Nataka kununua wifi router ya kusambaza intaneti nyumbani lakini itakaa masaa 6 tu. Je, nikiiwekea power bank itakuwa inakaa muda gani?

Nataka kununua wifi router ya kusambaza intaneti nyumbani lakini itakaa masaa 6 tu. Je, nikiiwekea power bank itakuwa inakaa muda gani?

Mi natumia ya kuconnect kwenye power moja kwa moja inapiga mzigo 24/7.
kama yangu nina HUAWEI hilo lenyewe kwanza ni powerbank pia
yaani hiyo ROUTER naweza tumia kama powerbank
unasahau hata siku 2 kama lina chaji fully mana battery lake ni 6600mah
20220804_231141.jpg
20220804_231201.jpg

nunua kama hii mkuu tena sasa hivi newversion zipo mpk 10000mah
 
ndicho nilichoandika kwenye post kuu hiki...

sasa je hii haina madhara ? power bank itaweza kuipa moto hio wifi router kwa muda gani ?
Hapana mkuu. Router na dongle ni tofauti. Hiyo router uliyoweka pichani ina battery yake. So unapotumia powerbank ni kwamba unacharge hiyo battery.

Unless kama unaweza connect kwenye powerbank ikafanya kazi bila battery. Ila kama utaitumia na battery, madhara ni kwamba battery yake itaishiwa nguvu mapema, maana unaicharge muda wote.

USB Dongle haina battery. Inahitaji tu powersource kufanya kazi. So haina madhara yoyote kuitumia kwenye powerbank. Na itakaa muda mrefu sababu haicharge. Inatumia moto kidogo.
 
Alternative tafuta repeater, signal booster funga hapo network ilipo italeta ndani, sema bei zake zimechangamka.
 
Nunua solar panel za kichina inakuja na kilakitu ndani hadi usb ya kuchaj hiyo wifi yako na redio na torch hiyo utaconnect direct hiyo mifi yako usiku inatumia battery ya sola mchana inachajiwa hapo utakuwa umekata mzizi wa fitina hizi zinauzwa elf 40
 
Hii solar inaweza hudumia laptop 2 na TV?
 
Back
Top Bottom