SoC02 Nataka kuwa mtu wa maarifa ndani ya Jamii

SoC02 Nataka kuwa mtu wa maarifa ndani ya Jamii

Stories of Change - 2022 Competition

Kikapuu

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
1,122
Reaction score
1,629
Utangulizi.

Maarifa ni elimu ambayo mtu huitaji ili aweze kuitumia katika maisha yake au kusaidia wengine kwa changamoto ambazo hawawezi kuzitatua kutokana na ufinyu wa maarifa. Maarifa unaweza kuyapata kwa kutumia elimu rasmi hiisiyo rasmi mfano mtaani. Tukiongelea neno mtu wa maarifa ni yule mwenye hulka ya kupenda kujifunza mambo mbalimbali kupitia njia tofauti tofauti katika maisha yake. Mtu wa aina hii ni muhimu katika jamii kwani huleta mapinduzi makubwa ndani ya jamii kwa sababu ya kuwa na hulka kujifunza vitu mbalimbali ndani ya jamii. Hivyo, hata wewe unaweza kuwa mtu muhimu iwe unajua kusoma au hujui, yote yanaezejana.

images (10).jpeg

(Picha kutoka mtandaoni)

Kimsingi kuwa na maarifa fulani hukatazwi zaidi ya wewe kuamua kuyatafuta au kutotafuta, utafutaji wa maarifa hauchagui umri na ndio maana tunajifunza na kurudia matendo mbalimbali kila siku mfano kupika, kulima au kufundisha. Nadhani ushakutana na baadhi ya watu hajui kusoma wala kuandika ila anafahamu ujuzi fulani mfano kutengeneza au kurekebisha pikipiki. Mtu wa aina hii alijijengea tabia ya kujifunza. Hakuna linaloshindikana ukiamua kufahamu kitu fulani basi tafuta nakala zake na jifunze. Uthubutu, uvumilivu, kutokuwa na wivu, imani, hekima na busara ni muhimu vitu hivi anaweza kukosa mtu mzima ila akawa navyo mtoto mdogo. Hivyo, usisahau kumuomba muumba wako akupatie na kukuimarishia vitu hivi kwani ni muhimu sana katika maisha yako. Elimu sio hadi uwe shuleni hata hapo ulipo unaweza kujifunza mambo mbalimbali na ukaelewa vizuri zaidi na kumzidi hata aliyepo darasani.
Je, unapenda kufahamu masuala ya afya, uchumi, ufundi, michezo au sanaa ?
Basi wakati wako ni sasa na sio baadae au siwezi, unaweza sasa.

Nawezaje kuwa mtu wa maarifa ?
Kama nilivyosema unaweza kuyapata kwa kutumia elimu rasmi au isiyo rasmi. Basi nitakuonesha namna tofauti tofauti za kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali na kuyatumia ndani ya jamii zetu. Kabla ya yote muuombe muumba akupe uvumilivu na kukupa au kukuongezea imani ya kujifunza zaidi, maana hata kwenye maandiko wanasema watu wangu wanaa gamia kwa kukosa maarifa au elimu haina mwisho. Hivyo, anza kujenga tabia ya kujifunza vitu vipya kila siku.
Njia hizo ni :

Kwa kusoma vitabu, upatikanaji wa vitabu ni rahisi unaweza kuvisoma kwa njia ya mtandao au kwenda maktaba. Katika mtandao kuna rasilimali nyingi sana kama unajua kuutumia na Kama hujui omba msaada kwa mtu anayeelewa ili akuelejeze namna ya kutafuta rasilimali zilizomo mtandaoni na ipi inaendana na wakati. Kwa upande wa maktaba unaweza kupata ushauri kwa wakutubi (wasimamizi wa maktaba). Pia, unaweza kujiunga na chuo chochote cha ufundi mfano VETA. Na kama unakipato kizuri ni vizuri ukanunua ili uwe huru zaidi kukisoma mda wowote.
images (8).jpeg

(Picha kutoka mtandaoni)

Kwa kushiriki katika jamii, kiuhalisia binadamu tunategemeana hata uwe na vitu kiasi gani bado msaada kwa wenzako ni muhimu. Unaweza ongeza au kuimarisha maarifa yako ndani ya wanajamii kwa kutoa mawazo na kutatua changamoto zao. Heshimu kila mtu iwe mdogo kwa mkubwa na penda kusikiliza mawazo yao kabla ya kupewa nafasi au kutoa mawazo yako. Penda kujenga tabia ya kujaribu, na Kama kitu hufahamu sena hiki sijui labda nielekeze au hadi nikakifatilie vizuri. Kupitia hivi utajijengea tabia ya kuwa mtatuzi wa changamoto kuanzia ndani ya familia hadi kwenye jamii.

