Nataka kujilipua na Volvo XC 90. Ushauri wenu wadau

Nataka kujilipua na Volvo XC 90. Ushauri wenu wadau

Unajua lkn Volvo inamilikiwa na Mchina Kama vile Landrover inavyomilikiwa na Mhindi?
Kuna nini cha ajabu hapo? Kwenye makampuni makubwa wawekezaji hutoka maeneo mbalimbali, lakini brand ni ya sehemu husika Mfano baada ya TATA group kumiliki JLR (jaguar Land Rover), bado brand na technology inayotumika ni kutoka UK,
 
Mkuu una uhakika? Umeona XC90 zilivyojaa hapa mjini? Nimeishi na Volvo tangu 2007 mpaka 2014. Mafundi wapo na Volvo ni gari moja simple sana kwenye matengenezo. Nazijua inside out hasa za mpakq mwaka 2012. Sasa hivi zimeanza kujaa xc60 za kuanzia 2012 na kuendelea nyingi ukiona inasumbua ujue mmiliki nae sio makini.
Unajua raha ya kuwa na babu kwenye kilinge ni raha sana, shukrani kwa kututia moyo sisi wenye tamaa na mindika isiyokuwa ya mjapani
 
Vipi spares zinapatikana?
Si mnunue magari ya uwezo wenu kuliko kuhangaika na vitu msivyo na uwezo navyo kisa kuwakoga watu? Mtu unanunua gari huku pressure imepanda to maximum.

Mara unaulizia kama spare zinapatikana, mara kama inakunywa mafuta kwa wingi, mara hiki mara kile... da. Hizi zote ni dalili kuwa huna uwezo wa kumiliki hilo gari.

Mwenye uwezo wa kumiliki gari anachagua gari analotaka, anafanya unasoma specifications zake, ananunnua gari. Hint: Kuna tofauti kati ya ''kuwa na uwezo wa kununua gari'' na ''kuwa na uwezo wa kumiliki gari''
 
Si mnunue magari ya uwezo wenu kuliko kuhangaika na vitu msivyo na uwezo navyo kisa kuwakoga watu? Mtu unanunua gari huku pressure imepanda to maximum...
Boss, yupo sahihi. Ni vizuri kununua gari baada ya research. Watanzania wengi uwezo ni kuwa na gari moja, sasa lazima ajue kuhusu spare na mafuta ili apime kama ni gari analoweza kulimiliki.
 
Mkuu umekereka Mimi kuuliza upatikanaji wa spares au kuna lingine mkuu?
Siwezi kukereka hata kidogo kwani hata kukujua sikujui. Nimesema ukweli kutokana na experince yangu ya watu wanaotaka kununua magari Bongo. BTW wabongo wengi ukiwa-criticize kwenye jambo lolote conlusion yao ni kuwa una wivu au huwatakii mema.
 
Swali likiulizwa linataka majibu, Comment yako Siyo jibu la swali husika!
 
Boss, yupo sahihi. Ni vizuri kununua gari baada ya research. Watanzania wengi uwezo ni kuwa na gari moja, sasa lazima ajue kuhusu spare na mafuta ili apime kama ni gari analoweza kulimiliki.
Yupo sahihi ndiyo na wala sipindi. Na ndivyo wanavyofanya watu wengi wenye uwezo mdogo. Na hiyo hasa ndiyo point yangu. Kujaribu kufanya hili kundi kubadilika kifikra. Kununua vitu kulingana na uwezo wao na siyo kuonyesha ufahari.
 
Ni klabu ya England inayomilikiwa na waarabu. Kwani kuna tatizo LR ikimilikiwa na wahindi? Maana naona ni kama unataka wasitamkwe
Swali ni kwamba ni klabu ya wapi! Wamiliki wanaweza kubadilika hata Dangote akijipanga akainunua Chelsea itabaki kuwa timu ya England. Mmiliki atakuwa Mnigeria!!
 
Yupo sahihi ndiyo na wala sipindi. Na ndivyo wanavyofanya watu wengi wenye uwezo mdogo. Na hiyo hasa ndiyo point yangu. Kujaribu kufanya hili kundi kubadilika kifikra. Kununua vitu kulingana na uwezo wao na siyo kuonyesha ufahari.
Okey boss
 
Back
Top Bottom