijijenge na kujitangaza
 
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Nafkiri tumetofautiana kidogo.
Binafsi sikumbuki mara ya mwisho nilikula lini kwa mama ntilie kwa sababu ya kuchagua sana chakula kutokana na namna ya mapishi na mazingira ya kuanzia jiko, namna ya uandaaji, muandaaji wa chakula, mahali ninapotengewa chakula hadi vifaa na vyombo. Ikitokea nikila huona ni kheri niingie kwenye mgahawa nitumie hata 15,000/- kwa ajili ya wali samaki tu lakini nile hali ya kuwa nimeridhika. Bahati nzuri sina circle kubwa hapa mjini kwaiyo naweza kumaliza hata miezi sita bila kwenda nyumbani kwa mtu nikala chakula cha huko so kula kwangu zaidi ni nyumbani, na kama nakuwa na mizunguko mingi sana na kuspend muda mwingi nje ya nyumbani basi hutafuta mgahawa wenye kueleweka ninywe hata supu ya alfu 3 lakini sio kuingia kwa mama ntilie na kila wali maharage na mchuzi ambao naweza kula vijiko vitano nikaishia hapo.
 
Basi nahisi utaenda kufanya vizuri sana pia nakutakia kheri nyingi sana katika hilo!
 
Itapendeza. Biriani isiwe dhana ya Chakula cha Kiislamu. Ipatikane kila siku.

Sehemu nyingi huuza Ijumaa, kama vile kishushio cha Swala..
Pale tanga kila ijumaa nilikuwa naenda sehemu moja hivi "Kwa HAMZA", walikuwa na biriana nzuri sana aiseeh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…