Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchina apewe , maua yake mkuuMimi nilianza biashara ya Usafirishaji miaka kama 10 iliyopita. Hata sasa hivi nafanya usafirishaji mizigo sana tu local ila kwakua imenibidi(Niko kwenye supply business) kwahiyo swala la kuwa na Gari linasaidia kupunguza gharama ya bidhaa nnazouza.
Ila kama ingekua ni uamuzi wangu nisingekuja kumiliki gari la mizigo tena KAMWE
Hio mil 100 tafuta biashara nyingine sio ya kuwa na gari moja.Ni Risk kubwa mno unajitafutia .Hakuna cha bima wala upuuzi wa bima. Utakufa siku sio zako
Ukiwa na magari mengi inasaidia kugawanyisha Risks. Madereva nao dahh kila siku ni kutishana na bastola mezani na kutiana lockup
Hakuna biashara pasua kichwa kama hii katika biashara zote nilizokwisha kufanya
Usione kina Usangu, Overland wanazungusha chuma tu kisauzi ila hii biashara sio mchezo.
Ungekua na mtaji wa Billion plus ningekushauri hata uanze kupambana na kina Sham Nunu na hao underdogs wengine na nisingekushauri huko kwenye Mascania. Howo anafanya vizuri sana saivi anaenda ligi za kina Daf/Volvo.
Amina MTUMISHIChukua Howo unapata ziro kilometer pamoja na unafuu wa spare parts pamoja na mafuta kiduchu kwakila kilometer unayotembea
Bhachu zinatengenezwa Kenya,Used yake kwa Tanzania labda uuziwe na matajiri wakubwa kama Usangu Logistics ndio walikuwa wananunua sana hizo trailer.Trailer used za BHACHU au HENRED FRUEHAUF zinaendaje wakuu
Na mimi ningependa kupata mrejesho wa R440Vipi mkuu? Ulifanikisha kununua R440 au ulibadilisha plan?
Nataka nianze na truck tatu la kichina kwa mkopo ,sina dowm payment . hivi wapi napata bila down payment😀nikopesheni truck wakuu
Well saidMkuu,
Nikupongeze sana kwa uthubutu huu.
Hii biashara ni nzuri ila ina changamoto zake za hapa na pale ila ina pesa.
Ili uweze kutoboa kwenye hii biashara jitahidi kumudu jazba zako kwa dereva wako tena hasa akiwa porini, Dereva ndiye mtu anayeweza kukufanya ufanikiwe na kukufanya ufeli mazima.
Trailer zipo za aina mbili,
Flatbed na Skelton
Kwa vile wewe ndiyo unaanza basi nakushauri uchukue flatbed kwa sababu kazi zote utabeba. Vilevile uchukue Trailer yenye (axles za BPW).
Kampuni zinazozalisha hizo trailer zipo nyingi hapo mjini, Superdoll, Simba na wengineo, Nashauri ununue trailer za mtumba.
Kikazi,
Kuna trip za local( za ndani)
Kuna trip za transit ( Nje ya nchi)
Trip za ndani sikushauri uzifanye kwasababu zinachosha gari na magurudumu. Ni bora ufanye hizo za Transit tu, tena za Dar - Lubumbashi tu.
Trip za Dar - Lubumbashi hazichoshi gari ingawa gari inachukua mwezi mzima au zaidi lakini pesa yake unaiona, Gari inaenda na mzigo na inarudi na mzigo (Copper)
Sasa ili uweze kufanya hizo trip za transit kwa mtu wa gari moja, nakushauri ufanye joint venture na mtu mwingine ambaye ana gari nyingi ili uweze kupata c28 ya TRA na hii itakusaidia kujikusanya na kujifunza mchezo.
Kwanini nasema hivyo, sijajua mfuko wako ukoje ila kuna mlolongo wa makadirio ya kodi, kukata vibali vya Zambia na mambo mengine, kwa gari moja ni story tu.
