Nataka kuhamia UDSM kutoka DUCE na kubadili kozi, inawezekana?

Inawezekana, ni ufaulu wako tu!

Changamoto ni mkopo kuchelewa kuhamishwa kutoka huko uliko (duce) kwa muda fulani kwenda udsm.
🙏🙏sawa kaka lakini mda uwo ukichelewa unaweza unakuwa haupati kabxa totally au
 
Muda ni baada ya kufungua chuo inaenda hadi wiki mbili dirisha linafungwa na maombi ya kuhama kozi hayafanywi kwenye ofisi za admission zinafanyika kwenye Academic Registration Information System(Aris) mfumo wa taarifa mbali mbali za wanafunzi nahisi baada ya kupata admission letter mtaambiwa mfungue huo mfumo...unaomba uko kuna kipengele cha program transfer chap kwa haraka tu kama umekidhi vigezo unachaguliwa tu kozi unayotaka ila muda mwingine wanataka uwe umelipa ada yote ya semester ndio uruhusiwe...Duce kwenda main campus ni rahisi kwa sababu ni chuo icho icho tu
 
Asante kwa maelezo yak ya kina🙏🙏 ila naomba niulize mfumo huo wote haupo online au ni lazma ufanyike chuoni
 
DUCE ni college ndani ya UDSM kwavile imejengwa nje ya main campus unajiona kama husomi UDSM. anyway fuatilia uhamie hapo Main Campus.
 
Ni kozi gani uliyachguliwa hapo DUCE?na ni kozi gani ambayo unataka kuhamia hapo main campus.?
 
Duce nimechaguliwa bachelor of education in science nataka bachelor of sciences in physics and chemistry ambayo iko udsm na duce haipo hio
Nakushauri baki DUCE ila soma bachelor of science with education (Physics and Chemistry). Hiyo bachelor of science in physics and chemistry ina changamoto mbili ambazo ni 1. Ugumu wa kuajiriwa na kujiajiri 2. Ugumu wa kupata GPA nzuri kwa uzoefu wa waliosoma hiyo programme pale UDSM.
 
Na mimi na mshauri asome hapo Duce hiyo program aliyo chaguliwa hiyo ya

UDSM anayotaka kuhamia itamsumbua baadae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…