Fibanochi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2018
- 476
- 1,018
Basi itakuwa biashara zote za usafirishaji zina changamoto Sana, me sikuwahi kuwa na gari kubwa la biashara Ila nimewahi miliki Bajaj na pikipiki kadhaa, aiseee aisikwambie mtu.....yaani ni pasua kichwa vby mno!
Mkuu mie nakushauri anza na Fuso Tandam ndio utapiga pesa zaid. Ninakushauri hvo kwa kuwa hapa home tuna Scania tatu na Fuso mbili ila Fuso ndio zinapiga kazi kuliko Scania.
Na pia km ni Scania kwa wewe unaeanza sikushauri kwa kuwa ni sumbufu sana hasa ikishaanza kuchoka. Scania za kukutoa umaskini ni zile model za kizaman.
Na pia wanaokushauri kuhusu magari ya abiria naomba usiwasikilize kabisaa, maana yana changamoto nyingi sana. Mie binafsi nina Nissan Caravan mbili ila ni kichefu chefu kitupu.
NB: nimekushauri kutokana na uzoefu wangu wa kuishi na hayo magari kwa muda mrefu.