Mkuu, Magurudumu ya gari yako hakikisha umenote zile serial number na uwe mfwatiliaji wa kuyakagua kila baada ya trip.
Dereva mtaji wake ni Diseal na Magurudumu, akiishiwa huko njiani anayanywa fasta na yanauzika sana hapo Tunduma au huko Mpika.
Punguza wanawake (Mademu) magari ni kama Majini hayapendi uchafu wa mwili, na pia dereva asikuzooee sana maana wanakuwaga na vinasaba vya kiswahili unaweza kujikuta yeye ndiye kawa boss na wewe ukawa mfanyakazi wake. Zingatia Services ya gari, usifuge magonjwa kwenye gari!
Naomba niishie hapa,
Cheza na dola mkuu.
Shukrani
Kaka habari , rate za lubumbashi zikoje siku hizi, na gharama za kuvusha gari zikoje ?Wakuu,
Niseme machache.
Marehemu Rugemalila Mutahaba aliwai kusema maneno haya, naomba kumnukuu" Ukifanya biashara na haikupi changamoto basi hiyo biashara haina faida kwako achana nayo"
Akaenda mbali tena, Mjasiriamali wa kweli ni yule anayebadilika badilika huwez kukomaa na biashara ya aina moja tu kwa wakati wote, Mwisho wa nukuu.
Hii biashara ina changamoto zake lakini ina pesa, sehemu yeyote yenye changamoto pesa inapatikana hapo.
Scania 113M ni horse nzuri lakini ina mapungufu yake, hii gari haitumii umeme mwingi na ulaji wake wa diseal ni mkubwa, lakini pia haina Kitanda.
Kwa mfano trip ya Dar -Lubumbashi, halafu Lubumbashi - Dar hiyo gari inatumia diseal lita 2400 na muda mwingine mpaka 2500 wakati scania 114L, 124L inakula lita 2200.
Kwa ushauri wangu, unaweza kuanza na scania 114L yenye horse power 380 cabin ndogo. Au ukishindwa sana basi chukua DAF XF 95 manual, (camis engine)
View attachment 1484869
View attachment 1484870
Kama nilivyosema awali, Dereva ndiye mtu muhimu sana atakaye kutoa hapo ulipo mpaka sehemu uliyopanga wewe kufika. Tatizo kubwa kwenye hii biashara wamiliki wengi wanamchukulia dereva kama barmaid.
Dereva mzuri unampataje? Madereva wazuri siku zote wanaibwa kutoka kwenye makampuni mengine.
Tengeneza mofolojia ya kazi yako vizuri, kwa mfano kuna kampuni X inamlipa dereva mileage ya kwenda Lubumbashi na kurudi dar TSHS 1milion
Kiaje? Dereva anapewa shs 500k kwenda Lubumbashi na anavyoingia Mgodini kupakia copper unampatia dola 100, akirudi dar unampa shs 300k kama return mileage. Sasa dereva kama huyo kwanini asiheshimu kazi na kutunza gari lako vizuri..!
Kwenye hii kazi reporting ni muhimu sana, mwenye mzigo wake anataka kujua gari iko wapi na imelala wapi? Sasa ili uweze kwendana na hii ari huna budi kutengeneza Kanuni ambayo itakuwa kama katiba ya kazi ofisini kwako.
Dereva aanze safari saa moja asubuhi na ikifika saa kumi na mbili jioni apaki gari atafute guest alale na atume ujumbe kwako kukupa report. ( Kuwa mkali sana kwa dereva anayepuuzia hili)
Madhara ya kutembeza gari usiku ni makubwa sana na yanaweza kukufilisi kabisa na ukajuta kwanini uliingia kwenye hii biashara ya magari kama wanavyoelezea wadau hapo juu.
Breakdown, jitahidi sana kuepuka hitilafu za njiani, funga spare za uhakika ambazo utaweza zipata sub-scania au kwenye maduka mengine ambayo yako vizuri.
