Jamaa mmoja aliingia cha city.. Alianzisha mahusiano nje ya ndoa na mchepuko ambaye hakuwa gongo la mboto mwisho wa lami
Baada ya muda mchepuko akaja na wazo la kupanga ili kupunguza gharama za gesti na pia kwa sababu za kiusalama.. Mwana kakolezwa kakolea
Akamwambia bidada atafute chumba.. Chumba kikapatikana akapewa hela akalipie miezi sita.. Akalipia akapewa na mkataba kwa jina lake mpangaji
Maisha yakaanza na godoro alilopewa pesa akanunue, akanunua sita kwa sita na risiti yake kabisa kwa jina lake.. Mdogo mdogo akawa ananunuliwa vitu vya ndani na hata wakienda wote risiti alikuwa anachukua yeye kwa jina lake
Mambo yakaendelea mpaka akafunguliwa biashara ya duka la vinywaji na bites.. Na ili akopesheke ikabidi awe na leseni ya bishara.. Mkataba wa pango, leseni friji na kila kitu vyote alikuwa anaandika majina yake japo pesa hatoi yeye
Baada ya mwaka bidada akaanza kusumbua anataka atambulike rasmi kama mke mdogo! Jamaa akaona huu mtihani sasa dini yake haimruhusu kuoa wake wawili
Bidada visa vikazidi jamaa akikataa kulala kwake anamtishia ataleta mwanaume mwingine.. Baadae ikawa ni ugomvi kila wakati
Jamaa akaona isiwe tabu akaamua kubwaga manyanga kunusuru ndoa yake..lakini akaamua achukue kila kitu alichomnunulia yule mchepuko
Siku ya siku kaja na canter achukue vyake binti kakimbilia kwa mjumbe kwamba anaibiwa.. Jamaa kuja kuulizwa anasema ni vitu vyake kaamua kuvichukua akaombwa ushahidi hana
Binti yeye katoa mikataba na rundo la risiti kwa kila alichokuwa ananunuliwa.. Risiti zote zilikuwa kwa majina yake kuanzia nyumbani mpaka kwenye biashara.. Jamaa kabaki katumbua macho
Kwa panic na hasira akawa anachimba mkwara wa kumfanyizia mchepuko wake.. Akaambiwa akithubutu ajue kila kitu kitafika kwa mkewe.....[emoji23]
Sent using
Jamii Forums mobile app