Nataka kutengeneza milioni 100tsh!

Nataka kutengeneza milioni 100tsh!

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,074
Ndoto yangu ni kutengeneza usd 50,000$ ndani ya miezi sita!inaweza kuwa ni ngumu lakini inawezekana kabisa kama ukitumia Juhudi,nguvu na maarifa ya kibabe zaidi!
Ni ukweli usiopingika kwa maisha ya kibongo bongo ukipata milioni 120 unaweza ukapunguza kabisa ukali wa umaskini,mfano hapo unaweza ukawa na nyumba ya milioni 30,gari ndogo tu yakufanyia shughuli zako milioni 15,na ukabaki na milioni 85 za kuendesha biashara zako!
Sasa hapo napiga mahesabu ni kitu gani utawauzia watu 5000 ambacho utapata faida ya dola 10 kwa kila kichwa!!!!?
Ama ni huduma gani unaweza ukafanyia watu 5000 kila mmoja akakupatia kiasi cha 10usd!!?
Idadi ya watanzania ni takribani milioni 50+
Lkn watu 5000 tu wanaweza kubadilisha maisha yetu Mimi na wewe!
Watu 5000 ni sawa na kupata watu 200 kila mkoa
 
Nilitaka kusema ni kiduku lilo amekuja na ID nyingine, lakini sentensi za mwisho zimenifungua unachofikiri.

Ngoja wajuzi zaidi waje.
Kila kitu kinawezekana.
[emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
 
impossible,unaongelea faida ya dola kumi ambayo ni sawa na karibu elfu 25,

itahitaji mtaji mkubwa mno ili uweze kuzalisha hiyo faida kwa watu 5000 tu,

fanya watu elfu 20,
faida iwe tsh 5000,
 
mfano tu,umenunua madela 20,000,

kwa bei ya kununulia tsh 10,000=

utatumia milioni 200,

utauza kwa 15000 kwa watu elfu 20,

utapata faida ya milion 100,

hapa yataka atleas utafute kitu utakachonunua kwa wholesale price ya tsh 5000 na uje kuuza kwa tsh 10,000,
 
Kumbuka mtoa mada ameweka limit ya miezi sita (6)

Sio lazima atengezene hiyo 100M kwa mkupuo mmoja, anaweza kuwa ma mtaji mdogo akazungusha kwa juhudi kubwa bila kukata tamaa, within six month alizojiwekea kama deadline akawa amefanikisha lengo.
 
Fanya hizi biashara utatoka chap..
Uza dawa za kulevya.
Uza mali asili kama pembe za ndovu.
Uza binadamu.
Uza vipodozi vyenye mercury.
Lete mrejesho baada ya huo muda, utaikopesha tz.
Biashara halali utachukua mda mrefu, huo hautoshi.

Nb: Unatakiwa uwe na connection za maana SANA.
 
Mawazo Chanya Sana.

Ila Kabla Ya Kuanza Moja Kwa Moja Na $50k Inabidi Uweze Kutengeneza $10k Baada Ya Hapo Ndio Utaweza Kuipata Hiyo Uliyokusudia.

Pia Kabla Ya Kupata $10k Inabidi Utengeneze Mazingira Ya Kupata $5k.

Tena Kabla Ya Kupata $5k Inabidi Uwe Tayari Una msingi Wa Kutengeneza $2k

Sasa Hapo Hatujazungumzia Umelenga Kwa Watu Wangapi Kwenye Kila Hatua.

Kila Kitu Kinawezekana Chini Ya Jua
 
Sana kaka but ungesema una kianzio cha Tsh ngapi na wewe una experience na kitu gani
 
impossible,unaongelea faida ya dola kumi ambayo ni sawa na karibu elfu 25,

itahitaji mtaji mkubwa mno ili uweze kuzalisha hiyo faida kwa watu 5000 tu,

fanya watu elfu 20,
faida iwe tsh 5000,
Ni biashara ya vifaa vya ujenzi/mbao au spares za magari ndio zina faida Kama hizo na mtaji wake uwe na angalau milioni 50 na sio maneno matupu.
 
Penye nia pana njia, all the best, hapa nilipo kenge nawaza fuata msafara wa mamba hata nimake Tsh1m hapa gengeni kwangu
Tchao, Muuza Nyanya, Kijijini Doma
 
Ndoto yangu ni kutengeneza usd 50,000$ ndani ya miezi sita!inaweza kuwa ni ngumu lakini inawezekana kabisa kama ukitumia Juhudi,nguvu na maarifa ya kibabe zaidi!
Ni ukweli usiopingika kwa maisha ya kibongo bongo ukipata milioni 120 unaweza ukapunguza kabisa ukali wa umaskini,mfano hapo unaweza ukawa na nyumba ya milioni 30,gari ndogo tu yakufanyia shughuli zako milioni 15,na ukabaki na milioni 85 za kuendesha biashara zako!
Sasa hapo napiga mahesabu ni kitu gani utawauzia watu 5000 ambacho utapata faida ya dola 10 kwa kila kichwa!!!!?
Ama ni huduma gani unaweza ukafanyia watu 5000 kila mmoja akakupatia kiasi cha 10usd!!?
Idadi ya watanzania ni takribani milioni 50+
Lkn watu 5000 tu wanaweza kubadilisha maisha yetu Mimi na wewe!
Watu 5000 ni sawa na kupata watu 200 kila mkoa
Issue kama hizi zinawezekana... Inataka mpango, ufuatiliaji, maono, kutokata tamaa, ubunifu wa mara mara na kutengeneza msingi.

Kujipa muda mfupi, ni kutengeneza au kujiandaa kushindwa ... Kinachosimama na kutoa mafanikio makubwa , hakijengwi kwa muda mfupi.. Kwa vile utahitaji watu, kuanza njia fulani na kuacha ,, Kuanguka mahali fulani, kuinuka na kuanza upyaa.

Lakini kuweka miezi michache ni kutaka kuingia kwenye biashara za kubahatisha, ambazo huleta kulia na kusaga meno..

Ati umeona mtu ameleta viazi, vitunguu Kariakoo,kahesabiwa mamilioni, mwingine anaingia kichwa kichwa , haiendi hivyo utapasua engine, mashine ya boxer haiwezi kuendesha Prado..
 
Ingia serikalini kapige rushwa.
Hio pesa ni fasta sana serikalini ukiwa mla rushwa.
Jiulize incharge wa kodi bandarini anashindwa kulaza 1m kwa siku from rushwa??
 
impossible,unaongelea faida ya dola kumi ambayo ni sawa na karibu elfu 25,

itahitaji mtaji mkubwa mno ili uweze kuzalisha hiyo faida kwa watu 5000 tu,

fanya watu elfu 20,
faida iwe tsh 5000,
Mkuu nimelenga hasa kwenye mtaji wa 5000usd,ni nunue kitu kwa 1usd kila item na Mimi niuze 3usd,then nafanya hivyo hivyo kwa speed ya miezi sita hadi nitimize malengo
 
Back
Top Bottom