Na unapopata breakdown najua kichwa kinawaka moto na pressure inakuwa juu, jitahidi sana kujicontrol, pokea simu ya agent aliyekupakilisha mzigo au mteja mwenyewe mwambie ukweli na umpe uhakika wa usalama wa mzigo wake na uhakika wa kutoka hapo ulipo nasa.
Kutokupokea simu za hao watu kutakuharibia sana na siku nyingine utashindwa aminiwa na ukizingatia ndiyo kwanza unaanza.
Kwenye hii biashara tuna utatu mtakatifu, ambao ni Dereva, Agent / Wakala wa mizigo na Fundi wako wa gari, Hawa watu ishi nao vizuri, kuwa nao karibu kushindwa mchepuko wako.
Chonde chonde usiruhusu lori lako kubeba mkaa, (kama ni kagunia kamoja basi akamwagie maji ndiyo akabebe)
Rate za mizigo sokoni huwa zinabadilika kutoka na ari ilivyo kwa wakati huo na kabla ya kumpatia agent nyaraka zako za gari basi jiridhishe kwa kufanya utafiti kidogo wa bei maana nao ni watafutaji kama wewe.
Shukrani sana!
Muwe na jumapili njema iliyobarikiwa
Ndugu naomba Rates za likasi, au lubumbashi za sasa.Umenena vyema Tandamu GVM yake ni Tani 24 ,Wakati kipisi GVM yake ni Tani 18..Mimi kwa upande nina uzoevu na magari makubwa aina ya Howo na Shacman na biashara ninazosimamia ni za Transit .Transit ni biashara nzuri sana kama utakuwa na gari kwanzia nne .Pia ikiwa unaelekea Nchi kama Zambia au Drc kuna faida ya kurudi na either Copper ,Manganese au Soya kutoka Chingola,Zambia.Bei ya Lubumbashi ina range kutoka 5500Usd to 6500Usd based on cargo loaded na negotiation power yako.Kwa Kolwezi na Likasi(DRC) 6000Usd to 7000Usd. Pia kwa upande wa Zambia bei zinabadilikia kulingana na umbali na Uzito wa Mzigo Mfano Lusaka 4000Usd to 4500Usd ,Mpika 3200Usd ,Choma 4500usd to 5000usd. Kwa kifupi unapo bargain hizi price uwe makini kwa kuzingatia umbali ,Uzito na aina ya mzigo unaobeba .Uzito na umbali itakusaidia kupiga hesabu ya mafuta ili usijee ukapata hasara .Aina ya mzigo ni muhimu kuna mzigo kama sumu,suplur ,lami na chemicals zote zitahitaji additional cost ya vibali kutoka Mamlaka husika eg GCLA,TANROADS,etc.Pia kuna mzigo mipana OOG au Abnormal Cargo hizi ukitaka kutaja bei umakini unahitajika zaidi kwa maana hapa kuna cost nyingi zinaweza kujitokeza .Kama ni pana sana kama above 4m unaweza kujikuta unahitaji kibali cha Tanroads,Escort moja au mbili,Polisi,Route survey ,matangazo kwenye vyombo nya habari .Pia kwenye hizi OOG unaweza kujikuta kama urefu umeenda juu utahitaji escort ya Tanseco kwa ajil ya nyaya zao. So kwenye inahitaji umakini ila ni mizigo yenye faida kubwa sana kwa transporter wengi wanaiogopa kulingana na sheria zake .Mwisho madalali ni wazuri kwneye kazi lakini kuwa nao makini wanaweza kukulalia sana kwenye bei .Jitahidi hapa kama ni mzigo wa Sub uangalie kwanza gharama ya malipo usifanye bora liende.Kwa mwenye maoni na Ushauri anaweza changia pia.
Kaka habari , rate za lubumbashi zikoje siku hizi, na gharama za kuvusha gari zikoje ?
Rate ya kurudi na copper nayo ikoje, Asante sana ukinijibu utakuwa umenisidia sana