Kwa bajeti ya milioni 20 sqm 800 utapata kiwanja kizuri tu na eneo karibu, katika mengi mengi ya kuzingatia pia usisahau yafuatayo
- Usiwe na haraka kumbuka nyumba ni kitu cha kudumu hivyo jipe muda viwanja vipo vingi, heri uchelewe lakini upate eneo lisilo na shida.
- Usikubali kulipa 100% lipa kwa installments hata kama zitakuwa chache hii itapunguza chances za full kutapelewa.
- Hakikisha umefanya utafiti kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Utafiti namaanisha kwa kuhoji majirani, mjumbe wa eneo (jua jina lake kwanza kabla ya kumwendea, jua na anapoishi, hii ni kuepuka kupata mjumbe feki.
- Kwa kuwa umesema unafanyia kazi nyumbani na kama unahitaji internet jiridhishe kuwa internet kwa eneo unalotaka kununua ina signals strenght ya kutosha.
- Angalia ukubwa wa barabara ulizopakana nazo je zina ukubwa wa kutosha maana kuna viwanja unauziwa barabara ina mita 3 hii ina maana kiwanja chako mwisho wa siku kitamegwa kupisha barabara za mitaa/mtaa so kiwanja kitapungua ukubwa.
- Hakikisha kiwanja kinafikika tena bila shida majira yote iwe jua iwe mvua iwe mafuriko. Epuka kununua kiwanja uelekeo ambao inabidi uvuke mto au mfereji na wakati kwenye huo mto au mfereji hakuna daraja lililojengwa. Hata kama mfereji/mto utakuwa mdogo vipi acha kununua hicho kiwanja maana siku mvua kubwa ikinyesha hakika utakuwa kisiwani.
- Hakikisha unajua unataka kiwanja maeneo gani yaliyo flat kama kigambon au yaliyo na milima milima kama kimara. Hii unaweza ukaona haina maana lakini ukipata kiwanja ambacho hakipo flat ujue itakuwa ikinyesha mvua kigogo tu inabidi urudishie mchanga uliosombwa na maji na vilevile kabla ya kujenga mara nyingi itakubidi ufanye kupasawazisha au ujenge kufuata bonde/mwinuko hii inaongeza gharama za ujenzi.Vilevile angalia kiwanja hakifanya maji kutuama maana unaweza kununua sehemu wakati wa kiangazi ikija masika maji ya mtaa yanajihadhi kwenye kiwanja chako! ila wakati wa kiangazi ahh pako safi.
- Ni vizuri kiwanja kisiwe mbali sana na barabara ya lami maana kama kipo mbali sana na lami na kwa mfano una gari ina maana gharama za matengenezo na mafuta zitaongezeka maana wakati wa masika daily unakanyaga madimbwi wakati wa kiangazi daily unakanyaga mashimo.
- Jua status yako maana kama unajiona una hadhi fulani basi itakubidi utafute maeneo yahadhi yako ambayo hata majirani zako na mijengo yao liyo mingi itakuwa ni ya hadhi fulani. Hii itaepusha kujisikis vibaya pindi ushajenga halaf unaona noma hata kuwapeleka ndugu marafiki zako maana majirani zako wengi wana hadhi fulani ambazo wewe huzipendi.
- Fanya utafiti kujua kama kiwanja hakina mgogoro kwa maana ya muuzaji na wanaomhusu na wasiomhusu i.e. majirani, ndugu, watoto, serikali.
- Epuka kununua kiwanja mahali mbapo kwa siku za usoni au hata siku za mbele sana serikali ina mipango ya kutumia hiyo ardhi, maana siku serikali ikiamka ikachukua hiyo ardhi utakuta umepoteza pesa, na muda wako.
- Kabla ya kunua angalia huduma za kijamii ambazo wewe ungependa ziwe karibu na wewe je zipo?
- Mtangulize Mungu, muombe sana asikuache ukanunua kiwanja ambacho kina shida za kiroho. Amini usiamini kuna watu maisha yao yamepata shida maana walinunua viwanja ambavyo vina shida katika ulimwengu wa roho.