Japo sipo kwenye mood ya kuandika, lakini nikipita kimya nitakua sijakutendea vema wala kuitendea vyema nafsi yangu.
Nina uzoefu niseme wa kutosha kuweza kutoa 'expart opinions' kwa mtu anyetaka kuanza biashara ya usafirishaji kwa kumiliki malori.
Nawapongeza wachangiaji wenzangu kwenye uzi huu, ila kuna mawili matatu nimegundua toka kwa hao wenzangu japo kuu hasa ni hili.
-Wengi hawana taarifa kamili na sahihi juu ya bei na uhalisia wa aina anuai za magari pia uhalisia katika sekta nzima ya usafirishaji hapa nchini.
Wengi wameshauri na umeonesha kuridhika na ushauri juu ya kuanza na Fusi-tandam. Mimi kwa uzoefu wangu sikushauri kuanza na tandam kwa sababu zifuatazo;
+ Gharama. Ununuaji na ubireshaji wa tandam huweza kufika 80-100mil hii ni gharama kubwa sana kwa gari ya tandam ukilinganisha na performance yake barabarani.
+Matunzo. Tandam ina gharama kubwa sana katika matunzo hasa hasa engine. Ukumbuke ile ni engine yenye HP kama 200 hivi lakini inabebeshwa tani 18 hivyo injini huchoka haraka na kuhitaji kubadilishwa. Ni kawaida kwa life span ya injini kwenye tandam kuwa miaka minne japo mara nyingine huweza kujikongoja hadi 8 kutokana na nidhamu yako ya kuibebesha mzigo
+Mifumo ya uendeshaji. Tandam nyingi hasa hasa nikiwa ni mzigo hata tani 12 tu ujue haina uwezo wa breaking za ghafla so katika kipengere hiki tegemea neema ya Mungu na kuthibitisha hili fuatilia ajali za tandam kugonga gari nyingine kwa nyuma utaambiwa sababu.
Kama utaamua kuanza na gari toka ukoo wa mzee Mitsubishi basi achana na tandam ila chukua fuso kipisi beba tani zako 7au 8 baas. We mwenyewe jiulize tu gari ulikua designed kubeba tani 5 ila Bongo Pasua Kichwa Engineering wanaifanya ibebe tani 18.
USHAURI WANGU SASA.
Kwa mtaji wa milion 100, anza na gari ambayo gharama ya manunuzi yake hadi kuingia road yaani horse na trailer yake isizidi 80ml.
Hapa utaona kipi rahisi kwako either kuagiza used ulaya au used ya kibongo bongo, ambapo kwangu naona ni sawa tu japo hakikisha kama ni used ya kibongo bongo usichukue iliyoingia nchini zaidi ya miaka miwili nyuma.
Hapo ukitaka kuagiza ni vema ukaanza na gari ambazo ni rafiki kwa mafundi na vipuri vyake mara ipatapo faida. Nashauri Scania series 4 yoyote kati ya 114 au 124 horsepower yoyote hamna shida najua hiyo hadi inakaa road itakugharimu kwenye 60ml hivi na trela lake ni 20ml tu.
Anza na safari za local na kwa kuwa wewe ni mgeni basi kichwa chako ni halali ya Dalali na atakupiga sana katika miezi mitatu ya kwanza hadi kichwa kikukae sawa utengeneze wateja wako. Route zinatofautiana na msimu kwani kuna wakati nyanda za juu kubalipa na kuna wakati kanda ya ziwa kunalipa.
Oya nimechoka kutype, ntaendelea kesho