Sema kariakoo watu Wana MAWE aisee!!! [emoji15][emoji15][emoji15]
Juzi kati nilikuwa hapo K/KOO natengeneza PC yangu kwa fundi mmoja kwenye kauchochoro kwenye haya maghorofa ya NHC.
Pembeni yangu alikaa mzee mmoja kavaa kawaida sana Wala sikumzingatia.
Mimi nilikuwa bize na mafundi wa Pc wakanipiga 30k Of ikapona.
Wakaja wadada wengine wawili wameleta mashine yao wakapigwa 40k matengenezo.
Sijakaa vizuri akatoka sista mmoja muonekano wa tomboy. Kavaa jinzi bwanga, tisheti KUBWAA!! na kasokota virasta kichwani. Mwendo wake wa kigumu sio kidada dada. Amevaa vile vibegi vya kiunoni kama vya diamond wanawekea simu sijui Hela.
Sasa akaja hadi kwa yule mzee ambaye sikumzingatia.
Sasa nahisi yule mzee kama sio mmiliki wa frem, meza, basi mganga yule [emoji2].
Sista akafungua zipu ya kile kibegi atakoa BURUNGUTU la Hela aisee Mimi mimacho kodoo!!! [emoji15].
Akahesabu fasta fasta kama teller wa benki wanavyojidai na Hela za watu, akampa mzee yule. Wakapiga stori mbili tatu, akaishia.
Nikasema tu huyu sista atakuwa na biziness yenye ujazo wa ukwasi hapa kati. At the same nikajionea huruma.
Kariakoo usimdharua hata wale wanatandaza biashara chini. Wanagonga Hela kuliko mtumishi wa umma wa huko TAMISENGA.