ushauri wangu kwako na kwenu wote mnaotaka kununua au kukopa tractor based on my experience, msichukue trekta kwa minajili ya kukodisha au kufanyia kaz za watu haijakaa vzr utalichosha mapema na inaweza isikulipe zaid ya kukupa unnecessary stress. Sbb wakulima wengi wanamiliki mashamba chini ya eka 3. Mara nyingi utajikuta ili ulime eka nyingi lazima utembee na tractor umbali mrefu na muda mwingi utajikuta unalitembeza trekta kwny njia mbovu ambayo nayo yana udongo/ardhi tofauti tofauti ngumu, laini, yenye mawe nk. Lkn pia trekta ni mashine haijatengenezwa kutembea tembea barabarani tena mbovu. Haya yote kwa ujumla wake yanalichosha trekta ila kama unashamba kubwa chukua trekta tumia kwa kazi zako. Na amini with proper management unaweza kukopa ilo trekta kama una 30 acres