Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Asante kwa maelezo yako. Ni kweli biashara yoyote ni kujitolea muda wako kwa asilimia zote, hasa nchi kama yetu yenye culture ya watu kupenda kusukumwa kama ng'ombe. Kwa upande wa gari ndiyo zaidi kabisa. Bila wewe kuwepo mwenyewe kuwepo lazima utaumizwa.

Ukitaka kujua biashara ya usafirishaji imejaa watu wenye ''ubongo wa kupenda kuiba'' wewe nunua chombo cha usafiri kwa ajili ya biashara halafu ambatana nacho mara kwa mara.

Utachukiwa na dereva na hata watu wa pembeni. Utasikia wanabeza ''tajiri gani habanduki kwenye gari''. Nchi yetu ni nchi pekee watu mfanyakazi anachukia tajiri kusimamia kazi yake.
Wiki hizo nilikuwa nafurahi sana kusafiri na tajiri!

Akiwepo kwenye gari tunakula na kulala hotel, changamoto yoyote inashughulikiwa kwa wakati na muda mwingine alikuwa akinisaidia kuendesha gari!

Kwa kifupi sigusi posho ya safari!
Kwa scenario kama hiyo ningeanzaje kuchukia tajiri kuwepo kwenye gari?

Dereva anaehudumiwa vizuri haibi! Ukiona unaibiwa ujue umeweka mbele ukali/ujeuri usio na maana/na ukorofi wa kipuuzi kuliko kuboresha mazingira ya kazi ya dereva wako..

Kwa tabia hizo utaibiwa, utaibiwa, utaibiwa mpaka uchakae hata kama unalala kwenye cabin!

-Posho unatoa kidogo tena kwa masimango!
-Dereva anaweza kukaa foleni hata siku nne, akihitaji umuongezee pesa ya matumizi anaambulia matusi!

-tairi ikipasuka unamlipisha! Na mambo mengine ya hovyo hovyo mengi tu kwanini usiibiwe? Kwa nini usiibiwe?
 
Kwa pesa ya kwanza nakushauri tafuta 113, 124 na kisha zifanyie matengenezo ya kutosha ndipo uweke barabarani.

Tatizo la R420, R440 zinahitaji uwe na akiba walau isiyo pungua 30millions just for emergency. Pia spare zake ni ghali sana pale SubScania, na hata sisi mafundi tunawachinja sana wamiliki wa R.

Mwisho nikukumbushe tu usisahau kukata bima kubwa yasije yakajutokea kama yule mama.

Pia biashara ya usafirishaji unapo ianza nivyeme ukaisimamia mwenyewe kwa ukamilifu na kila hatua, hii itakusaidia kupata uzowefu wa magonjwa ya magari pia jinsi ya upataji mizigo pasipo kupitia madalali.
Naweza pata wapi mafunzo ya ufundi wa scania?
 
Naweza pata wapi mafunzo ya ufundi wa scania?
Kama ni mtaani naweza nikakupa a,ba,cha,da...
Lakini kama ni chuoni, nakushauri utembelee VETA iliyopo karibu na wewe.

Ingawa ufundi wa hizi chuma unanoga zaidi ikiwa utajifunzia kitaa, na unaanza kuwa alwatan mazima. Pia utapata kujitengenezea wateja polepole(sio wa sisiem), na usije ukatarajia kuajiriwa kwa kwenye hii fani.
 
Hapo ndipo watanzania tunapokosea kama umepata kwenye vanilla kwanini hiyo 100M usiwekeze zaidi kwenye vanilla

Kama ulikuwa na shamba la hekari 10 kwanini usiwe na shamba la hekari 100 hujui kumiliki ardhi na shamba ndio utajiri mkubwa nchini
Nimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha

Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilicho nacho

Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?
View attachment 1484199


Swali la nyongeza 24 June 2020
Vipi biashara ya kusafirisha
Mafuta vs Mizigo
 
Hapo ndipo watanzania tunapokosea kama umepata kwenye vanilla kwanini hiyo 100M usiwekeze zaidi kwenye vanilla

Kama ulikuwa na shamba la hekari 10 kwanini usiwe na shamba la hekari 100 hujui kumiliki ardhi na shamba ndio utajiri mkubwa nchini

Yani wewe ndo unakosea kabisa..,kwanza sidhani kama mleta maada kasema kaacha kulima. Pili, ukwasi mara nyingi unaletwa na chanzo zaidi ya kimoja cha mapato, mkuu wewe hujui kwamba kilimo ni moja kati ya biashara zisizotabirika KABISA???! au haijawahi kulima? hivi unafaham kwamba pamba msimu uliopita ilinunuliwa sh 1200 na mwaka huu mkulima kauza kwa sh 850???!.Bado hujalima wewe😁
 