Kwa kuishi kiuhalisia na kuwa na marafiki wa faida, ukiishi kiuhalisia basi hata marafiki utapata wa kuendana na wewe na utakuwa huru zaidi. Marafiki wa faida watakuwa wanakupa ushauri na njia mbalimbali katika maisha ya utafutaji. Zingatia hili marafiki wa faida wanaweza kuwa wale wenye mtazamo chanya unaokubalika na jamii na wale usiokubalika na jamii. Kwa mfano unaweza kuwa na rafiki wa faida ile yeye kajikita kutumia maarifa yake kiuhalifu (wadukuzi) huyu atashusha thamani kiuhalisia.

Kwa kutumia muda mwingi ukiwa peke yako , unaweza kukaa sehemu tulivu, hii itakusaidia kujitambua zaidi na kukuongezea maono juu ya mambo mbalimbali uliyofanya na unayotarajia kufanya.Vipe nafasi hekima na busara ndani ya mwili wako. Kupitia hivi utaweza kutafakari ni mambo yapi mazuri na yapi si mazuri pamoja na kukujengea tabia ya kusema hapana au ndio kwa jambo lolote litakalokukabili.

Kwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kufatilia afya yako, kumbuka kuzingatia mazoezi ni muhimu kwa afya ya akili pamoja na kufatilia afya yako ili kuhakikisha upo imara zaidi. Watu wengi hatuzingatii masuala kama haya hadi umri ukienda ndio akumbushwe na daktari kufanya mazoezi na kufatilia afya yake. Hivyo ili uwe mtu wa maarifa unapaswa kuzingatia haya.

Kwa kupenda kufundisha wenzako, hii ni sawa na kuyafanya kwa vitendo maarifa (ujuzi) uliyoyapata kwa kusoma au njia nyingine. Tutajuaje kama unajua kitu fulani ? , basi kupitia kutenda tutafahamu uwezo wako na pia utajiimarisha vizuri na kuelewa zaidi. Baadhi ya watu hudai mtu anayefundisha huelewa zaidi kuliko anayefundishwa. Fundisha watu zaidi kadri uwezavyo hakuna mtu anayejua mambo mbalimbali na akaacha kuelewesha au kutoa ushauri ila yule anayedai anajua ila hafundishi wenzake basi huyo hajiamini na kakariri.

Matokeo yake.
Baada ya kujifunza mambo mbalimbali utajiona ni mtu wa tofauti ndani ya familia hadi jamii (kujitambua zaidi). Utakuwa ni mtu muhimu katika utatuzi wa changamoto zitokeazo miongoni mwenu, utakuwa ni mtu wa kuigwa na mwalimu wa jamii kiujumla. Upeo wa kufikiri utaongezeka kwa sababu ya wingi wa maarifa uliyonayo, utakuwa mwepesi wa kufikiri na kung'a ua mambo madogo na makubwa kwa usahihi.
images (9).jpeg

(Picha kutoka mtandaoni)

Mwisho, kuwa mtu wa maarifa inawezekana endapo ukikubali kujifunza na kujijengea tabia ya kufatilia mambo yenye tija. Tunajifunza mambo mengi sana hasa katika jamii na pia tunakumbana na changamoto nyingi sana. Changamoto hizi zinatatuliwa kwa kuwa na maarifa hata wewe huo uwezo unao bila kujali umri. Kuanzia sasa kuwa mtu wa maarifa kwa kupenda kujifunza mambo yatokeayo ndani na nje ya jamii yako. Anza sasa unaweza
 
Upvote 6
Vijana wa maana kama hawa ni adimu sana tanzania , si kwa ubaya ila siku moja moja tembelea kenya utakutana na waaina yako kibao.
 
Vijana wa maana kama hawa ni adimu sana tanzania , si kwa ubaya ila siku moja moja tembelea kenya utakutana na waaina yako kibao.
Ni kweli mkuu, ila kuwa na hulka ya kujifunza inasaidia sanaa ila niliikomaza wakati nasoma kozi ya maktaba. Vijana tunapaswa tubadilike na tukibadilika kizazi nacho kitakuwa katika eneo zuri.
 
Kama hujaweka bhangi uzi wako utakua batili, Bhangi inaongeza maarifa,ubunifu na uwezo wa kufikiri
 
Back
Top Bottom