Tajiri wa Magomeni
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 4,274
- 2,935
vipi kuhusu hizi MAN naziona zimekuwa nyingi nyingi barabaraniGari ambazo nina uzoefu nazo ni Howo na Shacman.
Ngoja nianze na Howo .
Howo ni miongoni mwa Gari za Kichina nzuri sana hasa kwenye utumiaji wa mafuta .Ukitaka kununu gari kama hii ni vema ukanunua Brand new .Maana bei ya mpya inashabiana na Bei za Scania used.Faida ya Howo mpya ni kuwa ina utumiaji mzuri wa mafuta hasi kulingana Horse Power (HP) yake ni 371. Katika biashara ya magari kitengo cha mafuta ni chagamoto so unapoata gari inayokula mafuta vizuri inapungiza gharama za uendeshaji. Pili Howo ikiwa mpya na ukapata dereva mzuri na mzoefu itakuchukua muda mrefu sana kupata hitilafu za mara kwa mara.Kwa kifupoi haina breakown za mara kwa mara na itakuchukua miaka Mitano mpaka 8 kuanza kusumbua.Kwa hiyo miaka kama utakuwa umeitumia vizuri utakuwa umeshrushisha hela yako na umeshanunua nyingine tena .
Upatikanaji wa spare ni rahisi kwa Tanzania ka sasa kuna mawakala wengi wa SINOTRUCK hapa Bongo so spare si tatizo.Pia spare zake bei affordable
Hasara za Howo.
Life span ya hizi gari ni fupi ukiliganisha na gari kama Scania .So ni vizuri kuitunza vizuri ili na yenyewe ikutunze pia.Service za mara kwa mara ni muhimu .
Ni muhimu ni kuwa mafundi wazuri na wanajua gari si bora fundi. Ikupendeza mara moja moja uwaite wenyewe wachina waicheki.
Gari za Shacam.
Ni gari ngumu na zenye nguvu sana, Nguvu kubwa inatoka kuwa na Horse Power kubwa kuna za 420HP na 440 HP .HP kubwa inasababisha ulaji mkubwa wa mafuta .
Fiada za Shacman ni pamoja na kuwa na nguvu kubwa gari kama hiii ni ngumu kukwama sehemu za rough Roads.Hii inaweza kupita sehemu ngumu kwa mfani mvua inanyesha huko migodini ni ngumu sana kukwama.
Inawe uwezo wa kubeba mzigo mikubwa kwa mfano inaweza kuungwa na trailer ya Lowbed na ikabeba mzigo heavy sana.
Hasara ya Shacman
Utumiaji mkubwa wa mafuta huchangia gharama za kiu edeshaji kuwa kubwa.
Life span yake pia si ndefu kama ilivuo gari nyingi za kichina.