KRISTIAN P
JF-Expert Member
- Feb 16, 2013
- 352
- 57
M
Huko Kigamboni ni msala
Acha kutisha watu tumechukua juzi Kigamboni Lugwadu biashara imeenda poa tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
M
Huko Kigamboni ni msala
😅😅😅comment zingineKwa sababu pamechanika mkuu, ukijenga tu unashonwa
Very wellKwa bajeti ya milioni 20 sqm 800 utapata kiwanja kizuri tu na eneo karibu, katika mengi mengi ya kuzingatia pia usisahau yafuatayo
- Usiwe na haraka kumbuka nyumba ni kitu cha kudumu hivyo jipe muda viwanja vipo vingi, heri uchelewe lakini upate eneo lisilo na shida.
- Usikubali kulipa 100% lipa kwa installments hata kama zitakuwa chache hii itapunguza chances za full kutapelewa.
- Hakikisha umefanya utafiti kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Utafiti namaanisha kwa kuhoji majirani, mjumbe wa eneo (jua jina lake kwanza kabla ya kumwendea, jua na anapoishi, hii ni kuepuka kupata mjumbe feki.
- Kwa kuwa umesema unafanyia kazi nyumbani na kama unahitaji internet jiridhishe kuwa internet kwa eneo unalotaka kununua ina signals strenght ya kutosha.
- Angalia ukubwa wa barabara ulizopakana nazo je zina ukubwa wa kutosha maana kuna viwanja unauziwa barabara ina mita 3 hii ina maana kiwanja chako mwisho wa siku kitamegwa kupisha barabara za mitaa/mtaa so kiwanja kitapungua ukubwa.
- Hakikisha kiwanja kinafikika tena bila shida majira yote iwe jua iwe mvua iwe mafuriko. Epuka kununua kiwanja uelekeo ambao inabidi uvuke mto au mfereji na wakati kwenye huo mto au mfereji hakuna daraja lililojengwa. Hata kama mfereji/mto utakuwa mdogo vipi acha kununua hicho kiwanja maana siku mvua kubwa ikinyesha hakika utakuwa kisiwani.
- Hakikisha unajua unataka kiwanja maeneo gani yaliyo flat kama kigambon au yaliyo na milima milima kama kimara. Hii unaweza ukaona haina maana lakini ukipata kiwanja ambacho hakipo flat ujue itakuwa ikinyesha mvua kigogo tu inabidi urudishie mchanga uliosombwa na maji na vilevile kabla ya kujenga mara nyingi itakubidi ufanye kupasawazisha au ujenge kufuata bonde/mwinuko hii inaongeza gharama za ujenzi.Vilevile angalia kiwanja hakifanya maji kutuama maana unaweza kununua sehemu wakati wa kiangazi ikija masika maji ya mtaa yanajihadhi kwenye kiwanja chako! ila wakati wa kiangazi ahh pako safi.
- Ni vizuri kiwanja kisiwe mbali sana na barabara ya lami maana kama kipo mbali sana na lami na kwa mfano una gari ina maana gharama za matengenezo na mafuta zitaongezeka maana wakati wa masika daily unakanyaga madimbwi wakati wa kiangazi daily unakanyaga mashimo.
- Jua status yako maana kama unajiona una hadhi fulani basi itakubidi utafute maeneo yahadhi yako ambayo hata majirani zako na mijengo yao liyo mingi itakuwa ni ya hadhi fulani. Hii itaepusha kujisikis vibaya pindi ushajenga halaf unaona noma hata kuwapeleka ndugu marafiki zako maana majirani zako wengi wana hadhi fulani ambazo wewe huzipendi.
- Fanya utafiti kujua kama kiwanja hakina mgogoro kwa maana ya muuzaji na wanaomhusu na wasiomhusu i.e. majirani, ndugu, watoto, serikali.
- Epuka kununua kiwanja mahali mbapo kwa siku za usoni au hata siku za mbele sana serikali ina mipango ya kutumia hiyo ardhi, maana siku serikali ikiamka ikachukua hiyo ardhi utakuta umepoteza pesa, na muda wako.
- Kabla ya kunua angalia huduma za kijamii ambazo wewe ungependa ziwe karibu na wewe je zipo?
- Mtangulize Mungu, muombe sana asikuache ukanunua kiwanja ambacho kina shida za kiroho. Amini usiamini kuna watu maisha yao yamepata shida maana walinunua viwanja ambavyo vina shida katika ulimwengu wa roho.
Naunga mkono hili ...Morogoro road sio ya kuichukulia pouwa kabisa ...tukumbuke tayar serikali ina mpango wa kutanua Barabara thamani ya maeneo ya hii njia itaongezeka kwa kasiWajanja wanaunua viwanja along morogoro road kibaha hadi chalinze hii ni promising area.
#MaendeleoHayanaChama
Goba bei ghali sana mkuu, milioni 35 kiwanja cha sqm 1000, tena kipo ndanindani
May I get that number, please.Nna dalali ambae ndio alienitafutia Mimi kiwanja maeneo ya mapinga, ukiwa tayari ntakuunganisha nae kaka,,kule kuzuri ,upate tu mtu muhaminifu
Kwa hiyo wewe sio mswahili? Kila mtu anunue anapo afford halafu ni wajibu wa mamlaka kuhakikisha mitaa inapangwa vizuri. Nenda mikoani kuna nyumba za tembe lakini zipo kimitaa zimejipangaIle Chanika ni Manzese ya baadaye mkuu
Kule sio pa kununua kiwanja patakuja kuwa uswahilini hatari. Ujenzi holela kama ule kwenye ardhi iliyo tambarare mwisho wa siku mitaro ya maji machafu itazagaa kama Vingunguti.
Na ndio maana viwanja vina bei nafuu sana Chanika kwa sababu vinauzwa na waswahili.
Sawa bro lakini mwerevu huuona msiba na kujifichaKwa hiyo wewe sio mswahili? Kila mtu anunue anapo afford halafu ni wajibu wa mamlaka kuhakikisha mitaa inapangwa vizuri. Nenda mikoani kuna nyumba za tembe lakini zipo kimitaa zimejipanga
Bro nahitaji namba ya dalali wa mapinga kama bado unayoNna dalali ambae ndio alienitafutia Mimi kiwanja maeneo ya mapinga, ukiwa tayari ntakuunganisha nae kaka,,kule kuzuri ,upate tu mtu muhaminifu
Bado ipo?Shekh fanya nikakupe plot yangu ya acre 1,chanika-kitanga 7.5M kama zawadi ya Ramadhani.
Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app