Nakushauri uende china kwasababu vitu ni bei nafuu sana na utapata idea ya vtu vingne pia
mimi naish huku ila sio guangzhou so nilipata nafasi ya kwenda kutembea guangzhou mwaka jana mwanzon
vitu vya kuwasaidia kwa experience na uelewa wangu kama atakae kuwa anajua zaid atanisahihisha
ticket mm za bei nafuu kabisa huwa nakata STA travels posta karibu na shule ya mtendeni jengo moja na Takims safaris n tours
hapo huwa napata ticket kuanzia laki 7 na ktu one way ya kwenda guangzhou ila ukate mwez kabla
kwa guangzhou inategemea sasa kama unakwenda kwaajili ya canton fair nakushauri ukae (wansheng wei) ni karibu sana na Canton na kama unataka kukaa mbal na maeneo waafrika waliojazana ...hio sehemu ni nafuu kwa hostels sio hoteli lkn hostels ni nzur sana ....anyway since ni mgeni hio sehemu inaweza ikawa mtihan kdogo hivyo waweza kaa (sanyuanli ) hapa kuna hoteli nying na za bei ya chini sana utapata chumba hadi cha elfu ishirini na ktu kupanda ila hadhi ya chumba ni kulingana na hela unayoilipia ...advantage ya hapa upo karibu na soko la nywele ..vipodoz ..na nguo ..walking distance na migahawa ya kiafrika ...pia soko la cm halipo mbali
kuna xiaobei ...hii ni kama posta ya guangzhou pia unaweza pata hotel nzur za kuanzia elfu 50 hv 40 kupanda ...advantage upo karibu na masoko
sasa basi una save vipi gharama zisizo za msingi
cha kwanza ...uwe na mwenyej ...wapo watu wanafanya io kaz ya kutembeza watu masokoni ila kwa experience yangu Wazanzibari wana bei ndogo sana kuliko wabongo ....mm nlimlipa mzenj elfu 70 kwa siku 3 kunitembeza masokon wakat wabongo wanataka hadi dollar 100 kwa siku
ishu ya pili ...ya kusave pesa guangzhou ni kununua chakula kwenye migahawa ya wachina (waislamu ) halal restaurants chakula ni close na chetu na nikizur kwa bei chee ...starting price ni elfu 4 hv wakat restaurant za kiafrika vyakula sahan had elfu 30 huko inafika
njia nyingne ya kusave hela guangzhou punguza matumiz ya taxi ...usafr wa gharama ndogo ni Treni ya underground (metro ) hii hadi airport mpaka hotel unayokwenda unaweza unganisha ukalilipa buku 3 au nne na ni umbali tuseme kimara mpaka mbagala hv wakat umbali huo taxi unalipa hadi elfu 60 hv
kingne chochote unachotaman kununua hakikisha upo kwenye soko sahihi ndio utapata bei nzur usione tu kiduka kinauza cm ukadhan ni bei nzur hapana nenda kwenye soko halisi la hio bidhaa utapata bei nzur
kingine ukifika sokon take your time zunguka kabla kufanya maamuz maana bei ni tofaut na wauzaj ni weng sana ...ukipanda taxi hakikisha unatoa pesa kamili .maana madereva taxi huwa wanatoa chenj hela feki sometimes ....usimwamini mtu na mizigo yako ..matapel weng hata waafrika
View attachment 1328791View attachment 1328793View attachment 1328794
mtaj huo 20m unatosha kabisa just go kila lakheri
Sent from my iPhone using JamiiForums