Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

inaonekana umzoefu kwenye haya mambo, unaweza kunisaidia ni yako????
 
Jamaa kakupa wazo zuri sana. Yani kama mimi naweza sema anza na mtaji wa 5mln kabisa. Ukiwa unaanza biashara kuna mambo mengi sana ya kujifunza, kuna makosa mengine sana unatafanya. Unatakiwa uwe mtu mvumivu na mtu wa kujifunza sana. Uvumulivu unakuja na pesa pia, uwe na pesa ya kwamba ukikosea unaweza anza tena. Ukigawa mtaji wako kwa 5mln utakuwa na chansi 4, ukifeli mara ya kwanza, una chansi ya pili, ukifeli tena unachansi ya tatu, mpaka ukifika mara ya 4 angalau unakuwa umekomaa.

Mtu yoyote asikuvunje moyo hapa.
 

Thubutu hata siku moja usithubutu kutumia ma AGENT utalia kilio cha samaki.

Ushahuri mbovu kabisa huu.
 
Bora umeongea
Agent lazima ale cha juu
Lazima akuletee usichotaka
Kipindi naanza kuuza spea za pikipiki katoro Geita rafiki yangu aliniunganisha na jamaa mmoja ambaye ni mzoefu wa kiagiza kutoka Dar.
Aliandaa oda ya 5ml na kesho yake nikaingiza pesa kwenye akaunti ya benki na nyingine M-pesa kwa kuwa yalikuwa ni makampuni 3 tofauti.
Baada ya siku 3 mzigo ukafika kama tulivyoandika oda na nikaanza biashara na jamaa nikampa posho ya elfu 50 kwa msaada wake.
Alahaula! Kumbe bora ningenunulia mzigo palepale katoro kwenye maduka ya jumla au ningepanda basi kwenda mwenyewe. Kuikweli NILIPIGWA VIBAYA. Laki 5 na 72 elfu ilipigwa kwa kugawanyisha mzigo kwenye ufungaji. Siku zinashuka box zangu na yeye zika shuka zake kumbe zimetoka kwenye hela yangu bila mimi kufahamu.
Kilichokuja kunitoa usingizini baada ya mwezi mzima kuna kampuni moja wapo iliambatanisha invoice copy. Bei tuloagizia ni tofauti na bei halisi ya Dar, jamaa alizidisha kwangu ila oda halisi ilikuwa na bei ya chini na ndio maana mzigo aliugawanya ili ufungwe tofauti. Nilichoka hoi.
Nilishukuru Mungu kwakuwa sikupigwa pesa yote na mzigo ulifika japo kwa gharama ya juu na faida kidogo. Nilimuuliza jamaa akakosa cha kujibu.
Potea njia wakati wa kwenda ila kurudi wewe ni mwenyeji. Nilifanya juu chini nikapata namba za makampuni husika tena kutoka kwenye simu yake bila ya yeye kufahamu. Alishangaa tu kuona mizigo inatiririka kutoka Dar. MWANZO MGUMU.
 
Dar noma sana,jamaa alikufanya fursa.
 
ndo usenge wa kufanya kazi na wabongo, lazma akupige ndio ajiskie amani. Uaminifu 0 ndio maana hata wakidakwa viwanja huwa ni deport tu haina msalia mtume...kufumba na kufumbua uko Kipawa
 
ndo usenge wa kufanya kazi na wabongo, lazma akupige ndio ajiskie amani. Uaminifu 0 ndio maana hata wakidakwa viwanja huwa ni deport tu haina msalia mtume...kufumba na kufumbua uko Kipawa
Hahah kipawa moja hio.
 
ndo usenge wa kufanya kazi na wabongo, lazma akupige ndio ajiskie amani. Uaminifu 0 ndio maana hata wakidakwa viwanja huwa ni deport tu haina msalia mtume...kufumba na kufumbua uko Kipawa
Siwezi kutuma mzigo kabla yakufika kule nakujionea soko likoje
 
Hayo ndo mawazo yakujenga tunayoyataka, shukuran
 
Naku(Pm) namba za mchina ( yuko china kiwandani) anadeal na accessories ukichati nae muulize bei ya accessories unazohitaji anaweza pia kukupa mwongozo wa simu unazohitaji
utagundua mtaji wako ni mkubwa mno tena
Naamini utaharakisha zaidi safari yako

All the best mkuu..!

Nauza simu na accessories
 
Mkuu Kama Hutojali PM Na Hiyo Number Kwangu Pia
 
Mimi pia kaka km hutojali ni pmhizo namba
 
A You are the best
 
Huu ni ufinyu wa akili, kuna gharama za kujifunza, kwa mara ya kwanza anaweza asipate faida kubwa lkn kujifunza ni muhim sana katika biashara Ticket na malaxi China sio gharama kubwa
Sasa hiyo TZS 20 million ukitoa ticket na malazi unabakiwa na nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…