Nataka kumfungulia mchepuko wangu duka la bidhaa za kike (urembo) na watoto. Nipeni ushauri kuhusu bajeti na mahala sahihi hapa dar

Naunga mkono hoja!
 
Mi nadhani kwa vile mara nyingi hizi pesa tunazohonga sio "hard earned money", ngoja tu wanawake wazifaidi. Hela ya jasho haiwezi kuhongeka hata siku moja, ila hii ya deals nk ngoja waitafune.
 
Nani kakwambia mchepuko unafunguliwa biashara? Jiandae kupigwa matukio mazito huko mbele
 
Sasa kwanini mlioa, aisee hii dynamic siielewi kabisa. Yaani umekubaliana kabisa na mtu kuwa tutakuwa sisi wawili tu halafu unaanza kuuvunja mkataba kifisadi. Sasa sibora utoe taraka, yote hayo ya nini. Halafu tunaita wake sio waaminifu ila sisi tunasigina sheria kinoma. Ungefunga ndoa isiyosema siyo sisi 2 ningekuona wa maana. Ila this is stupidity. Tuhurumieni dada zetu, nao ni binadamu.
 
Mwingine huyu hapa. Naona unamkaribisha shetani sebuleni. Jivuruge mkuu jiwashie moto. Kila la kheri.
 
Unashirikishaje watu Dhambi zako? Sisi tuna yetu na Muumba hatujayamaliza tafafhali na nnakuambia Acha UZINZI
 
Nimesoma kila neno mzinifu wewe...

Mkeo kuua biashara haina maana hana uzoefu
Eti jamani amejuaje kuwa mchepuko hataiua biashara? Biashara kufa hakuna sababu moja kwamba muhusika hana experience, ni sababu ila sio sababu pekee.

Comment yangu ni hiyo tu, hata hivyo naunga mkono hoja ya mchepuko kufunguliwa biashara, kwasababu kuna muda hawa watu ni wa muhimu sana, na tukisema kila mwanamke ajifungulie biashara mwenyewe, biashara zitakuwa za kuhesabika mjini hapa.
 
Na pia biashara zote hizi anazoziona zimesimama mjini, alishawahi kujiuliza zimechoma mitaji mara ngapi mpaka kufikia break even?

Binafsi sipingi mchepuko kufunguliwa biashara sababu hatujui ni kwa namna gani anamfaa mkuu, napinga mama mjengo kukatiwa tamaa.
 
Hapo ni kumuuwa tuu huyo mchepuko basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…