Nataka kuwa Tajiri kupitia Barber Shop

Kuna watu ni mabingwa wa kukatisha wenzao tamaa! Kumbe hata wao hawana chochote cha maana!
Mkuu wewe piga kazi! Anza mdogo mdogo, ndoto zako zitatimia tu!
Hata mbuyu ulianza kama mchicha!
 
Amesema akimaliza chuo atafungua biashara ya kinyozi.

Huko chuoni anasomea nini?
KAsema yupo chuo kwa hiyo anataka kufanya akiwa bado chuo. Wewe ndo akili ndogo unashindwa hata kuelewa kilichoandikwa. Bora hata ana akili ya kuwekeza bumu lake. Wengine wanaishia kulewa tu pesa yote na kula mikate kama panya semester nzima:biggrin1:
 
Nenda kwa shigongo atakupa management ya kuwa na ukwasi
 
Fungua saluni usijali hata kama kwenye huo mtaa zipo 1000, baharesa asingefungua azam tv kwa sababu tu vituo vya tv vipo Vingi au mengi tajiri mwenzake alishakuwa nayo tangu 1994.

..... Achievers don't do different things, they do things differently.
 
Pambana... nimenunua IST mwanzoni mwa mwaka huu kwa biashara hiyo..
Zangu nimezitega kila kona ya mji...
Unamtaji mkubwa sana dogo!
 
Nilishawahi kuwa na ndoto ya kuwa na chain of barbershops kama ilivyo mac donald's. Sijui ilipotea wap
 
Napiga Advanced Dip ya education

Ni vizuri sana kujiajiri mkuu!,Lakini kwa ww ambae upo chuo unasomea Education na maswala ya kuwa kinyozi wapi na wapi?,kwa mantiki hii Tanzania yetu tutapata walimu wanakuwa vinyozi na vinyozi wanakuwa walimu na madaktari wanakuwa mapolisi na mapolisi wanakuwa madaktari na hata watu waliosomea ufundi garage wanakuwa Madiwani!
 
Mkuu,jaribu kupeleleza soko la kinyozi eneo unalo taka kufanyia kazi.
Kama inalipa,anza kwa ujasiri wote... Siri ya kufanikiwa kiuchumi ni kuto bagua kazi.
 

Kumbe kweli watoyo wa matajiri wapuuzi eenh Mtoto Tajiri
 
Last edited by a moderator:
haha,sio kwamba mie ndio nitakuwa kinyozi,ila nitamuweka mtu afanye kazi kisha atakuwa ana niletea hesabu tu
 
nita anza na moja then nitafungua nyingine nikiona napata faida nzuri..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…