Nataka kurudiana na X wangu baada ya miaka minane. Ushauri

Nataka kurudiana na X wangu baada ya miaka minane. Ushauri

Habari za wakati huu wadau?

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza. Ninataka kurudiana na mwenzangu ambae tulitengana miaka minane iliyopita, naombeni maoni ushauri namna ya kuishi nae maana huko alikokuwa atakuwa kajazwa sumu nyingi sana.

Karibuni.
Sababu za kuachana ni nini?
If he /she cheated on you never go back…..
 
Ungeweza kueleza sababu ya kuachana ungepata ushauri mujarabu mkuu
 
Mwanzoni tulitengana kwa sababu niliachishwa kazi,nikakaa home kama mwezi,mambo yalivyokuwa magumu zaidi nikatafuta hela nikamwambia arudi nyumbani kwanza niendelee kupambana,mambo yakishakuwa sawa atarudi tena town,nikamwachia nauli ya kumfikisha nyumbani kwa wazazi wangu,baadae jioni nampigia simu nijuwe amefika wapi,hakuwa anapatikana,nikawapigia simu nyumbani kama amefika huko,wakasema hajafika,basi kesho yake ndiyo akaniandikia sms kwamba asingeweza kwenda nyumbani kumbe ile hela niliyompa alienda kupanga chumba mahali akakaa hapo.

Samahani bro, niruhusu nikutukane, wewe ni limbukeni na mtu dhaifu sana hata kuwaza tu kumrudia!
 
NAmuonea huruma maana yeye ananipenda kuliko mimi navyompenda.
Muache mtoto wa watu nikajua una lolote kumbe hamna kitu, huruma ya nini miaka nane yote hiyo kama kuna mwenye mapenzi ya kweli kati yenu angekuwa anaokota makopo kila mtu abakie aliko.
 
Mwanzoni tulitengana kwa sababu niliachishwa kazi,nikakaa home kama mwezi,mambo yalivyokuwa magumu zaidi nikatafuta hela nikamwambia arudi nyumbani kwanza niendelee kupambana,mambo yakishakuwa sawa atarudi tena town,nikamwachia nauli ya kumfikisha nyumbani kwa wazazi wangu,baadae jioni nampigia simu nijuwe amefika wapi,hakuwa anapatikana,nikawapigia simu nyumbani kama amefika huko,wakasema hajafika,basi kesho yake ndiyo akaniandikia sms kwamba asingeweza kwenda nyumbani kumbe ile hela niliyompa alienda kupanga chumba mahali akakaa hapo.
Sio kupanga chumba mkuu wewe c ndio ulimpa mtaji wa milioni mbili aende kununua mazao kumbe kapotea akaenda kuolewa huko
 
Back
Top Bottom