mlima wa mizeituni
JF-Expert Member
- Sep 7, 2019
- 1,387
- 2,444
Wiki hizo nilikuwa nafurahi sana kusafiri na tajiri!Asante kwa maelezo yako. Ni kweli biashara yoyote ni kujitolea muda wako kwa asilimia zote, hasa nchi kama yetu yenye culture ya watu kupenda kusukumwa kama ng'ombe. Kwa upande wa gari ndiyo zaidi kabisa. Bila wewe kuwepo mwenyewe kuwepo lazima utaumizwa.
Ukitaka kujua biashara ya usafirishaji imejaa watu wenye ''ubongo wa kupenda kuiba'' wewe nunua chombo cha usafiri kwa ajili ya biashara halafu ambatana nacho mara kwa mara.
Utachukiwa na dereva na hata watu wa pembeni. Utasikia wanabeza ''tajiri gani habanduki kwenye gari''. Nchi yetu ni nchi pekee watu mfanyakazi anachukia tajiri kusimamia kazi yake.
Akiwepo kwenye gari tunakula na kulala hotel, changamoto yoyote inashughulikiwa kwa wakati na muda mwingine alikuwa akinisaidia kuendesha gari!
Kwa kifupi sigusi posho ya safari!
Kwa scenario kama hiyo ningeanzaje kuchukia tajiri kuwepo kwenye gari?
Dereva anaehudumiwa vizuri haibi! Ukiona unaibiwa ujue umeweka mbele ukali/ujeuri usio na maana/na ukorofi wa kipuuzi kuliko kuboresha mazingira ya kazi ya dereva wako..
Kwa tabia hizo utaibiwa, utaibiwa, utaibiwa mpaka uchakae hata kama unalala kwenye cabin!
-Posho unatoa kidogo tena kwa masimango!
-Dereva anaweza kukaa foleni hata siku nne, akihitaji umuongezee pesa ya matumizi anaambulia matusi!
-tairi ikipasuka unamlipisha! Na mambo mengine ya hovyo hovyo mengi tu kwanini usiibiwe? Kwa nini usiibiwe?