Nataka kununua Heavy Motor Bike aina ya Kawasaki ila ushauri ninaopata kwa walionizunguka ndio napata uoga

Nataka kununua Heavy Motor Bike aina ya Kawasaki ila ushauri ninaopata kwa walionizunguka ndio napata uoga

Villky_J

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2017
Posts
492
Reaction score
609
Habari zenu wadau....bila shaka ni wazima wa Afya.

Kuna jambo linanitatiza naombeni ushauri wenu. Nilipanga mwaka 2023 angalau ikifika tarehe 01 January niwe na kausafiri kangu (Gari) walau isiyozidi Mil 13.

Sasa kutokana na mambo kutokwenda sawa nimejikuta nina kama Mil 7 mkononi...sasa nikaona wazi wazo langu haliwezi kutoboa, hata nikataka kuchukua kagari mtaani katakuwa ka hovyo [emoji26]

Wazo nikalihamishia kwenye bike off course napenda sana piki piki.

Kwa amount hiyo kwa yule mwanangu wa zanzibar sele mapikipiki napata kawasaki safi kabisa na chenchi kidogo inabaki [emoji16]

Sasa nikasema niulize wadau wawili watatu wanipe maoni yao....kila ninaemshirikisha anasema bro naona umeyachoka maisha [emoji26][emoji24] huna muda tutakuzika achana na hayo mavitu....sasa naona ni bora nisingeulizwa nimeingiwa na hofu kubwa jambo ninaliuliza hata gari unaweza pasta ajali kikubwa ni umakini tu...

Sasa naombeni ushauri wenu nipo so confused [emoji53]
2021-H2-R.jpg

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Watu tunaendesha pikipiki mwaka wa 2 huu. Muhim ni kuwa makini fata sheria za barabarani na practice safe driving wakati mwingine sheria ipo kwako lakin mtu anakuletea mzima mzima so unapunguza mwendo unampisha. Ukitaka ku force tunakupoteza mapema mzee.

Uzuri wa bike huwazi kuhusu foleni. Kigamboni mpaka town nafanyia kazi zangu mikocheni ni dk 35 tu nipo kazini ila nikivuka na gari ni lisaa limoja na nusu.
 
Habari zenu wadau....bila shaka ni wazima wa Afya.

Kuna jambo linanitatiza naombeni ushauri wenu. Nilipanga mwaka 2023 angalau ikifika tarehe 01 January niwe na kausafiri kangu (Gari) walau isiyozidi Mil 13.

Sasa kutokana na mambo kutokwenda sawa nimejikuta nina kama Mil 7 mkononi...sasa nikaona wazi wazo langu haliwezi kutoboa, hata nikataka kuchukua kagari mtaani katakuwa ka hovyo [emoji26]

Wazo nikalihamishia kwenye bike off course napenda sana piki piki.

Kwa amount hiyo kwa yule mwanangu wa zanzibar sele mapikipiki napata kawasaki safi kabisa na chenchi kidogo inabaki [emoji16]

Sasa nikasema niulize wadau wawili watatu wanipe maoni yao....kila ninaemshirikisha anasema bro naona umeyachoka maisha [emoji26][emoji24] huna muda tutakuzika achana na hayo mavitu....sasa naona ni bora nisingeulizwa nimeingiwa na hofu kubwa jambo ninaliuliza hata gari unaweza pasta ajali kikubwa ni umakini tu...

Sasa naombeni ushauri wenu nipo so confused [emoji53]
View attachment 2450153

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
ni piki piki nzuri japo kwenye price sidhani kama uko sahihi maana tuliyokuwa nayo tuliiuza 24m na ilikuwa na 320km phr

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Chukua chuma hiyo achana na hao washamba wa magari
Mm ninayo KTM, hizi bike zina raha yake sana.
Hapo ahida sio hiyo Pikipiki, shida ni huyo sele. Una uhakika yupo Zanzibar? Kuwa makini wengi matapeli sana
KTM unyama mwingi mnoo. Nillipata moja kwa 7m ila mfuko ukagoma ila ni kitambo sana

Pia anaweza tafuta BAJA 250cx/ Honda XLR 250cc sio mbaya
 
Hiyo ml saba unapata ractis safi kabisa ndugu ndugu hapa ninapotype mwili wote na mkono unauma vibaya mno,ni takribani wiki mbili tangu nipige mzinga mmoja matata sana wa piki piki nikaapa mimi na piki piki basi tena jichunguze tabia yako kwanza katika chombo kinahitaji uwe mwanaume na sio mvulana basi ni piki piki na kingine nilichogundua unawez kuwa makini sana lakini akatokea jamaa wa visendo na kiduku cha rasta akakusababishia ajali kwa ujinga wake ,nb kanunue gari
 
Back
Top Bottom