Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara

Dunia Kote Ukiwa Na Hisa Kwenye Kampuni, Ikipata Hasara Na Wewe Unapata - Ikipata Faida Na Wewe Unapata. Ndivyo Ilivyo.

Mtu Anaekwambia Eti Ukiwekeza Utapata Faida Tupu Ni Tapeli, Labda Kwenye Fixed Deposits Za Bank !
Hapo sasa itabidi ajiridhishe kuhusu uimara wa hiyo biashara na kampuni ili asije akapatwa na asiyoyatarajia, na muhimu kama ataridhika na mwenendo wa hiyo biashara/kampuni basi awe sehemu ya control hasa kwenye finances
 
Mkuu duka la mazaga (general mechandise) linalipa sana kama ukiliweka kwenye right location, asikudanganye mtu. Kama jamaa akikomaa na kusimamia biashara yake kwa uchungu, mbona atatoboa fresh tu!
 
Mkuu duka la mazaga (general mechandise) linalipa sana kama ukiliweka kwenye right location, asikudanganye mtu. Kama jamaa akikomaa na kusimamia biashara yake kwa uchungu, mbona atatoboa fresh tu!
Mkuu Mimi Nikisema Niuze "Pipi" Tu Kwa Wholesale.
Hata Kama Kila Pipi Nitapata Faida Ya Tsh 30 !
Nikisambaza Pipi 500,000 Tu Tayari Nina Tsh 15,000,000 !!
Kumbuka Pipi Ni FMCG Na Nchi Yetu Ni Kubwa, Hivyo Pipi Laki 5 Utasambaza Ndani Ya Hata Wiki 3 Tu !
Tena Utawasambazia Hao Hao Wenye Maduka. Ni Jambo La Kuwekeza Tu Kwenye Branding, Logistics Na Marketing !

Sasaa Wewe Mwenye Duka Utapata Faida Hiyo Baada Ya Muda Gani Na Mwendelezo Wa Biashara ya Duka Ni Upi ?

Maana Kwa Mimi Mtaji Ukikua Na Mzunguko Wako Ukikaa Vizuri Unaweza Hata Kukopa Ukafungua Kiwanda Cha Pipi.

Anyway sisi tulishazoea biashara zetu za maduka, grocery, bar, chipsy, bodaboda, genge, daladala na kama hizo.
To each his own !!
 
Kwanza umejiandaa na Side effect za mkopo biashara sio faida tu kuna kuchelewa kupata faida au kufa kabisa nakuishi na take-home ya 100K mwaka mmoja hutaweza himiri.

Minakushauri weka kwenye biashara pesayako mwenyewe ya savingi...save kwelikweli hadi kufikia 4M kwa mwaka unaweza kama huna mke then fanya reserch hasaa biashara isiyohitaji usimamizi mkubwa na iliyo na uwezo wa kukua mfano Carwash wekeza 4M yako mpaka utakapo jirizisha unapata faida yamaana kopa hata 10M wekeza kwelikweli ongeza mtaji kwenye biashara ya kwanza mtaji mwengine wekeza kwenye biashara ya pili hutajuta ukitumia njia hiyo.

Uzuri wa hii hata biashara ikizingua ni pesa yako haiasiri mshahara na ikifanikiwa hata mshahara take-home ikiwa 10,000/= wewe utaishi safi tu.
 
Biashara gani hiyo? Naweza nikawekeza
 
Jiandae kulia kilio kikuu.

Mjomba uandishi wako kweli wewe ni mwalimu au mnajimu?
 
This is either FOREVER LIVING, AIM GLOBAL, Q NET, NAMAINGO or Other Miradi ya Udufuaji of that kind.
 


CHUMA ULETE.
 
Ushauri mzuri
 
Kama una Mke asiye mtumishi muweke kwenye hyo biashara kisha na wewe uwe unaifuatilia kwa karibu. Tofauti na hapo ifanye wewe mwenyewe. Ukiajiri mtu anaweza akakutia hasara halafu ukachanganyikiwa bure! NB: haya yote tuyasemayo kuhusu hasara si lazima yatokee hivyo ila kuna uwezekano Mkubwa kutokea hayo!
 
