Nataka kujivua gamba ila.......................

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Nalewa hata katikati ya wiki....huyu mke wangu ananikondesha,ana mdomo nye acheni tu.
hapa naelekea nyumbani huku natunga sound za kumwingilia,
ni mbishi,ana kiburi,nikiwa serious kumweleza mambo ya msingi anaongea kitaarabu huku ameshika pua halafu anaondoka kwa kiburi huku akitembea kwa maringo na kuvibrate makalio makusudi,nikimpeleka kwenye vikao ya wazee akianza kuongea mpaka kikao inaharibika na kubakia mwenyewe kama mwenyekiti huku wengine kimya.
Kumchapa makofi naona huruma!
kumwacha napata wakati mgumu maana anajua kukata mauno kitandani mambo yake si kitoto ila siishi kwa amani.
amekubali nimwoe wa pili ?je nikimwoa wa pili akafundishwa taarabu si ndo wataunda bendi.

msaada bhandugu hapa kichwa kimeganda nimekaa katikati ya barabara magari yanipigia honi!
 
mpleke mashauzi classic modern taarab..
 
...lol....e bana eeee?

images
....kuna mtaalamu hapo nakushauri ukaonane nae...khaa?
 
duh mvumilia uyo mmoja, yaani mwanamke mmoja anakupeleka mbio mpaka ulimi nje, ndo uoe/ uongeze mke wa pili utakufa au utalazimika kuiama nyumba
 
yaani niko poa kabisa hata mtaalamu mwenyewe ataona niko kawaida tu
 
duh mvumilia uyo mmoja, yaani mwanamke mmoja anakupeleka mbio mpaka ulimi nje, ndo uoe/ uongeze mke wa pili utakufa au utalazimika kuiama nyumba
dah we labda hujakutana na mwanamke mwimba taarabu
 
Kamanda, watu wanaingia tarabu kwa pesa ,wewe unayo free ndani unataka kuikimbia?, komaa hapo hapo kamanda, ushasevu buku 5 ya kiingilio.
we hujawahi kwenda kwenye show halafu msanii mwenyewe anaboa ile mbaya???
 
Mimi waifu akileta za tarabu natunza hela tu, infakti mipasho ya kinamama inaniturn on kweli, ile akinitilia "babu utajijuuuu!" basi mimi mzuka ushapanda kitambo wala sihitaji maandalizi tena.

hahahahahahahaha! Aliyesema kloro mzima anahitaji vidonge vya asprin.
 
Mimi waifu akileta za tarabu natunza hela tu, infakti mipasho ya kinamama inaniturn on kweli, ile akinitilia "babu utajijuuuu!" basi mimi mzuka ushapanda kitambo wala sihitaji maandalizi tena.
we bonge la mvumilivu,mi kwa upande wangu palestina na israel inaweza kutokea chumbani
 
Pole excellent. Labda ungejaribiu kuepuka yale yanayompelekea kuchongoa mdomo sana. Kwa mfano ukirudi nyumbani straight from work mapemaa! Atachonga juu ya nini?
 
Back
Top Bottom