Yani wewe ndo unakosea kabisa..,kwanza sidhani kama mleta maada kasema kaacha kulima. Pili, ukwasi mara nyingi unaletwa na chanzo zaidi ya kimoja cha mapato, mkuu wewe hujui kwamba kilimo ni moja kati ya biashara zisizotabirika KABISA???! au haijawahi kulima? hivi unafaham kwamba pamba msimu uliopita ilinunuliwa sh 1200 na mwaka huu mkulima kauza kwa sh 850???!.Bado hujalima wewe😁
kama ni hivyo leo cargill wangekuwa wanatengeneza ndege..the issue is kama ni line ya business inatwist but you dont change the industry ndio maana Hp wana laptops, pc na printers different businesses ila the same industry

mie ni muumini wa ku stick kwenye the same industry angekuwa ni mzungu angetoa m30 kwenye research and development ya new method of farming ya vanilla na hapo ndio inakufanya uwe the best katika biashara, ila eti unalima then kesho una duka la hardware kesho kutwa una sijui nini ni mwanzo wa kufilisika .. anaweza kuwa inspired by bakhresa na mo lakini those guys are conglomerate na huwezi kuwa conglomerate lazima the previously business uwe na track ya revenue inayoeleweka. na huajiri consultants wa maana wakitaka ku put their hands in the new field

Naweza kuwa sijawahi lima ila am damn good katika business ... sasa kilimo cha vanilla na transportation company ni industry ipi iko very complicated?
 
Mawazo ya kijinga.Si ajabu wewe ndio biashara unafanya na hutaki wengine wafanye.Hao walioweza wana nini yeye ashindwe.Watz ni kikatishana tamaa tu.
Ukitaka kuanzisha business yoyote halafu ukaomba mawazo kutoka kwa watanzania automatically hiyo biashara hutaianzisha kamwe utaghairi tu endapo utaamua kuchukua ushauri wao 90% watakukatisha tamaa na 10% ndio watakupa moyo uendelee, sijui watanzania tukoje yaani kwani hao wanaoifanya wana nini na kwa nini umkatishe tamaa mwenzako?

Though tunafahamu kila biashara ina changamoto lakini huwezi kuogopa kuingia humo kwa sababu ya changamoto ni lazima uingie ili upambane na hizo changamoto na utakapozishinda ndio mafanikio yanapoanzia. Tusitishane wala kukatishana tamaa wakuu akifanikiwa yeye itakuwa ni fursa pia ya kusaidia wengine na wanaweza wakawa hata ndugu zako pia.
 
Ukitaka kuanzisha business yoyote halafu ukaomba mawazo kutoka kwa watanzania automatically hiyo biashara hutaianzisha kamwe utaghairi tu endapo utaamua kuchukua ushauri wao 90% watakukatisha tamaa na 10% ndio watakupa moyo uendelee, sijui watanzania tukoje yaani kwani hao wanaoifanya wana nini na kwa nini umkatishe tamaa mwenzako? Though tunafahamu kila biashara ina changamoto lakini huwezi kuogopa kuingia humo kwa sababu ya changamoto ni lazima uingie ili upambane na hizo changamoto na utakapozishinda ndio mafanikio yanapoanzia. Tusitishane wala kukatishana tamaa wakuu akifanikiwa yeye itakuwa ni fursa pia ya kusaidia wengine na wanaweza wakawa hata ndugu zako pia.
Marehemu ,mzee Mengi aliwahi kuulizwa kwanini Watanzania hawakui kiuchumi alijibu akasema Watanzania wana tatizo la KUKOSA UTHUBUTU WA KUFANYA JAMBO.
 
Kwa pesa ya kwanza nakushauri tafuta 113, 124 na kisha zifanyie matengenezo ya kutosha ndipo uweke barabarani.

Tatizo la R420, R440 zinahitaji uwe na akiba walau isiyo pungua 30millions just for emergency. Pia spare zake ni ghali sana pale SubScania, na hata sisi mafundi tunawachinja sana wamiliki wa R.

Mwisho nikukumbushe tu usisahau kukata bima kubwa yasije yakakutokea kama yule mama.

Pia biashara ya usafirishaji unapo ianza ni vyema ukaisimamia mwenyewe kwa ukamilifu na kila hatua, hii itakusaidia kupata uzoefu wa magonjwa ya magari pia jinsi ya upataji mizigo pasipo kupitia madalali.
engine mpya za 113 zinapatikana?
 
Mimi naona bora Tamdam ya kutengenezwa hapa hapa nchini. Mtu anunue fuso ya kawaida kisha aibadili.

Kama hataona engine/cabin/chassis vitakuwa vimechoka ni bora akanunue fuso Malawi au Msumbiji kisha aikate ije kama spea kisha abadili kwenye gari aliyonunua.
nasikia malawi magari yanauzwa kwa bei rahisi sana
 
Back
Top Bottom