Nataka kutengeneza milioni 100tsh!

Nataka kutengeneza milioni 100tsh!

impossible,unaongelea faida ya dola kumi ambayo ni sawa na karibu elfu 25,

itahitaji mtaji mkubwa mno ili uweze kuzalisha hiyo faida kwa watu 5000 tu,

fanya watu elfu 20,
faida iwe tsh 5000,
Yaani kwa hesabu za haraka haraka,

kwa watu 5000, faida ya elfu 25, kama profit margin yako ni 30%, ina maana hapo kila bidhaa moja ni kama 83 elf hiv, ambapo kwa za kutosha watu 5000, mtaji wake ni Ml 400 hiv
 
Nilipata random thoughts mwaka jana June 2018 hakika nilitesa akili yangu sana kutafuta ways out nakuwaza wateja intervals mwisho nikawaza kutengeneza product ambayo wateja watainunua ambayo itakuwa repeatedly bila kunilazimu kukuza eneo la biashara mfano wilaya mkoa ama ukanda.

Ni mwanzo mzuri nashauri andika kwenye kitabu kisha ulifanyie kazi kwa miezi kadhaa binafsi sijafanikisha bado ila nina vitu nilivyovifanyia kazi naamini muda ukifika nitafanikisha kwa kiwango fulani.

Ukipata jibu lifanyie kazi upesi kwani unapohisi wazo ni lako na ni jipya kuna watu zaid ya 500 duniani wanaweza kuwa na wazo kama lako na kulifanyia kazi hivyo ukichelewa wewe ndio unakuja kuonekana umekopi
Ndoto yangu ni kutengeneza usd 50,000$ ndani ya miezi sita!inaweza kuwa ni ngumu lakini inawezekana kabisa kama ukitumia Juhudi,nguvu na maarifa ya kibabe zaidi!
Ni ukweli usiopingika kwa maisha ya kibongo bongo ukipata milioni 120 unaweza ukapunguza kabisa ukali wa umaskini,mfano hapo unaweza ukawa na nyumba ya milioni 30,gari ndogo tu yakufanyia shughuli zako milioni 15,na ukabaki na milioni 85 za kuendesha biashara zako!
Sasa hapo napiga mahesabu ni kitu gani utawauzia watu 5000 ambacho utapata faida ya dola 10 kwa kila kichwa!!!!?
Ama ni huduma gani unaweza ukafanyia watu 5000 kila mmoja akakupatia kiasi cha 10usd!!?
Idadi ya watanzania ni takribani milioni 50+
Lkn watu 5000 tu wanaweza kubadilisha maisha yetu Mimi na wewe!
Watu 5000 ni sawa na kupata watu 200 kila mkoa
 
Fanya hizi biashara utatoka chap..
Uza dawa za kulevya.
Uza mali asili kama pembe za ndovu.
Uza binadamu.
Uza vipodozi vyenye mercury.
Lete mrejesho baada ya huo muda, utaikopesha tz.
Biashara halali utachukua mda mrefu, huo hautoshi.

Nb: Unatakiwa uwe na connection za maana SANA.
Haha ngoja nianze kuuza vipodozi sasa
 
Dah! Kwanini kila nalowaza nalikuta humu jf? Lakini angalao tumetofautiana kwenye swala la muda, wakati wew unafikiria kutengeneza mil. 100 ndani ya miezi 6, mimi mawazo yangu ni kutengeneza mil. 100 ndani ya miaka 5. All in all yote ni malengo.
 
Sawa mkuu
Nilipata random thoughts mwaka jana June 2018 hakika nilitesa akili yangu sana kutafuta ways out nakuwaza wateja intervals mwisho nikawaza kutengeneza product ambayo wateja watainunua ambayo itakuwa repeatedly bila kunilazimu kukuza eneo la biashara mfano wilaya mkoa ama ukanda.

Ni mwanzo mzuri nashauri andika kwenye kitabu kisha ulifanyie kazi kwa miezi kadhaa binafsi sijafanikisha bado ila nina vitu nilivyovifanyia kazi naamini muda ukifika nitafanikisha kwa kiwango fulani.

Ukipata jibu lifanyie kazi upesi kwani unapohisi wazo ni lako na ni jipya kuna watu zaid ya 500 duniani wanaweza kuwa na wazo kama lako na kulifanyia kazi hivyo ukichelewa wewe ndio unakuja kuonekana umekopi
 
Tuko tofauti sana wakati wewe ukiwaza kupata 100M in your bank account Kuna wengine goals zao nikupata 100k Twitter followers,100k instagram followers,100k whatsap status viewers.
 
Kama unamtaji namipango mizuri hiyo pesa unaipata tena bila kutokwa jasho angalia nibiashara gani ambayo ukiiweka mtaan kila mmoja ataipenda mf ano unaweza kufanya biashara yamazao kukusanya kutoka vijijin nakupeleka mojakwamoja inchi zajiran naamini utapata hiyo hela hata kabla yamiez 6kwakuwa biashara yamazao haimuweki mtu
 
Unaonekana hujui kabisa kitu kinachoitwa biashara, endelea tu kuwa Mwalimu wa shule ya msingi hapo hapo
kwa bongo hii, hakuna biashara ya hivyo, mtaji milioni 10, kwa mwezi ukijitaidi sana labda faida milioni 1
 
Mkuu usilete makuzi na Biashara kilamtu angekuwa millionaire kwa ratio izo.
Sileti makuzi angalia nyuzi zangu utaelewa ndugu,
NInachokiongea ndhicho ninakimaanisha, Mtaji wa mil 5 unafunga hesabu Elfu 80 hadi laki per day
nilichokiongea nina uhakika nacho
 
Kama ukishindwa kutengeneza faida ya milioni 1 kwa mwezi kwa mtaji wa milioni 3 inabidi kupimwa mkojo!mkuu huyo sio mfanyabiashara
Acha utani mtaji wa 10M mwezi upate 1M itakuwa ujachanga vizuri karata.
 
Mkuu kama upo serious na hela unayo mkononi now

Biashara ya kununua mahindi vijijini kwenye mikoa ya Mbeya, ruvuma, rukwa, Njombe then unauza kwenye mikoa yenye ukame lazma utapata hiyo hela Chini ya miezi sita

Mf rukwa debe la mahindi ni 5k_6k kwa gunia la debe 10= 50k

Ukisafirisha mpaka mikoa ya kanda ya ziwa au nje ya nchi haipungui 120k kwa gunia la debe 10
Uko sahihi sana mkuu. Very bright idea akiifanya hii akiwa na capital ya 5000usd atafikia lengo lake.
 
Back
Top Bottom