Nataka kununua NISSAN EXTRAILL

Nataka kununua NISSAN EXTRAILL

HAMNA GARI HAPO NA SPAIR ZAKE GHARAMA NA PIA NNGEKUSHAULI TAFUTA TI AU IST KWAKO ITAKUFAA
 
Mwalimu??!?!!....nyie nyie wenye stress za mishahara mpaka mnataka kuua watoto wa watu kwa vipondo[emoji86] [emoji86] ...unataka miliki X trail, hongera asee!



(Joke)
 
Itamtesa na kitu gani? Mweleze ajue...mafuta vipuri au nn?
HAIFAI TU
NISSAN anakula mafuta, spea zake bei ghali, si imara kulinganisha na TOYOTA
kwa level ya SUV anunue RAV4, Harrier au Kluger hatajuta
lakini km anapewa kwa bei ndogo achukue lakini ajue hatamuuzia mtu hicho ni kimeo mwenzake kakishtukia.
 
HAIFAI TU
NISSAN anakula mafuta, spea zake bei ghali, si imara kulinganisha na TOYOTA
kwa level ya SUV anunue RAV4, Harrier au Kluger hatajuta
lakini km anapewa kwa bei ndogo achukue lakini ajue hatamuuzia mtu hicho ni kimeo mwenzake kakishtukia.
Nimetumia Rav4 kilitime na xtrail rav 4 inakula zaidi ya xtrail...xtrail ni ngumu kuliko rav 4..offcourse ni ngumu kuuza pia nissan ila yangu nimeuza karibuni..lakini huo ni ushauri tu anaweza kuupima kisha aamue.
 
Du huwezi pata ushauri mzuri humu Kila mtu anajua kwelikweli.
 
Ni gari nzuri sana, fuel economy, gari ya juu, ina nafasi kubwa ndani. Ila ina sensors nyingi hivyo unatakiwa kuwa makini hizo sensors. Kama ikitokea kuna mlio ambao sio wa kawaida nenda kwa fundi coz mara nyingi huwa ni sensore tu ndio zinazingua ila mafundi wa kibongo hawawezi unakuta wanafungua mpaka engine wakati tatizo lilikuwa ni sensor ya kubadilisha na kuweka mpya. Ni gari ambayo sio kila fundi anaweza kuitengeneza coz inatumia teknolojia ya juu sana. Ina sehemu nyingi za umeme. Mm nina fundi wangu mmoja ambaye yy huwa anatengeneza sana magari ya umeme. Ni fundi mzuri sana na ndiye aliyenishauri niinunue. X-trail ni gari nzuri sana kiongozi.
 
Ukitaka kununua gari angalia mahitaji yako na budget yako. Wapo wanaokushauri usinunue wakati wao hawajawahi kuimiliki na hapo hapo watakushauri ununue wanachokipenda wao. Kiufupi ni gari nzuri sana kuliko Toyota kwenye aspect nyingi. Stability, consumption, space, confort etc.

Ukiona inakula mafuta vitu viwili plug ama air throttle sensor. Badilisha inarudi kama imetoka japan ukiona haimalizi speed badili fuel pump.

Huu mwaka wa tano inatembea nchi nzima

u
 
Mim nataka Toyota raumi jamanii hapo VIP?? Nipen ushauri
 
Niliwahi kufuatilia hizi mada za Xtrail, mwaka jana wakati nataka kununua gari, nikataka kukata tamaa na Nissan...lakini baada ya kidadisi kwa seasoned owners na mmoja alikuwa anasafiri nje ya nchi akaniachia miezi mitatu, nikaishia kununua ya kwangu kabisa. Mpaka leo mwaka mmoja sijutii uamuzi wangu, ingawa mwaka mmoja ni mfupi lakini nimegundua wapondaji wengi humu ndani wanasumbuliwa na cognitive bias ya "halo effect"
 
xtrail haina tatizo , tatizo ni mafundi wetu wa mtaani kila kitu wanataka kutumia nyundo, hio ni very smart car, kama ni hivo nissan wasingeendelea kuzitengeneza, but ukiwa unaenda gereji smart , hio gari utaitumia mpaka vitukuu
for more information kama wataka kuagiza, contact/whatssap 0674518707

Japanese Used Cars Stock List | Autocom Japan
 
kwa nini unaniambia hivyo mkuu??
kama wewe ni mwalimu na kamshahara ka kairuki X- trail itakutesa kwa spare part, jaribu kwenda Kariakoo ulizia bei ya power window ya nissan na Noah na baada ya hapo utakuja na jibu
 
Back
Top Bottom