Umelijibu vizuri sana hilo kenge....au lituambie lilishawahi kuanzisha idea gani mpya
 
Biashara ya duka ni kati ya biashara nzuri sana kama ukifuata misingi yake
1. Hakikisha location ni NZURI
2. Hakikisha bidhaa ZOTE ulizonazo zipo kwenye daftari.
3. Hakikisha duka lisiwe sehem ya utatuzi wa madeni yako kwa maana kutoa pesa hovyohovyo
4. Hakikisha unakagua mwenendo wa biashara angalau kila wiki kwa kupiga mahesabu ya mauzo na bidhaa.
5. USIRUHUSU mchumba wako awe anaingia dukani kuuza.
6. Hakikisha mtoa huduma awe muaminifu na wewe umuamini, tena inatakiwa wewe uwe ni msaidizi na mkaguzi tu, usiruhusu awe na muda wa kutoka bila sababu ya msingi.
7. KUKOPESHA NI KUFUKUZA WATEJA.
Hayo ni yangu mengine jiongeze
 
Inaitwa " a stepping stone business" yaani wafanyabiashara wengi kabla ya kuingia kwenye biashara nyingine walizonazo walianza kwenye hiyo biashara. Vitu vya msingi kuvijua kwenye biashara hiyo

1. Uaminifu na Weledi wa Kijana ni kitu cha kwanza ili ufanikiwe ktk biashara hii tumeshuhudia wafanyabiashara wengi wakianguka na wengine wakiamka tokana na Wasaidizi ktk biashara hizo

2. Faida ni ya uhakika ingawa ni ndogo inayokuwa kwa muda mrefu inabidi uwe mvumilivu sana ili duka likae sawa na mwanzoni uwe na ufuatiliaji wa karibu sana

3. Uchaguzi wa eneo la kufanya biashara nalo ni muhimu. Kwa mfano kuna eneo ambalo hakuna Muajiriwa hata mmoja, sehemu nyingine unakuta Waajiriwa wa kumwaga

4. Ukaguzi, Uchunguzi na Utunzaji kumbukumbu wa mara kwa mara ni muhimu sana itakusaidia kujua maendeleo ya biashara, itakusaidia kubaini mbinu za kibiashara, ville vile itasaidia kujua kama msaidizi ana mapungufu au laa
Unaweza mchunguza hata huyo kijana wako kama ana kauli njema kwa wateja au laa, yuko aggressive au laa kwa kutumia watu wengine ambao wataenda dukani kama wateja

5. Mahusiano mazuri toka kwa Suppliers na upande mwingine Customers ni kitu cha muhimu sana ili ufanikiwe bila kusahau mahusiano na taasisi za fedha Ukiwa na mahusiano mazuri na Suppliers ni rahisi kupata bidhaa nyingi kwa mali kauli upande wa Customers utajua mahitaji halisi ya wateja na wachache utaowakopesha watakulipa timely

6. Teknolojia ni muhimu katika utunzaji kumbukumbu vile vile hivi sasa kuna App maalum za kufanya Manunuzi directly kutoka kwa Manufacturer au Dealer na Software saidizi ktk Stock Traxking na Sales Tracking

7. Mahitaji ya Kisheria, hakikisha huna ugomvi na Serikali na Mamlaka zake kwa kulipa kodi na tozo zote zinazohitaji

8. Wekeza ktk kujifunza na kutaka ushauri. Tafuta Business Consultant akupe ushauri at least kila baada ya miezi 3 fanya nae kikao. Wekeza ktk kujifunza toka kwa wafanyabiashara wenzio. Nilishaona mtu anadaiwa kodi na TRA Tshs 60m lakini baada ya kutafuta Tax Consultant na kuziweka report zake vizuri alilipa Tshs 2.5m

9. Jitofautishe wewe na biashara yako, sio kwa sababu biashara ni yako basi kuwe hakuna mpangilio Baba, Mama, Watoto, Mjomba wanaingia na kutoka dukani kadri watakavyo. Kukiwa na hali kama hiyo wasaidizi dukani hufurahia sana kwani chochote kitakachotokea dukani hawatawajibika. Uhusiano.wako wewe na duka ni faida tuu, hivyo basi chochote utachochukua dukani lazima kiorodheshwe hatimae kilipwe au kikatwe kwenye faida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…